Manji amuokoa Komba, anunua shule zake

Manji amuokoa Komba, anunua shule zake

Manji kamuokoa mzinzi huyo


Sent from my iPad Air using JamiiForums mobile app
 
mkuu nimecheka sana, eti mzee wa msituni hawezi kufungwa, ashukuru manji tu manake ccm wenzake walishamtosa.

sintashangaa baadae shule zikakabidhiwa ccm au akarudishiwa komba si mnakumbuka momose cheyo naye alikopa benki nyumba ikapigwa mnada akanunua manji lakini baadae mzee ben akamuagiza manji amrudishie cheyo na akairidisha toka muda huo cheyo mtiifu kwa ccm vilevile ccm haiwezi kusahau kirahisi fadhila za komba na msishangae komba akatoa wimbo wa kampeni muda si mrefu na akalazimishwa kuifufua na kuitumikia bendi ya chama
 
Jamani kama mtu hujui sheria ni vizuri ukaepuka ku-comment kisheria. Tangu lini kesi ya madai ikampeleka mtu jela.

Mwenyewe hiyo sheria hujui, kesi ya madai mtu anaenda jela kama kawa, anaenda as civil prisoner ingawaje utaratibu ni tofauti kidogo na kesi za jinai rejea civil procedure Act
 
Sakata la mali za John Komba kupigwa mnada kufuatia deni la Tsh bilion 1.2 analodaiwa na benki ya CRDB limefikia tamati baada ya mfanyabiashara nguli na Mwenyekiti wa klabu ya Yanga, Bw Yusuf Manji, kununua shule na baadhi ya mali zake zote ambazo zilikuwa zipigwe mnada ili kufidia deni.

Komba alikuwa anakabiliwa na uwezekano wa shule zake kupigwa mnada (na kufungwa jela) ili kufidia deni hilo alilokopa CRDB miaka 5 iliyopita.

Source: Mwananchi.

MAONI YANGU
Komba amshukuru sana Manji kwa kumuokoa kwenda jela na kupigwa mnada kwa mali zake. Sipati picha kama Komba angefungwa jela kile kitambi chake angekificha wapi. Lazima kingenywea kama puto lililotoboka. Hivi alidhani kuendesha shule ni sawa na kuimba kwaya na kusimamia bendi? Chezea mkopo wewe!

Ulimwengu wa Ccm, ukiwa kwenye sytem unapeta tu. Kufungwa hufungwi kufilisiwa hufilisiwi
 
Tena hapo bado uswaiba umetumika sana,ilitakiwa ziwe zimepigwa mnada siku nyingi ila Kimei akaweka uswaiba akavuta muda mpaka mdhamini manji alipotokea
 
ni sheria gani inayoruhusu mdaiwa kufungwa?

Sheria ya mwenendo wa makosa ya MADAI inaruhusu cheki section na order zinazohusiana na kaza hukumu ambapo mdaiwa akishindwa kulipa deni moja kati ya mbinu ni kwa mdai kuiomba mahakama imfunge mdaiwa kama civil prisoner na kifungo hakizidi miezi sita na mdai humlipia gharama za kukaa gerezani mdaiwa bt kifungo hakifuti deni na kinaweza kujirudia lakini si zaidi ya mara tatu YOU CAN SAVE YOURSELF BY FILING MAOMBI YA KUWA DECLARED INSOLVENT
 
Kitambi cha Komba ndio mtaji wa chama Twawala.....Hahaha.... Komba ni mzigo ktk chama.....
 
Jamani kama mtu hujui sheria ni vizuri ukaepuka ku-comment kisheria. Tangu lini kesi ya madai ikampeleka mtu jela.

angefungwa jela kwa kuidanganya benki. aliidanganya crdb kwamba mali zake zina thamani zaidi ya fedha alizokopa huku akijua kwamba hata angeuza mali zake zote hadi ubunge haufiki hata nusu ya fedha anazodaiwa (Tsh1.2 billion).
 
Jamani mimi sijaelewa vizuri hapa mnaposema Manji amemuokoa Komba ni katika misingi ipi?

Kama shule ndo hivyo imeshakwenda na Manji the same as ingekwenda na CRDB, au bei aliyopewa na Manji ni kubwa kuliko deni la CRDB hivyo anabaki na chenji? Hebu nielewesheni ameokoka vipi?
 
Mkuu inaonyesha hata ww sio mdau wa sheria au km ni mdau basi mzembe coz umeshindwa kufahamu kuwa kesi ya madai inamfunga mtu...NOTE. Kesi ya madai mdaiwa anafungwa na mdai anatakiwa kumlipia mdaiwa gharama za matumizi pindi atakapokua jela...
 
Back
Top Bottom