As I know ipo hivi...Msamaha wa Kodi unatolewa kwa gari yoyote unayoitaka kwa Mtumishi wa gari, gari hiyo sifa zake kubwa isizidi cc 3000. Gari hilo litakusaidia ww kukuwahisha kazini na mizunguko yako binafsi.
Msamaha wa Kodi unatolwa kwa mara moja kila baad ya miaka 4. Changamoto ni kuwa hilo gari ukiliuza lazima hiyo Kodi uliyosamehewa ilipwe😀😀
Yaani yule uliyemuuzia akienda TRA kubadilisha kadi ya gari/Jina la umiliki lazima akutane na rungu la TRA, sasa kazi kwako maana kumpa mtu zigo nobody wants, otherwise gari inashikiliwa.
Kingine kwenye msamaha wa Kodi unaweza kuapply mapema kabla hata gari haijafika, cha muhimu n kuwa ukishatumiwa zile documents orijino za Gari lazima uziwalishe TRA kwa uhakiki na approvals.
Mifumo ya utoaji wa msamaha wa Kodi kwa sasa ipo online kwa goods and services...Sasa kwa Mtumishi wa umma nafikiri lazima uwe registered huko na check number yako na credentials na ufanye application online, sidhani kama wanapokea tena makabrasha ya fomu.
La mwisho, usiwe mvivu sana, nenda Ofisi yoyote ya TRA iliyo karibu yako watakupa mwongozo sahihi wa namna ya kupata Msamaha wa Kodi kwa gari utakaloagiza.