Manji: TFF na BMT wanafanya njama jina langu likatwe ili nisigombee Yanga, nina ushahidi wa sauti

Manji: TFF na BMT wanafanya njama jina langu likatwe ili nisigombee Yanga, nina ushahidi wa sauti

MWENYEKITI wa Yanga, Yussuf Manji amechukua fomu za kutetea nafasi yake makao makuu ya klabu, Jangwani, Dar es Salaam leo na kudai kwamba kuna njama zinafanywa na baadhi ya watu ndani ya Baraza la Michezo la Taifa (BMT) na Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) wakate jina lake.

Akizungumza na Waandishi wa Habari leo mchana Jangwani, Manji alidai kwamba alileta mpelelezi kutoka nje ya nchi akanasa mbinu hizo chafu hadi ushahidi wa sauti anao.
Akasema katika sauti hizo wanasikika baadhi ya wanachama wa Yanga wakipanga njama kwa kushirikiana na watu wa TFF na BMT ili kukata jina lake katika uchaguzi.

Akasema na hiyo ndiyo sababu hawana imani na TFF kuendesha uchaguzi wao na akasistiza Yanga itafanya yenyewe uchaguzi wake, tu kwa kusimamiwa na TFF.



Manji akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani. Kulia ni Makamu wake, Clement Sanga



Manji akizungumza na Waandishi wa Habari leo makao makuu ya klabu, Jangwani. Kulia ni Makamu wake, Clement Sanga



Manji akizungumza faragha na Makamu wake, Clement Sanga

Pamoja na hayo, Manji ambaye aliwasikilizisha Waandishi wa Habari na wanachama waliokuwapo sauti hizo, akatangaza kumfuta uanachama, mwanachama ambaye sauti yake imevuma zaidi kwenye rekodi hiyo, Msumi.

“Mimi kama Mwenyekiti wa Yanga, natangaza kumfuta uanachama Msumi, ataitwa Kamati ya Maadili kujieleza. Na pia natangaza kuwafuta wanachama wale wote ambao sauti zao zimo humu,”amesema Manji.

Pamoja na hayo, Manji akamuagiza Ofisa Habari wa klabu, Jerry Muro kupeleka sauti hizo Jeshi la Polisi Tanzania kwa ajili ya uchunguzi zaidi na awe anatoa taarifa kila wiki kulingana na mwendelezo wa uchunguzi.

Aidha, Manji akasema anawafuta uanachama walke wote ambao wamechukua fomu za kugombea Yanga TFF.

Manji akasema kwamba Yanga inachukiwa na TFF kwa misimamo yake, ikiwemo kukataa baadhi ya mikataba ya Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara, ambayo inainyonya klabu hiyo.

Akadai na kwa sababu hiyo TFF wanafanya jitihada yeye aondoke Yanga ili wapate urahisi wa kupitisha Mikataba isiyo na maslahi na klabu.
“Sisi tumetaka kujenga Uwanja wetu hapa (Jangwani), lakini tumehangaika na hatujapata sapoti yoyote ya TFF,”amesema.

Manji akadai japokuwa watu wanalalamika Yanga inabebwa na TFF, lakini ukweli ni kwamba klabu hiyo inaonewa.

“Tunapangiwa ratiba ngumu, tunacheza mechi bila kupumzika, wanataka Yanga ifungwe, ili Manji aambiwe ondoka, lakini tumechukua ubingwa, makombe yote, na Azam kabebwa ashiriki Kombe la Shirikisho,”amesema.

“Tumewasaidia (Azam) ndugu zetu, si vibaya, lakini tulikuwa tuna uwezo wa kucheza mashindano yote ya Afrika. Ligi ya Mabingwa na Kombe la Shirikisho, ila kanuni haziruhusu,”amesema.

Mvutano umeibuka kuhusu uchaguzi wa Yanga SC ambayo sasa inawaacha njia panda wanachaa wa klabu hiyo, wakiwa hawajui washike lipi baada ya TFF kutangaza na kuendesha mchakato wa uchaguzi wa klabu hiyo - wakati huo huo Yanga nayo ikitangaza na kuendesha mchakato yenyewe wa uchaguzi wake.

Yanga imesema uchaguzi wake Yanga utafanyika Juni 11 na si Juni 25. TFF imenza kutoa fomu za kugombea Yanga mapema wiki hii, wakati klabu hiyo leo nayo imeanza kutoa fomu na Manji amekuwa mtu wa kwanza kuchukua, akifuatiwa na Makamu wake, Clement Sanga waliyekwenda pamoja.

Waliochukua fomu TFF ni Aaron Nyanda, Titus Osoro wanaowania nafasi ya Makamu Mwenyekiti, Paschal Laizer, Edgar Chibula, Mohammed Mattaka, Mchafu Ahmed Chakoma, Bakari Malima ‘Jembe Ulaya’ Omari Said kutoka Zanzibar wanaowania Ujumbe wa Kamati ya Utendaji


Heee, kumbe YANGA upo mgogoro, anayebisha basi ataona matokeo yake...ngoja niishie hapa...lakini sina hakika kama kasi ya serikali ya awamu ya tano inaendana na kasi hii ya YANGA, tusubiri tuone...I smell a rat...
 
Seriously nataka kujua mpaka anafikia stage ya ku hire private investigator na ku rekodi mazungumzo binafsi (sheria hapa imekaaje) ili tu apate uongozi Yanga.


Hapa ndipo ulipogusa, there is a problem somewhere, tutasikia mengi katika hili...nakwambia there is something wrong somewhere...
 
Seriously nataka kujua mpaka anafikia stage ya ku hire private investigator na ku rekodi mazungumzo binafsi (sheria hapa imekaaje) ili tu apate uongozi Yanga.
Manji ni mfanyabiashara mkubwa hapa Tanzania so usishangae yeye kuwa na mlinzi kutoka nje,unakumbuka yule jamaa wa Home Shoping Centre alivyomwagiwa tindikali ?
 
Seriously nataka kujua mpaka anafikia stage ya ku hire private investigator na ku rekodi mazungumzo binafsi (sheria hapa imekaaje) ili tu apate uongozi Yanga.
Kwa upeo wangu mdogo naona kama kaingilia faragha za watu.
 
Mi nashangaa Tff kupanga uchaguzi Yanga mbona klabu zipo nyingi hawaitishi uchaguzi huko. Ndio mara ya kwanza kusikia tff kusikia wakishinikiza uchaguzi
 
Katiba ya yanga inasemaje kuhusu ukomo Wa vipindi vya uongoz kwa mwenyekiti...

Hili swali nasikia wahindi weusi Wa yanga hawataki kulisikia
 
Seriously nataka kujua mpaka anafikia stage ya ku hire private investigator na ku rekodi mazungumzo binafsi (sheria hapa imekaaje) ili tu apate uongozi Yanga.

Sio apate yeye ndio kiongozi halali sasa kwanini mpitie njia ya mkato kumtoa. Anakodi private investigator na mbona amekodi mpaka kocha wa kufundisha Yanga hukuuliza?
 
Yalishasemwa haya, Yanga uchaguzi ulitakiwa kufanyika zamani badala ya Manji kuendelea kuitawala klabu kwa ujanja ujanja ilihali hana mpinzani wa kumsumbua.

Kutokufanyika uchaguzi kwa muda mwafaka ni kukaribisha matatizo yasiyo ya lazima kwa kuwa kuna wengine wanatamani kuwa viongozi hata kama hawawezi kuwa na mafanikio zaidi ya haya, lakini ni kuwapa nafasi wapinzani wako maana ni kujidanganya kuwa Manji anapendwa na watu wote pale Yanga.
 
kati ya yote namuunga mkono kukataa mikataba ya kinyonyaji ya TFF lakini hajaeleza baada ya kukataa amefanya nini
Huyu mtu yanga watakuja kumchukia sana kwani muda wote ambao amekuwa kiongozi pamoja na kutengeneza migogoro ya kikatiba bado hajaiwezesha yanga kujitegemea na utumbuaji wa majipu wa Magufuli sasa hivi atakimbia yanga ndipo yanga itakapoanza kugeuka opmbaomba
 
Mimi napenda sana simba hila kwa hili TFF wanataka yanga kuingia kwenye migogoro halafu sura za waliochukua fomu wote hali wanataka kupiga hela...
 
Back
Top Bottom