Asante
JF-Expert Member
- Dec 18, 2009
- 2,086
- 1,081
Inashangaza sana kuitwa Dar es Salaam International trade fair. Ukweli kinachofanyika hapo ni sawasawa na magulio mengi yanayofanyika sehemu mbali mbali hapa nchini, tofauti gulio hili linatoza kiingilio.
International trade fair yeyote ni kualika makampuni, mashirika ya serikali mbalimbali za nje kuja kuona bidhaa za viwandani, mazao mbali mbali kutoka mashambani, mifugo, samaki, madini nk. lakini maonyesho yetu yanaonyesha bidhaa za nchi nyingine na kutumia fursa hiyo kufanya mauzo ya bidhaa zao.
Tunataka bodi inayohudumia gulio hilo watuambie ni order au mikataba ya bidhaa zipi zinazozalishwa hapa nchini zilisainiwa na taifa litauza tani ngapi nje ya nchi na taifa litaingiza kiasi kadhaa cha fedha ya kigeni.
Lakini utashangaa uongozi wa gulio la saba-saba watajivuna mwaka huu wameingiza kiasi fulani cha fedha na kuvuka lengo walilojiwekea.