Manispaa ya Kahama itakuwa kama Jiji la Mwanza miaka 10-15 ijayo

Acha uongo wewe nyegezi hadi Nyamuhongolo ni kama 20km haifik 30km. Ukipita ile bypass ya usagara hadi kisesa ile sio shortcut?
Sijaongelea bypass ya kisesa usagara kumbe hata mwanza huijui zaidi ya kukariri tu, nimesema labda shirtcut ya buhongwa adi igoma kupitia kishiri ndio inaweza kuwa 20+ km, lakin kwa mzunguko tu ni zaidi ya 30+ km.... Ngoj nikuache uendelee kupuyanga na ubishi, na hii yote kwasababu ya wivu wa kwanini Mwanza inastendi mbili.
 
Wewe unamawazo finyu kweli mimi Mwanza ni nyumbani Nyegezi kona pale ila sina ukabila au ukanda kama wewe.
 
Ni ukweli usiopingika miji miwili hii ya Kanda ya Ziwa inakuwa kwa kasi sana Jiji la Mwanza na Manispaa ya Kahama. Lakini kasi ya ukuaji na maendeleo ya Manispaa ya Kahama inaleta projection ya kuwa Kama Jiji la Mwanza baada ya miaka 10 ikichelewa miaka 15..

Mwaka 2002 nilifanikiwa kufika Wilaya ya Kahama, ikiitwa Halmashauri ya wilaya ya Kahama ikiwa na eneo kubwa la utawala lakini mji ukiwa mdogo sana. Eneo la mji ilikuwa ni Nyihogo, Uhindini, Malunga, Mungura(kidogo) , Majengo (padogo) na Nyasubi ndo walikuwa wanaanza kugawa viwanja na kujenga. Mhongolo, Igomelo, Masaki, Phantom, Mbulu nk kote hapakuwepo.

Baadaye mabadiliko na maendeleo yakaanza, mji ukapewa hadhi ya mji mdogo, haikuchukuwa muda ikapandishwa hadhi ya kuwa Halmashauri ya mji, na sasa miaka mitatu sasa ni Halmashauri ya Manispaa.

Mwaka 2003 nilifanikiwa kufika Mwanza. Kiwango cha Maendeleo ya Mwanza ya miaka hiyo ndiyo maendeleo ya Kahama ya leo. Mwaka huo 2003 stand katika mji wa Mwanza ilikuwa mjini katikati--- Sahara. Na Barabara ya lami iliishia Mkuyuni. Mwaka huo huo 2003 mwishoni ikawa inaanzishwa stand ya Nyegezi. Maeneo ya Mkolani na Buhongwa hayakuwa na watu. Wakati stand inaanzishwa pale Nyegezi watu walilalamika na kufoka kwa kupelekwa porini na kwenye mivumbi.

Kwa kasi inayoonekana Manispaa ya Kahama kwa watu kuongezeka kwa kuhamia, kuzaliana, mzunguko wa biashara na pesa, maghorofa kujengwa kama uyoga nk. Kuna uwezekano mkubwa Mwanza ya leo 2023 ikawa Kahama ya 2033 au 2038. Jiji la Mwanza miaka hiyo sijui itakuwa kama miji gani ya leo.

Changamoto iliyopo kwenye miji hii ni kukosa kuzingatiwa (upendeleo) support kubwa kutoka Serikalini. Imagine jiji lile la Mwanza hakuna University hata moja ya serikali. Barabara za njia nne hakuna ukiacha Ile ya Ilemela tu, hakuna hospital kubwa ya rufaa ya serikali (Ile ya Bugando ina mkono na mguu wa Wanatoloki).

Ebu imagine jiji la Mwanza, serikali itupie na kujenga Chuo Kikuu Kama UDOM na hospital nyingine kama Mloganzila au Benjamin Mkapa.... ? Ebu fikiria barabara ya kutoka Usagara hadi Mjini iwe njia nne au sita na Ile ya mjini hadi Kisesa iwe nayo njia nne. ..... Wakati huo huo pata picha zile barabara za Kahama mjini zote zipigwe lami, na serikali ipeleke miradi pale hata Chuo cha VETA tu!!! Hapa nasema kuwa maendeleo makubwa ya jiji la Mwanza na Manispaa ya Kahama mengi ni wananchi/wafanyabiashara. Serikali ikipeleka miradi kadhaa miji hiyo, tutaijua vzr lake zone. Hongerni wana Kahama na Wana Mwanza.
Vimji vya hovyo kama magulio ya mifugo hakuna kitu Cha maana huko ni mlundikano wa watu mafukara tuu kwenye Miji yote 2.
 
Hao wasukuma wa kanda ya ziwa wako serious kusaka pesa,hiyo miji ongezea na katoro ya geita ni miji ya kumake money.
Kwanza kadiri maeneo mengi ya Nchi yanavyozidi kufunguliwa na kufika Kwa miundombinu aina mbalimbali,inazaliwa Miji mipya na pia uhamiaji kwenye Miji mikubwa unapungua matokeo yake hiyo Miji mnayoitaja Kwa Sasa haiwezi kukua Kwa Kasi ya awali.
 
Yes kahamaa..maendeleo ni hatua...now days kwa Tanzania situation n the same..kubwa n watanzania esp vijana wamebadilika sn kimawazo kuhusu kujenga..sahv ukienda hata vijiji vya ndani ndani hko unakuta kijana amejenga.hii inapelekea miji kutanuka...kifupi nchi imefunguka..hta hapo kaham Kuna Sehem sahv mnaona mapori...give it miaka 5 utanambiaa..watu wanaongezeka na vijana wamechamgamkaa....chamuhim vijana tuamke tuu
 
Kwani kupeleka chuo cha serikari na hospital ndio maendeleo. Mbona mwanza kitambo imeendelea bila hivyo . Kuna uhusiano gani chuo cha serikari na maendeleo
Tens hakukuwa na barabara ya lami inayounganisha na mikoa mingine zaidi ya barabara ya Mwanza - Musoma / Sirari ambayo iliishia Nyanguge lakini Mwanza iliendelea fresh tu wakati mikoa mingine ilikuwa inateseka
 
Ni ukweli usiopingika miji miwili hii ya Kanda ya Ziwa inakuwa kwa kasi sana Jiji la Mwanza na Manispaa ya Kahama. Lakini kasi ya ukuaji na maendeleo ya Manispaa ya Kahama inaleta projection ya kuwa Kama Jiji la Mwanza baada ya miaka 10 ikichelewa miaka 15..

Mwaka 2002 nilifanikiwa kufika Wilaya ya Kahama, ikiitwa Halmashauri ya wilaya ya Kahama ikiwa na eneo kubwa la utawala lakini mji ukiwa mdogo sana. Eneo la mji ilikuwa ni Nyihogo, Uhindini, Malunga, Mungura(kidogo) , Majengo (padogo) na Nyasubi ndo walikuwa wanaanza kugawa viwanja na kujenga. Mhongolo, Igomelo, Masaki, Phantom, Mbulu nk kote hapakuwepo.

Baadaye mabadiliko na maendeleo yakaanza, mji ukapewa hadhi ya mji mdogo, haikuchukuwa muda ikapandishwa hadhi ya kuwa Halmashauri ya mji, na sasa miaka mitatu sasa ni Halmashauri ya Manispaa.

Mwaka 2003 nilifanikiwa kufika Mwanza. Kiwango cha Maendeleo ya Mwanza ya miaka hiyo ndiyo maendeleo ya Kahama ya leo. Mwaka huo 2003 stand katika mji wa Mwanza ilikuwa mjini katikati--- Sahara. Na Barabara ya lami iliishia Mkuyuni. Mwaka huo huo 2003 mwishoni ikawa inaanzishwa stand ya Nyegezi. Maeneo ya Mkolani na Buhongwa hayakuwa na watu. Wakati stand inaanzishwa pale Nyegezi watu walilalamika na kufoka kwa kupelekwa porini na kwenye mivumbi.

Kwa kasi inayoonekana Manispaa ya Kahama kwa watu kuongezeka kwa kuhamia, kuzaliana, mzunguko wa biashara na pesa, maghorofa kujengwa kama uyoga nk. Kuna uwezekano mkubwa Mwanza ya leo 2023 ikawa Kahama ya 2033 au 2038. Jiji la Mwanza miaka hiyo sijui itakuwa kama miji gani ya leo.

Changamoto iliyopo kwenye miji hii ni kukosa kuzingatiwa (upendeleo) support kubwa kutoka Serikalini. Imagine jiji lile la Mwanza hakuna University hata moja ya serikali. Barabara za njia nne hakuna ukiacha Ile ya Ilemela tu, hakuna hospital kubwa ya rufaa ya serikali (Ile ya Bugando ina mkono na mguu wa Wanatoloki).

Ebu imagine jiji la Mwanza, serikali itupie na kujenga Chuo Kikuu Kama UDOM na hospital nyingine kama Mloganzila au Benjamin Mkapa.... ? Ebu fikiria barabara ya kutoka Usagara hadi Mjini iwe njia nne au sita na Ile ya mjini hadi Kisesa iwe nayo njia nne. ..... Wakati huo huo pata picha zile barabara za Kahama mjini zote zipigwe lami, na serikali ipeleke miradi pale hata Chuo cha VETA tu!!! Hapa nasema kuwa maendeleo makubwa ya jiji la Mwanza na Manispaa ya Kahama mengi ni wananchi/wafanyabiashara. Serikali ikipeleka miradi kadhaa miji hiyo, tutaijua vzr lake zone. Hongerni wana Kahama na Wana Mwanza.
Sawa kabisa ila kumbuka mji mdogo wa Katoro wilayani Geita unakuwa kwa kasi kuliko hata hiyo Kahama. Miaka kumi ijayo Katoro itakuwa mji mkubwa sana.
 
Ni kweli, uko sahihi kuwa Katoro inakua. Lkn haimaanishi kuwa Kahama inashindana na Katoro. Maeneo mengi nchini yanakua
 
Kinachoshangaza huo mji mdogo wa Katoro hata Katibu Tarafa hayupo, wala mkuu wa Wilaya lakini jinsi unavyokwenda kasi inashangaza sana.
Ndiyo changamoto ya miji ya Kanda ya Ziwa, maendeleo mengi ya miji iliyopo Kanda ya Ziwa, serikali imewekeza kidogo sana
 
Back
Top Bottom