Ndugu Habari za Muda huu.
Zingatia kichwa cha habari hapo.
Kijana wa mdogo wangu anafuga Sungura, na amedokezwa juu ya biashara ya mkojo wa wanyama hao. Kuwa unahitajika kama Booster kwenye mazao ya Horticulture.
Miundombinu ya Kuteka mkoja huo katika mabanda ya Sungura unaendelea kwa sasa. (Almsot kuisha).
Changamoto aliyonayo ni kuwa afahamu kwa uhakika ni wapi ba nani anayenunua na ni bei gani kwa lita moja, awali tuliambiwa ni 5,000/=TSHS kwa lita moja.
Arusha aliagizwa Tengeru atapata mteja. Lakini pale Tengeru ni nani haswa au ni Taasisi ipi kati ya zile za kilimo zilizoko pale zinafanya biashara hii ndio swali tulokosa jibu.
Ndugu kwa anaefahamu tunaomba msaada ili kijana nae ajikwamue kupitia Fursa hii.
Nawasilisha