Manispaa ya Mwanza kuna watu hawajui Kiswahili washindwa kuelewana na makarani wa sensa

Manispaa ya Mwanza kuna watu hawajui Kiswahili washindwa kuelewana na makarani wa sensa

Mdukuzii

JF-Expert Member
Joined
Jun 27, 2022
Posts
2,552
Reaction score
6,422
Nimecheka sana ITV karne hii kuna watu hawajui Kiswahili.

Karani wa sensa amekuwa katika wakati mgumu leo kuelewana na mwananchi.

Kila akiulizwa anajibu nahene jawiza mayo. Hapo ni Kisesa, ndani ya manispaa kabisa; nauli 600 kwenda mjini, sio kijijini.
 
Nimecheka sana ITV karne hii kuna watu hawajui kiswahili
Karani wa sensa amekuwa katika wakati mgumu leo kuelewana na mwananchi..
Kwa hiyo huyo karani siyo mzawa wa Mwanza aliwezaje kupata hiyo nafasi wakati hajui lugha ya mawasiliano mahala anapoenda kufanya sensa ..

Hao jamaa wamefanya makusudi kwa kuwaa ajira za sensa hazikuzingatia wanufaika wa maeneo husika.

Wala siyo la Kushangaa bali tujishangae sisi kumchukuwa Mtu kutoka Kigoma kwenda kufanya kazi ya Ukarani usukumani tena kwenye Eneo ambalo hajawahi kulikanga wala kuishi maeneo husika
 
Apambane na hali yake[emoji1787][emoji1787] tena bora KWA wasukuma anaweza akaelewa hata neno moja moja [emoji1787]angekua KWA wabaya ndio angejua hajui
 
Umeambiwa waliopata Sensa wote ni wazawa wa maeneo hayo?kuna watumishi wa umma ambao wanafanya KAZI maeneo tofauti na walikozaliwa ulitaka waende kuombea kwao?
ulimaikiliza Mama Anna Makinda vizuri kuwa makarani watatoka wap[i wa maeneo husika... huku nilipo kati makarani 27 watatu ndiyo wakaazi wa eneo husika
 
Tuanzie hapo kwanza, hakuna Manispaa ya Mwanza, kuna jiji la Mwanza ambalo lipo wilaya ya Nyamagana na kuna Manispaa ya Ilemela ambayo ipo wilaya ya Ilemela. Na Kisesa ipo wilaya ya Magu japokuwa wakazi wa pale wameji-attach sana upande wa jiji

Sensa inahusisha watu wote waliolala kwenye kaya usiku wa kuamkia tarehe 23 August hivyo kama kuna mgeni anahesabiwa pia hivyo sio wote waliopo mjini ni wa mjini na sio wote waliopo kijijini ni wa kijijini.
 
Usiseme manispaa Sema manispaa ya jiji
Unajua ulichokiandika. Manispaa ya Jiji no kitu Gani.?

Halmashauri zina level tofautofaut
Halmashauri ya wilya
Halmashauri ya mji

Halmashauri ya manispaa
Halmashauri ya Jiji
Kuna hadi halmashauri za mji mdogo, kijiji etc

Kwa kifupi hakuna manispaa yaa jiji
 
Mleta muda kisesa n Kama kijijini tu mkuu nenda kule bujora ndiyo utajua nachoongea kisesa ipo magu mkuu

Halafu hakuna ubaya wala aibu mtu kuongea lugha yake mama
 
Kwa hiyo huyo karani siyo mzawa wa Mwanza aliwezaje kupata hiyo nafasi wakati hajui lugha ya mawasiliano mahala anapoenda kufanya sensa ..

Hao jamaa wamefanya makusudi kwa kuwaa ajora za sensa hazikuzingatia wanufaika wa maeneo husika.

Wala siyo la Kushangaa bali tujishangae sisi kumchukuwa Mtu kutoka Kigoma kwenda kufanya kazi ya Ukarani usukumani tena kwenye Eneo ambalo hajawahi kulikanga wala kuishi maeneo husika
Hao makarani walitoka mbeya. Waliyofanya interview na walioitiwa kazi ni tofauti
 
Kwenye zoezi la utambuzi Mara zote zingatia kuweka watu wanaoendana na jamii husika.

Wakati wa maombi yakazi iltakiwa kuwa na kuthibisha kuwa muombaji ni mkazi wa eneo husika, anajua lugha na tabia za wakazi husika, anaheshimu mila na miongozo ya Ile jamii.

Kama karani hawezi kuwasiliana na Kaya husika inamana hakuandaliwa kuwa mkamilifu.

Siku mwisho tume ya send itakuwa na 28% timamu ya watu walihesabiwa wengine itakuwa n taarifa fake
 
Back
Top Bottom