Manji aliamsha dude; ameahirisha safari ya Yanga kesho kwa gari, watasafiri kwa ndege


Hakuna kitu kama hicho wala ukweli wowote hapo ila kinachofanyika sasa ni Yanga ' kujipendekeza ' kwa Manji ili ' kumshawishi ' arejee Yanga na anayefanya / anayeratibu huu ' upuuzi ' wote ni Katibu Mkuu wa Yanga Mkwasa na Mtangazaji wa ' hovyo hovyo ' wa Efm na mwana Yanga ' lia lia ' kabisa Maulid Kitenge.

Kadri uzi huu utakavyokuwa unaendelea mbele nitakuja kuelezea ' kiundani ' kabisa tabia za huyo Kijana Kushoto Kwako pichani ambaye ni ' Komandoo ' wa Yanga SC aitwae Carlos Ze Don kisha ndipo mtajua ni kwaninu huwa anapenda sana ' kujikombakomba ' kwa Manji.

Carlos Ze Don ameacha historia ya aibu sana Visiwani Zanzibar hasa kipindi kile cha mashindano ya Kombe la Mapinduzi ambapo alichofanyiwa na Wazanzibari kilimfanya hadi ' azimie ' kabisa na akawahishwa jijini Dar es Salaam kwa matibabu ' maalum ' na nakumbuka alikaa karibia miezi miwili hatoki ndani na anakwepa Watu.

Ukitaka kujua kama Manji amerudi Yanga au hapana mtafuteni jibu ambalo Nahodha wa ' kulazimisha ' wa Yanga SC Nadir Haroub ' Cannavaro ' kisha awaambieni jibu ambalo Manji alimpa siku ile Kesi yake ikifikia kikomo pale Kisutu ila ninachojua ni kwamba Manji alimwambia Cannavaro kwamba kwa sasa anaomba wamuache kwani ' amechanganyikiwa, amerudishwa nyuma na anataka kujipanga upya kiuchumi ' ila akawaelekeza waende kwa ' Tajiri ' mmoja mwenye Ofisi zake jirani na Benki ya Kizalendo pale Posta ili awasaidie kwa sasa. Na Manji hakumuacha hivi hivi Cannavaro ambapo alimuuliza Swali ambalo lilimfanya Cannavaro ainame chini kwa aibu na kushindwa kulijibu ambapo alimuuliza kwamba inakuwaje wakati wote wa Kesi alikuwa hawaoni pale Kisutu kumuunga mkono ila sasa ameshinda Kesi ndiyo wanajifanya kumkumbuka na kuwa karibu nae?

Wana Yanga mtawadanganya wasio na akili humu ila kwa Sisi Wajanja wa mjini / Watoto wa mjini na tunaojua michezo yote ya hatari na Siasa zetu hizi za Simba na Yanga wala hamuwezi kutupata. Manji wala hana haja tena na Yanga SC na hafikirii tena kuwasaidieni ila semeni tu ukweli kwamba kuna Waziri wenu mmoja wa Wizara ' Nyeti ' ambaye anawapenda Yanga kuliko hata wale Watu ' wasiojulikana ' ndiyo amewashawawishi Marafiki zake kadhaa ' matajiri ' wenye mahaba na Yanga ndipo ' wamejichanga ' jana mchana na leo Timu ikaondoka na Ndege kwenda ' Kufungwa ' huko Kagera na Shinyanga.

Endeleeni kuwadanganya ' wajinga wajinga ' ila Manji ameshajivua rasmi Yanga SC.

Nimemaliza.
 
Mkuu ile barua ya FIFA uliyo tuambia imetumwa kupitia DHL vp? tunataka point zetu 3 na ubingwa
 
Manji is back mkuu! ... ...
 
Mkuu ile barua ya FIFA uliyo tuambia imetumwa kupitia DHL vp? tunataka point zetu 3 na ubingwa

Acha Ujinga / Ungumbaru suala lililopo mezani sasa ni hili la Manji kurudi na kuisaidia Yanga SC na jinsi linavyopotoshwa na akina Mkwasa na Kitenge kwa ' maslahi ' yao na ' kujipendekeza ' Kwao Kwake.
 
Hivi unafahamu surerity wa dhamana ya Manji au unaonge ongea tuu?
 
Acha Ujinga / Ungumbaru suala lililopo mezani sasa ni hili la Manji kurudi na kuisaidia Yanga SC na jinsi linavyopotoshwa na akina Mkwasa na Kitenge kwa ' maslahi ' yao na ' kujipendekeza ' Kwao Kwake.
tutakuamini vp tena kma kule kwenye DHL uli tuingiza chaka?
 
Manji is back mkuu! ... ...

Endelea ' Kudanganywa ' na ' Kudanganyika ' hivyo hivyo. We hushangai na hujiulizi swali kuwa Mimi ni mwana Msimbazi tena wa ' Kindakindaki ' kabisa lakini nayajua ya ndani kabisa ya Yanga SC kuliko hata Wewe na hao Yanga wenzako? Mtafute Nahodha Nadiri Haroub ' Cannavaro ' atakupa zaidi ya haya niliyoyaweka hapa na asipokuambia au akikukwepa rudi tena hapa Kwangu nikuelekeze mahala pengine ambapo utapata ' taarifa ' sahihi kabisa.
 
Mchakato wa hisa unaendeleaje?
 
Tutakurudia kumbe bado anawashwa!!! Hiyo Timu itakuponza wewe jifanye tu hamnazo kama MURO.mwenzako ni msemaji wa ccm-academia
 
Jibu hoja,mkuu Gentamycene,acha kutapa tapa

Na ndiyo maana ' matahaira ' wengi wanaopatikana nchini Tanzania wana Mapenzi / Ushabiki na Yanga SC. Simba SC kumejaa ' Majiniasi ' tupu na ndiyo maana unaona sasa tunaenda vizuri na karibia tu na Sisi tutakuwa kama TP Mazembe au Liverpool FC au FC Barcelona au AC Milan au PSG au Kaizer Chiefs au Asante Kotoko au Canon Sports au Enyimba FC au Zamaleck FC ' Kimaendeleo ' na kuwaacheni nyie mkijikombakomba kwa ' Panjuani ' Manji.
 
Naona vyuma vimekaza.
 
Magu ni kiongozi mchoyo. Anawachukia ssna matajiri. Hajui kama matajiri ni moja ya chachu ya maendeleo.
 
Daaaah, masikinii, yanga inatia huruma sana aisee!!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…