Manka: Dada Poa maarufu Dodoma Aliyetekwa na kutoonekana kwa miaka 3 sasa

Hii hata mimi nilifuatilia kuhusu kupotea kwa wauza simu wa China Plaza, nikaja kugundua jamaa walikuwa wanadili na simu za wizi nyingine kutoka nje huko, zikiingia Bongo zinabadilishwa IMEI kisha zinauzwa, pia walikuwa na biashara zao za magendo na walishakamatwa mara kadhaa na kuachiwa

Pia kuna askari walikuwa wakitafuta iPhone 16 ikawa inaonekana imezimia maeneo ya Aggrey wakamtaiti dogo na wakamwonyesha picha za watu waliowapoteza na dogo wote anawafahamu

Dogo akawajibu, "MMOJA AINGIE NDANI KISHA MMOJA AI-RING SIMU IKIITA OFISINI KWANGU NIKAMATENI MIMI"

Jamaa wakamshangaa mbona anajiamini sana, akawajibu, "KWA SABABU SIMU YENYEWE TANGU ITOKE SIJAWAHI KUIONA NA SIJUI INAFANANAJE PIA HUYO FUNDI MWENYEWE WA KUFLASH SIMU HAJAINGIA PIA HUMU NDANI KUNA CAMERA ILE PALE INAREKODI MATUKIO YOTE"

Siku hii ndo nikaamini kweli jamaa wanahusika kupoteza watu haswa wale wanaojua kabisa wakikamatwa watatoka hivyo wanaamua kumalizana nao wenyewe tu
 
Hii ndio Tanzania. Napenda sana watu wanavyofanya kazi hawalali usiku na mchana ili nchi ibaki salama.
Ulinzi wa raia na mali zao.
Kuwa raia mwema.
 
Nilichojifunza, kuwa raia mwema, tii sheria bila kushurutishwa, acha kiherehere, ukionywa sikia na utulie, ukijifanya mjanja sana, wapo wajanja zaidi...

Nchi inahitaji amani na utulivu
 

Pole zake Manka. Pole zake Paroko. Dawa za kuchanjia ili usikamatwe ukiiba zinafeli...kama gari linaloshindwa kupanda mlima ana kuanza kurudi nyuma kwa speed kali, ndio unavyokuwa mwisho wake
 
Mwenye picha ya paroko tafadhali. Na yeye tumuone.
 
ZINGATIA SANA HAPA 👉🏾 "Manka aliambiwa amkanye bwana wake Paroko kuhusu hiyo tabia ya wizi wa pikipi ila Manka aliishia kuwatukana watu na pia Paroko alitembeza mapanga kwa wote alioona wanamfatilia kwenye ishu zake". 🙏🙏
 
Ukiishi maisha ya hovyo tegemea mambo ya hovyo yatakukuta. Vitu ambavyo amefanya vimetia najisi maisha yake ulinzi wa MUNGU ukatoweka hakukuwa na ulinzi wa MUNGU katika maisha yake.

Ukahaba,kuishi na mhalifu,wizi,dhuruma,ufitini,uongo,tamaa,hivyo vote huvuta matatizo katika maisha ya mwanadamu. Na ukikaa na mtu mwenye hivi vitu madhara yake hata wewe yatakuhusu na utadhurika tu iwe isiwe.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…