Manunuzi ya Subaru Forester

tztz

JF-Expert Member
Joined
Jun 30, 2021
Posts
274
Reaction score
253
Habari Wana JF Kuna mtu n mtumishi wa umma anataka kuagiza Subaru forester ya 2012 angependa ajue gharama hadi anaiweka mkononi

Pia angependa kujua akipitia process za kuomba msamaaa wa kodi kama mtumishi wa Umma n shingapi atatumia hadi chuma kinamfikia mkononi
 
Huo msamaha wa Kodi Kama mtumishi wa umma sijawah kuusikia.

Wazoefu karibuni .

Extrovert
 
Nimetoka kulipa ushuru juzi tar 24/07/2024 wa Subaru forester XT Kwa kiwango cha Tsh 9,963,499/=
Bado ushuru wa bandarini Tsh 1,200,000/= hii naenda kulipia jumaatatu au jumanne ili nikabidhiwe gari hapa bado BIMA ...

Mwambie huyo jamaa anayeta msamaha wa Kodi eti kwakuwa ni mfanyakazi wa umma ajipange na million 12 baada ya CIF
HII NDIYO TANZANIA
 
Mkuu so jumla hadi anaiweka mkono n shingapi
 
Nlisikia huwaga Kuna msamaha wa kodi kwa watumishi wa Umma ndo nlitaka kujua je kama bado upo ? Na akiuomba hyo gari hadi anaiweka barabarani n shingapi aandae
Nlisikia huwaga Kuna msamaha wa kodi kwa watumishi wa Umma ndo nlitaka kujua je kama bado upo ? Na akiuomba hyo gari hadi anaiweka barabarani n shingapi aandae
Kuna mtumishi wa umma afu kuna shirika/Taasisi ya umma anachanganya mambo
 
Tupende kulipa Kodi kwa maendelea ya Taifa letu.
 
Atakuja kushtuka ili aupate msamaha atatoa chochote kitu na kucheleweshwa juu.
 
Na pia ajue kwamba msamaha upo kwa magari yasiyo na uchakavu wa zaidi ya miaka 8 nafikiri Ina maana atatakiwa aagize gari iliyozalishwa si chini ya mwaka 2017
 
Nlisikia huwaga Kuna msamaha wa kodi kwa watumishi wa Umma ndo nlitaka kujua je kama bado upo ? Na akiuomba hyo gari hadi anaiweka barabarani n shingapi aandae
Wanyakazi wa TPA ndiyo walikuwa wana offa hiyo! Sijui kwa sasa!
Kama sikosei Mwajiri ndiye anawalipia ushuru.
Na ili apate msamaha wa ushuru anakopeshwa Mkopo wa gari na TPA!
Kama mfanyakazi ataamua kujinunulia gari kwa hela yake hapo lazima alipe ushuru.
 
Hivi hii exemption iliwahi kufanyika kwa watumishi wa umma hapo kabla?
 
Msamaha wa kodi kwa mtumishi wa umma upo na ni mara moja tu unaruhusiwa kuingiza gari ya kutembelea na siyo ya biashara.

Kabla ya kuagiza au ukiagiza inabidi uandike barua ya kuomba msamaha wa kodi,usiombe watu wa masijala wakaisahau gari ikifika gharama za storage utazilipa mwenyewe.
 
Hii saizi sidhani kama ipo walianza mwaka jana. Ilikuwa unapewa mkopo wa kununua gari,kusafirisha na bima (CIF) mpaka gari inapofika Tanzania. Ushuru wewe hausiki ni part ya mkopo kuwezesha upate usafiri hata uagize gari ya 2023. Watu walivuta gari za kisasa sana.

Saizi mambo yamebadilika DP world yupo kwenye Management, access itakuwa ya wachache sana
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…