Manka: Dada Poa maarufu Dodoma Aliyetekwa na kutoonekana kwa miaka 3 sasa

Sinerio inaonyesha hao ni majambazi sugu, manka anatumwa akodi bodaboda halafu anamlebgeshea paroko, naye paroko anamaliza kazi, Watu wengi tu ni wezi na majambazi ispokuwa huwa wanajificha pahala, mfano kwenye siasa, au biashara za hapa na pale, kuzugia na kufichia ujambazi wao!
 
Snitching Ina gharama yake!!

Ishu za maendeleo pekee zinaweza pelekea kuchukiwa na jamii!!mfano waliochakachua fedha za imma kwenye ujenzi ukifichua TU wanaaanza kukuzingua!!

Kuhusu manka aliji expose sana Kwa hai jamaa pia anahusika na kumlinda jambazi hizo zinatosha kabisa kukuharibia coz jeshi la polisi halipendi kuharibiwa image yake!!

Ishu ya Bhangi na polisi Hilo ni eneo lao la kujipatia mishe pia ni biashara za wakubwa Hawa was chini ni supplier TU wazito wapo juu!!!

Angebadili identity tu kwenye jamii!!
 
Ila
Bora uibe pesa za umma mabillion Kwa mabillion kuliko kumuibia mlalahoi mwenzako million ya mkopo na kumua kabisa au kumwachia ulemavu
Ila wewe akili hauna kumbe hujui hizo mabilioni ndio pesa za walalahoi ili watoke huko kwenye hoi hadi hai?!! Unadhan mabilioni ni pesa ya rais kama masisiemu wanavyogamba!!
 
Wewe ndo huna akili kabisa na umri wako utakuwa mdogo hujawahi kutafuta chochote siku ukiwa mkubwa na ukiingia kwenye game ya utafutaji utanielewa
 
kukosekana kwa Utawala wa sheria kwa kuwafanywa wengine kuwa juu ya sheria ni tatizo sugu kwenye nchi yetu, Ndio moja ya sababu kubwa inayosababisha kuzidi kwa uhalifu mana kila mtu anaamini anaweza kufanya tukio na isiwe kitu.
 
Natumaini mko powa wanajukwaa hili la JF (JamiiAfrica)

Leo tarehe 05/05/2025 imetimia siku 1075 au miaka 3 kasoro tangu dada maarufu kwa jina la Manka (Sauda jina la kuzaliwa) apotee kwa kutekwa na watu wasiojulikana katika mazingira ya kutatanisha yeye pamoja na bwana wake aitwaye Paroko.

Fuatana nami hadi mwisho wa kisa hiki.

Ilikuwa ni siku ya Jumatano tarehe 26/05/2022 saa 4 asubuhi ndipo watu walipogundua Manka hayupo chumbani kwake.
Manka, dada maarufu aliyekuwa anajiuza mitaa ya Chako ni Chako huku akiwa amepanga chumba mitaa ya Chang'ombe Extension huku akiishi na bwana yake aliyejulikana kwa jina la Paroko.

Paroko, 'mchinjaji' wa pikipiki za wizi Dodoma alikuwa akishirikiana na vijana wa kihuni toka mitaa ya Hazina, Chang'ombe pamoja na Majengo katika kazi zake hizo za kihalifu.

Manka aliambiwa amkanye bwana wake Paroko kuhusu hiyo tabia ya wizi wa pikipi ila Manka aliishia kuwatukana watu na pia Paroko alitembeza mapanga kwa wote alioona wanamfatilia kwenye ishu zake.

Jinsi alivyopotea.
Siku ya Jumanne 25/05/2022 mchana ilikuja gari dogo jeupe ikiwa na wanaume 3 ikimuulizia Manka, wapangaji wenzake wakawajibu kuwa Manka hayupo, kisha gari ikaondoka.

Siku iliyofuata yaani Jumatano ya tarehe 26/05/2022 wapangaji wenzake na Manka waliamua kumpigia simu mama yake Manka aliyekuwa anaishi Nkuhungu wakimueleza kuwa usiku wa jana (Jumanne) kulitokea purukushani kwenye chumba cha mtoto wake Manka na mpaka sasa hawamuoni hivo aje haraka.

Mama mtu alichukua pikipiki mpaka Chang'ombe kwa mwanae maana alipata wasiwasi pia.

Mama Manka alipofika, yeye pamoja na wapangaji wenzake na Manka waliamua kwenda kwenye chumba cha Manka ila cha ajabu walikuta geti la mlangoni limerudishiwa tu ila halijalokiwa na mlango wa mbao wa ndani ni kama umevunjwa kitasa na uko wazi pia.

Walipoingia ndani walikuta vipisi viwili vya bangi kitandani, kibiriti pamoja na pakti moja ya sigara.

Walipoangalia upande wa kwenye jiko la gesi walikuta hotpot iliyokuwa na ugali ndani yake pamoja na mchuzi na samaki kwenye sufuria wakiwa wameharibika.

Na ukutani karibu na mlango wa kutokea nje kulikuwa na alama ya mkono wenye damu yaani ni kama kuburuzwa na damu au kwa namna hiyo.

Ikabidi wapige simu polisi, na polisi walipofika eneo la tukio na pia katika kuchukua maelezo ndipo wapangaji wakasema kuwa siku ya Jumanne ilikuja gari dogo jeupe mchana kumuulizia Manka na ilipomkosa ikaondoka.

Na siku hiyohiyo ya Jumanne saa 9 usiku ilikuja tena gari dogo ila jeusi na walishuka wanaume 4 mmoja akiwa kavaa 'kinyago' cha kufunika uso na kwenda moja kwa moja kwenye chumba cha Manka na walipogundua yupo ndani wale watu wakaanza kuvunja mlango polepole.
Waliendelea kusema kuwa wapangaji 2 ilibidi watoke nje ili kwenda kumsaidia Manka maana kulianza kusikika kelele za kuomba msaada toka kwa Manka na bwana ake Paroko, ila walipojaribu kusogea mlangoni kwa Manka waliambiwa na wale watu kuwa watawabeba na wao hvo warudi ndani haraka.
Hvo wapangaji wale wakaingia ndani kimya na kufunga milango.

Watu wale wakafanikiwa kumchukua Manka na bwana wake Paroko, wakawaingiza kwenye gari na kupotea nao jumla mpaka leo.

Maswali yakabaki kwa raia.
🔹️Je, wako wapi Manka na bwana ake Paroko? Wako hai au ndio hivo wameshamalizwa?

🔹️ Je, ujambazi wa Paroko ndio umesababisha kupotezwa kwao au kuna namna ingine?

🔹️ Au alilengwa mmoja aidha Manka au Paroko ila waliokuja waliamua kuwamaliza wote kwa kuwa watekaji walijulikana?

🔹️ Manka alikuwa na tabia ya kupeleka habari/ukuda wa baadhi ya askari 'information' kwa wakubwa zao bila kuogopa, je hii pia ilichangia kupotezwa?

🔹️ Manka alikuwa na ujasiri wa kuamka asubuhi na kwenda polisi kuwataja wauza bangi au unga wa mtaani kwao na hata kuwataja askari wanaopokea pesa za malaya au za wauza gongo Je hii nayo ndio sababu?

🔹️ Manka alikuwa anafika mpaka ofisi za kwa mkuu wa mkoa wa Dodoma au Central Police ili kuwachongea dadapoa wenzake kuwa wafungwe jela.

🔹️ Paroko alikuwa ni mkimya sana na mpole, ila ukiingia kwenye 18 zake jua umeisha.

Mpaka leo ni miaka takribani 3 si mwili wa Manka wala wa Paroko uliopatikana.
Ndugu wa pande zote wamefuatilia mpaka wameamua kunyoosha mikono juu na kumwachia Mungu.

Tujifunze kuishi vizuri na watu. Tusiwe ma-snich kwa namna moja ama ingine na pia kuacha tabia ya kuiba au kupora mali za watu. Hujui watu wamehangaika kiasi gani ili kupata hizo mali.

Hapo kuna mkanganyiko kwani haijulikani ni nani hasa kawateka kutokana na kuwatendea ubaya makundi 3.
Dadapoa wenzake, Askari, Wauza unga na bangi au aliokuwa anawaibia 'kazini'

Ogopa sana kumuharibia mtu ugali wake.

Manka ameacha watoto 2
Mmoja wa kiume yuko darasa la kwanza na mwingine wa kike yuko darasa la 7

View attachment 3325357View attachment 3325359View attachment 3325361View attachment 3325362

Wabillahi Tawfiq
Hii Dunia ni ndogo sana tusimwache Mungu aseeee
 
Polisi wana daftari lao ambaro wakifikia mda kesi wajawahi kuweza mahakamani wanacho fanya kukupeleka mahakama ya kuzimu.
Ukiwa mtu wa dili na michongo ndio utajua ili wawe watu wenye itelejensia kali
 
Back
Top Bottom