Manji kuzikwa Marekani kumedhihirisha kiwango kikubwa cha ujinga. Tuna safari ndefu kama nchi katika katiba na elimu ya uraia

Mkuu, salama lakini.

Ila hao wazee Hayati Mwalimu aliidhinisha wapewe diplomatic passport za dharura ndo wakawa wazitumia.

Hizo zaweza kurudishwa wakati wowote.

Hati za dharura uhamiaji wanazo.

Nchi karibu zote duniani wanazo.
 
Mkuu, salama lakini.

Ila hao wazee Hayati Mwalimu aliidhinisha wapewe diplomatic passport za dharura ndo wakawa wazitumia.

Hizo zaweza kurudishwa wakati wowote.

..salama mkuu.

..sikujua kwamba walipewa PASI ZA KIDIPLOMASIA / DIPLOMATIC PASSPORT.

..mimi nilidhani ni pasi za kawaida tu hizi tunazotumia hata walalahoi.
 
Fahamu kwamba unaweza kupata passport ya kusafiria ya Marekani bila kuwa raia wa Marekani.
 
Wana hoja wahindi wengi sio wazalendo,wako huku kuchuma tu ila wana passport au nasaba ,mapenzi na nchi zingine,wahindi sio watu wa kuwaamini
Wanaotuibia na kutuuza kila siku kwa bei waitakayo wao ni raia wa nchi gani? Wana passport ya taifa gani?
Wananzengo tuamke. Tumekuwa mafala kupitiliza. Kuwa na passport mbili au tatu au nne havina uhusiano na uzalendo.
Tena Manji mwenye passport mbili au tatu inawezekana alisaidia watanzania wengi kuliko hawa wezi uchwara wanaoiba na kuficha pesa zetu kwenye mabenki huko nje.

Bottom line, passport zaidi ya moja ni kutafuta security na predictability kwenye daily life. Mara nyingi havina uhusiano na uzalendo.
 
Ulikuwa na nafasi nzuri ya kutoa elimu ya uraia lkn haujafanya hivyo ukidhani elimu inatolewa darasini tu.Tz bado tunayo safari ndefu kweli kweli.
 
Sasa kuliko kuponda tu mwanzo mwisho si ungetoa elimu hata kwa ufupi tu angalao ambao hawajui wajue
 
Ana hoja nzr asipuuzwe
 
Mkuu umeshawahi kupata experience ya kuishi inje ya inchi?
Ukajifunza vitu..
Lazima uelewe kwamba binadamu sio mbuzi au mifugo kwamba unaweza ukajichukulia sheria unavyotaka.

Passport uliyonayo i ni identification kwamba wewe ni nani,,
Na unatokea wp?

So ni lazima ubalozi husika ujulishwe na maamuzi yafanyike kwamba mtu wako atapelekwa wp?

Ukiona mtu anazikwa popote kule elewa balozi imeridhia au ni raia wa hapo..
Wacha kushupaza shingo mkuu..

98% ya wahindi matajiri na waarabu sio raia wa Tanzania.
Wengi wana duo Citizens
 
Kumleta Tanzania gharama ni kubwa
 
Nimekuwa nikitafakari vp wasomali wana exposure kubwa sana duniani. Kwa mfano nimepata taarifa moja imeniimoress sana. Wasomali wamezaliwa tz, lkn kwasasa familia hiyo haipo tena tz. Wachache wako Zambia, watoto wengine wako uk, us, Canada na belgium.

Nikajiuliza kwanini nasi tusipigie hatua tuwafikia wao. Kinyume chake tuishi kwa kusubiri siku yetu ya kufa.

Tukubali kama vile akili ya walio wengi hawataki kurudi vijijini kwao na hiyari wabaki dar na kubangaiza na vibarua. Hivyo hivyo tukipata bahati kuondoka nje ya mipaka. Wengi watakataa kurudi tz. Dunia iko diverse jamani.

Gen Z inawahusu zaidi
 

Kwani suala la mtu kuzikwa sehemu huangaliwa uraia, kama ni hivyo basi hizi sheria zilizo tungwa na binadamu za kijinga sana. Mtu akifa sehemu fulani azikwe huko huko, mambo ya kusafirisha maiti huonyesha ujinga wa watu.
 
We unadhani ccm wanatumia nguvu kubwa kutawala bongo
 
You nailed it mkuu..
Mimi nilibaki kusikitika.
Na inashangaza wengine nilipitia profile zao wamejiwekea wasifu bachelor.....
Ndio hii sample inayowakilisha watz wengi zaidi
 
Umetumia njia rahisi sana kutaka wewe pia ufundishwe kupitia comment maana hujui pia. Hakuna elimu ya bure
 
Sikusoma shule za kujazana ujinga za "Swahili medium". Kuandika na kusoma Kiswahili kwa kiwango kikubwa nimejifundisha hapa Jf
Ni kama Nyerere, alipokuja Dar ndiyo wazee wa Dar wakamfundisha Kiswahili.

Unalo?
Nyerere alipofika DSM kwanza hakuaa katika vijiwe vya jahawa, hakuambukizwa uvivu, uswahili na umwinyi, mambo ambayo mpaka leo ni mzigo uswahilini huku.

Nyerere alishuka toka Pugu kuwakomboa kwanza waswahili kwa kuishi pamoja nao Magomeni. With new radical thinking, waswahili WAKAMCHAGUA kuwaongoza!
Upo hapo?
 
Kuzikwa wapi haijalishi cha muhimu ukiwa hai uweze kutafuta pesa kwa ajili ya familia yako. Kuzikwa hata mwezini unaweza kupelekwa huko na kufukiwa iwapo pesa ya kufanya hivyo unayo.

Wahindi na waarabu ni wahangaikaji wa miaka na miaka wanalelewa wakifundishwa nidhamu za kimaisha ambazo sisi waafrika hatuna. Wanajua maana ya umoja ni nguvu sisi tunaishia kurogana na kuumizana wenyewe kwa wenyewe halafu akifa Manji tunahisi kupata muda wa kuwasimanga wahindi!.

Tubadilike kwanza sisi wenyewe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…