Manula huku alikua anatoka wapi?

Manula huku alikua anatoka wapi?

Mgagaa na Upwa

JF-Expert Member
Joined
Sep 30, 2013
Posts
13,481
Reaction score
28,116
Tuweke maaba pembeni,tujibu kwa hoja za kimichezo,kipa jana alikua chini ya kiwango
IMG-20181119-WA0002.jpeg
 
Tuweke maaba pembeni,tujibu kwa hoja za kimichezo,kipa jana alikua chini ya kiwangoView attachment 939165
We jamaa huenda hukuangalia mpira jana..kama uliangalia ili tukio lilikupita...kuna beki mmoja alirudisha mpira nyuma akaupiga vibaya nafikiri sababu uwanja ulikuwa na mchanga mipira ilikuwa haitembei kwa bahati mbaya mpira ukaenda miguuni kwa foward...forward akabaki yeye na kipa..ikabidi kipa atoke ili kubana goli forward akapiga shuti mpira ukakutana na kipa ukamgonga ukarudi hapo ndo kipa alikiwa anarudi sababu alikuwa ametoka kuokoa na asingetoka hilo lilikuwa goli moja kwa moja..inaonesha unachuki zako kwa manulla
 
Kwa hapo Manula alikuwa anarudi baada ya kutuokoa...... kosa ni pale alivopangua kishamba ule mpira uliozaa goli....
Ule mpira haujapanguliwa kishamba kama unavyosema ule mpira ulipigwa vizuri na ulishamzidi kipa sema kuruka ndo bahati akakutana nao....so alivyoupangua bahati mbaya ukawa bado upo uwanjani mtu akaruka kichwa ukapita miguuni mwa mabeki wawili...kwa jinsi ule mpira ulivyopigwa si rahisi kipa ku u control kama watu wanavyofikiria...jamaa anaweza kuwa kweli alikuwa na madhaifu yake but lile goli c la udhaifu
 
Sasa hapo wa kuzomewa ni Manula au huyo Foward aliyekosa mpira ukampita tobo na kukosa goli la wazi kabisa.
 
And ule mpira ulivyopigwa ni zile kona zinazoingiaga zenyewe kilicho msaidia manulla alikuwa kasimama palepale mpira ulipokuwa unaingia so akaruka akawa amekutana nae but hata angefanikiwa kuuokoa ingekuwa kaubahatisha tu...
 
BREAKING NEWS

Picha kama inavyojieleza....emmanuel amunike ndo bas tena
IMG_20181118_141440_663.jpeg
 
We jamaa huenda hukuangalia mpira jana..kama uliangalia ili tukio lilikupita...kuna beki mmoja alirudisha mpira nyuma akaupiga vibaya nafikiri sababu uwanja ulikuwa na mchanga mipira ilikuwa haitembei kwa bahati mbaya mpira ukaenda miguuni kwa foward...forward akabaki yeye na kipa..ikabidi kipa atoke ili kubana goli forward akapiga shuti mpira ukakutana na kipa ukamgonga ukarudi hapo ndo kipa alikiwa anarudi sababu alikuwa ametoka kuokoa na asingetoka hilo lilikuwa goli moja kwa moja..inaonesha unachuki zako kwa manulla
ila mtoa post atakuwa hakuangalia gem
 
Sipati picha mechi ya jana ingefanyika uwanja wa taifa na matokeo ndy kama yale!
Nahisi kamanda mambosasa angekuwa na kazi ya ziada kuwazuia mashabiki wasitoe kipondo kwa team nzima ya taifa

Ova
 
Ila yote kwa yote ule uwanja nao majanga, bora ucheze kwenye kipara hizi nyasi bandia sijui kama ni nzuri in the long run. Kuna krosi ndefu ilipigwa kwa mchezaji wa lesotho ingekua ni nyasi halisi mpira ungedunda ukatoka ila badala yake ukadunda ukatulia mchezaji akauwahi, ni kama kipindi cha pili beki wa stars alivyorudisha mpira kwa kipa sababu ya nyasi kwa kiasi fulani zikachangia speed ya mpira kuwa ndogo isingekua ubinafsi wa mchezaji wa lesotho ilikuwa watupige la pili.
 
Back
Top Bottom