HOJA Manispaa ya Ubungo, LATRA na Jeshi la polisi usalama barabarani ondoeni bajaji njia kuu za Bunju na Morogoro road

HOJA Manispaa ya Ubungo, LATRA na Jeshi la polisi usalama barabarani ondoeni bajaji njia kuu za Bunju na Morogoro road

Hoja ya Mdau inayopendekeza maboresho au mabadiliko ndani ya jamii, inayotakiwa kuangakiwa kwa mapana na Mamlaka husika

N'yadikwa

JF-Expert Member
Joined
Aug 10, 2014
Posts
8,308
Reaction score
12,812

Wadau, hili jambo limekuwa kero kubwa kwa watumiaji wa barabara maeneo Bagamoyo Road na Morogoro Road.​

Idadi kubwa ya bajaji zinazoingia na kufanya shughuli kwenye barabara kuu, hasa maeneo yenye msongamano mkubwa wa magari, imekuwa ikichangia usumbufu kwa watumiaji wengine wa barabara.

Tatizo si uwepo wa bajaji kama chombo cha usafiri bali ni mahali zinapotumika na namna zinavyosimama, kupakia na kushusha abiria.

Katika baadhi ya maeneo, bajaji zinaonekana kusimama ovyo, kuingia na kutoka kwenye njia za magari bila mpangilio, kupakia abiria kandokando ya barabara na wakati mwingine kufanya U-turn au kusubiri abiria kwenye maeneo ambayo si salama. Hali hii inaweza kuongeza msongamano na hatari ya ajali.

Rai yangu kwa mamlaka husika:​

1. Manispaa ya Ubungo isimamie matumizi ya barabara na vituo vya bajaji katika maeneo yake na itenge maeneo maalumu ya kupakia na kushusha abiria ambayo sio mainroad kama Morogoro Road.

2. LATRA ihakikishe bajaji zinafanya kazi kwenye maeneo na njia zinazoruhusiwa na ichunguze kama idadi na route zilizopo zinaendana na mpangilio wa usafiri wa maeneo husika.

3. Jeshi la Polisi – Kikosi cha Usalama Barabarani lichukue hatua za kudhibiti bajaji zinazozuia mtiririko wa magari, kusimama maeneo yasiyoruhusiwa au kufanya vitendo vinavyohatarisha usalama wa watumiaji wengine wa barabara.

Kuna foleni ndefu za muda mrefu sana Dar es Salaam ambazo ni za kujitakia.

4. Mamlaka zisishughulikie bajaji moja moja tu; ziangalie mfumo mzima. Kama wananchi wanahitaji usafiri wa karibu, basi wawekwe utaratibu wa bajaji kutumia service roads, vituo maalumu au njia za ndani, badala ya kuzifanya barabara kuu kuwa vituo vya kusubiria abiria.

Barabara ya Morogoro tayari inabeba mzigo mkubwa wa magari na abiria. Hivyo, kila kinachoweza kupunguza mtiririko wa magari kinapaswa kudhibitiwa kwa umakini.

Tunaomba mamlaka zifanye ukaguzi wa pamoja Bunju na Morogoro Road na kutuambia: Bajaji zinaruhusiwa kufanya nini kwenye barabara kuu, zinaruhusiwa kusimama wapi, na ni hatua gani zinachukuliwa dhidi ya wanaokiuka?

Tukidhibiti uholela wa ubebaji wa abiria kwa kutumia kila chombo bila utaratibu hata tujenge barabara vipi foleni zitaendelea kututesa. Hapa tuweke siasa pembeni.
 
Back
Top Bottom