Manyanyaso na chuki kazini zimepelekea kuugua ugonjwa wa figo

Habari zenu watanzania wenzangu popote mlipo, mimi nikiwa member hai wa forum napenda kutoa ushuhuda wa manyanyaso kazini yalivyopelekea kuangukia kwenye ugonjwa sugu wa figo.

Mimi ni mfanyakazi wa taasisi fulani serikalini, nimeajiliwa 2007, katika kupata kwangu ajila sikuwahi kufikilia kwamba makazini kuna chuki na manyanyaso yanayotokana na ukabila na muonekano wa mtu,ushirikina na maslai binafsi ya mtu.

Katika maisha yangu ya kuajiliwa sikuwahi kupata furaha ya kazi hii ninayoifanya tofauti na siku ninayopokea mshahara, kazi hii niifanyayo ni kazi ambayo kama mwanao ataajiliwa huku na hukumjengea misingi halali ya upatikanaji wa pesa ni vyema umuambie ajiendeleze kielimu angalau anaweza kupata nafuu.

Mimi baada ya kuajiliwa nikapangiwa huko mikoa ya kanda ya ziwa nikaanza kazi kwa kukaribishwa na manyanyaso ya kikabila, hapa ndipo nikaanza kupata joto la kazi yangu, ebu fikilia kuna kazi ya malipo mazuri ya pesa mezani alafu wewe upo hapo na umeiomba au unaitaji lakini mtu kwa mamlaka yake na kwa kutumia ukabila anampa mtu mwingine ambaye ni kabila lake ambaye anatafutwa akiwa hajui hili wala lile.

Sasa mambo kama haya yamenitokea zaidi ya mara Mia moja na katika nyakati hizo zote moyo wangu ulikuwa unaumia nikiwaza kwa maumivu makali ya moyo kwamba kwanini mimi nanyanyasika hivi, sababu ni muonekano wangu au kabila langu au elimu yangu au nimelogwa, lakini mwisho majibu yakaja kuwa ni ukabila na ushirikina .

Kwa kuwa sikuwa mtu wa kujiongeza niliishi maisha ya dizaini hii kwa miaka mingi huku nikiamini kuwa ni mambo yatakayoisha tu baada ya muda flani,lakini imekuwa ni endelevu mpaka hatma ya mwisho ya mates ya moyo yalipojitokeza.

Nikiwa sifahamu kwa undani elimu ya maradhi ya moyo ambayo kiuhalisia wakati naumia kwa manyanyaso niliyokuwa nayapata nikweli wakati nawaza moyo ulikuwa unaumia sana kwa kusikia kabisa yale maumivu.

Hatma ya yote .mwaka 2024 mwezi wa 4 nikiwa kazini kwangu nikapata habari njema kutoka kwa rafiki yangu kwamba kuna kazi ya pesa ipo nisiondoke, mimi nikakubaliana naye na nikawa naisubilia mpaka jua lilipozama, kitu kilichonitokea usiku ule ni funzo kwa wanangu na wale wote wanaotegemea kupata kwa visivyo halali.

Mimi nilisubiri sana lakini kilichonishangaza ni kuona watu ambao wahusika wa mchongo wakitawanyika mmoja mmoja, mimi nikaona kwamba huu ndio muendelezo wa yaleyale ambayo nayakataa na baada ya kuona hali ile mimi nikaamua kuondoka kurudi nyumbani.

Nikiwa nyumbani nikapigiwa simu na yule aliyenipa ule mchongo kwamba rudi halaka, nikapanda gari nikarudi niliporudi katika kuakikisha kazi ninayotaka kuifanya nikawa najaribu kuwauliza baadhi ya wahusika lakini sikupewa ushirikiano wowote, kilichoniuma zaidi ni baada ya kusikia mtu wangu wa karibu ambaye alinidokeza ishu iyo kwamba wenzake wamechukizwa na kitendo cha kunishirikisha mimi ivyo hata yeye hawezi kuhusishwa tena.

Mimi baada ya kusikia kauli iyo nikaondoka nikiwa na hasira na maumivu makali ya moyo, kwa kuwa usiku mnene ulishaingia sikwenda tena nyumbani, badala yake nikaenda kwa mwanamke fulani ambaye mimi nilikuwa na mahusiano naye lakini nilikuwa nashiriki naye kwa tahadhari na kwa kutumia condom.

Usiku ule nilikwenda kulala kwake na nilishiriki naye bila condom kitu ambacho sio kawaida yangu, nilifanya kama sehemu ya faraja yangu lakini niliishia kwenye stress kubwa ya nadharia ya kuambukizwa ukimwi, baada ya siku iyo ikaja kwamba kabla ya masaa 72 niwe nimempima na nimepima HIV.

Siku iliyofuata nikafanya vipimo mwenyewe na yeye majibu ni NEG, shida ikaja kwamba asubuhi yake nikaenda kuvicheki kama vimebaki kama vilivyo nikakuta kwake inaonyesha mistari mitatu mimi ni uleule mmoja, hapa nilikuwa sina uelewa wa vipimo.

Nilikuwa najitaidi kabla ya masaa 72 niwe nimejua kila kitu, baada ya majibu kuwa vile nikamshirikisha nesi fulani kwa kumtumia picha za vipimo vingine ambavyo tulipima naye usiku wa siku ile ya pili, nesi akasema mbona kama naona mstali kwa mbali hebu njoo na mwenzio, nikamjulisha ila alikuwa mbali ivyo nikaenda mwenyewe tu na kunishauri kwa kuwa muda unaisha ni bora nianzishe tu dawa ile ya ndani ya masaa 72, nikachukua na kukinywa bila kula licha ya kushauriwa lazima niwe nimekula.

Nikiwa na stress ya juu na mapigo ya moyo ya juu nikiwa nimekunywa kidonge ,yule dada akaja nanikamuelekeza aende hospitality akapimwe na alivyokwenda na kupimwa akakutwa hana maambukizi.

Siku mbili baadaye tumbo likaanza kuniuma bila kuharisha ila choo nilikuwa napata kwa shida,sometimes nilikuwa nikienda aja kubwa natoa uteute kama kamasi nyeupe na mkojo nilikuwa nakojoa mara kwa mara, nikanywa dawa mbalimbali nikidhani ni amiba,nikaenda kupima magonjwa yote lakini hakuna kilicholeta unafuu.

Baada ya mwezi nikaanza kukosa usingizi nikama napata mawenge,kukooa wakati nimelala, na maumivu ya kichwa baadaye nikaona miguu inavimba hapo nikaona naitaji kwenda hospitality kubwa,nikaenda na kupimwa na kuelezwa figo zangu hazifanyi kazi kwa ufanisi kwa kuwa damu inaonyesha sumu zipo 130 kwa viwango vyao wenyewe wanajua nikashauriwa nifuate mtindo bora wa kura itanisaidia kupunguza uwezekano wa muendelezo wa ugonjwa.

Sasa katika hali hii niliyonayo ninaamini kwamba kama ningelikuwa na kazi nyingine mfano:UALIMU.nisingepata ugonjwa huu kutokana na nature ya kazi hiyo inatoa nafasi kubwa ya muajiliwa kuwa huru na kufanya shughuli zako nyingine.

Lakini pia napenda kuhitimisha kuwa makazini tupendane hata kinafiki kuna wengi wanapata maradhi kutokana na tabia za viongozi au wafanyakazi wenzako mimi ni mfano wa wahanga waliadhiriwa na ukabila,ukanda,chuki na mambo mengine kazini hasa ukiwa mpole na husiye na makuu na husiye na muonekano wa kuwafuraisha wengine.

Asanteni.
POle sana
 
Pole mno Ila nachojua upendo ni illusion yaani ni nadharia and doesn't exist, anayebisha abishe tuone, hakuna cha upendo wa mzazi ama mtt kwa mzazi yaani what's being done is just exchanging of values aka trading if no values then you become nothing,hata inzi wenyewe Kama huna kidonda ama jalala kwako wanasepa Sasa unadhani binadamu yeye ni nani
Siyo kweli, in fact ukiwa na thamani ndio utachukiwa zaidi. Ofisi niliyopo nimeshuhudia hayo, kuna jamaa ana perform kuliko sisi wote ila kila siku anawekewa vikao afukuzwe kazi!! Ndio unashangaa inakuaje wakati ndio anaipaisha taasisi.
 
Wewe ndio mwenye tatizo, binadamu yeyote ukishakua mtu wa lawama lazima watu wakutenge,
Mwanaume unalalamika badala uchukue hatua
 
Mwanaume unalalamika badala

Wewe ndio mwenye tatizo, binadamu yeyote ukishakua mtu wa lawama lazima watu wakutenge,
Mwanaume unalalamika badala uchukue hatua
Wewe hujui ni namna gani mtu anafikia hatua za kuwa
Wewe ndio mwenye tatizo, binadamu yeyote ukishakua mtu wa lawama lazima watu wakutenge,
Mwanaume unalalamika badala uchukue hatua
Naomba unifunze kuwa na roho mbaya na ya ukatili na kutojali.
 
Chuki makazini haina sababu, watu watakuchukia tu, hata wanaokuzidi kwa kila Hari, wanaweza kukuchukia, Mtu wa, Mungu, mmoja, alinifafanulia hili, akasema, ni, swala LA kiroho, wewe unakuta una roho/spirit nzuri, sasa waliokuzunguka wana evil spirit, mapepo,roho zinaonana! Sasa hayo mapepo yao, yakiiona roho yako nzuri, lazima yazue tafrani! Zitakazojidhilisha kwa matendo ya wazi! Pole sana
Nini solution ya hayo yote Mkuu??..Maana umeongea vitu vya msingi sana..Mtumishi alikuoa ushauri gani tena ??
 
Kwanini usiombe uhamisho huoni km utakufa kwa hiyo ofisi.
shida kubwa sana ni kwamba chuki si za eneo la kazi bali ni jamii fulani au kabila fulani ambao wanaamini kwamba taasisi ni haki yao na wako wengi hivyo kokote uendako utawakuta.
 
Hapo huwezi kuwalaum kwa asilimia 💯 hao wafanya kazi wenzako.
Kitu cha muhimu kwa sasa angalia afya yako na zingatia ushauri wa madaktari. Jisamehe na usamehe hao jamaa zako.
Moja ya majuto ya nafsi yangu juu ya mkasa wangu ni kuwa tusiwafundishe watoto utu na ukalimu bali tuwajaze kutojali na roho ya ukatili na ushirikina juu, nafahamu kwa kuwa yote yamenitokea.

Ukiwa na roho ya ubinadamu utapendwa na watu unaowapa huduma lakini si wale unaofanyanao kazi.
 
Kawaida sana
Ni kweli ni kawaida ila kwangu nimekuja kujua makazini roho nzuri haina nafasi, ni bora kumfunza mwanao roho mbaya ili akapambane na walimwengu kuliko kumfunza utu , ukarimu na upendo kwa imani kuwa utakupeleka peponi.
 
Balaa tupu yaan,kaza mkuu
 
Habari zenu watanzania wenzangu popote mlipo, mimi nikiwa member hai wa forum napenda kutoa ushuhuda wa manyanyaso kazini yalivyopelekea kuangukia kwenye ugonjwa sugu wa figo.

Mimi ni mfanyakazi wa taasisi fulani serikalini, nimeajiliwa 2007, katika kupata kwangu ajila sikuwahi kufikilia kwamba makazini kuna chuki na manyanyaso yanayotokana na ukabila na muonekano wa mtu,ushirikina na maslai binafsi ya mtu.

Katika maisha yangu ya kuajiliwa sikuwahi kupata furaha ya kazi hii ninayoifanya tofauti na siku ninayopokea mshahara, kazi hii niifanyayo ni kazi ambayo kama mwanao ataajiliwa huku na hukumjengea misingi halali ya upatikanaji wa pesa ni vyema umuambie ajiendeleze kielimu angalau anaweza kupata nafuu.

Mimi baada ya kuajiliwa nikapangiwa huko mikoa ya kanda ya ziwa nikaanza kazi kwa kukaribishwa na manyanyaso ya kikabila, hapa ndipo nikaanza kupata joto la kazi yangu, ebu fikilia kuna kazi ya malipo mazuri ya pesa mezani alafu wewe upo hapo na umeiomba au unaitaji lakini mtu kwa mamlaka yake na kwa kutumia ukabila anampa mtu mwingine ambaye ni kabila lake ambaye anatafutwa akiwa hajui hili wala lile.

Sasa mambo kama haya yamenitokea zaidi ya mara Mia moja na katika nyakati hizo zote moyo wangu ulikuwa unaumia nikiwaza kwa maumivu makali ya moyo kwamba kwanini mimi nanyanyasika hivi, sababu ni muonekano wangu au kabila langu au elimu yangu au nimelogwa, lakini mwisho majibu yakaja kuwa ni ukabila na ushirikina .

Kwa kuwa sikuwa mtu wa kujiongeza niliishi maisha ya dizaini hii kwa miaka mingi huku nikiamini kuwa ni mambo yatakayoisha tu baada ya muda flani,lakini imekuwa ni endelevu mpaka hatma ya mwisho ya mates ya moyo yalipojitokeza.

Nikiwa sifahamu kwa undani elimu ya maradhi ya moyo ambayo kiuhalisia wakati naumia kwa manyanyaso niliyokuwa nayapata nikweli wakati nawaza moyo ulikuwa unaumia sana kwa kusikia kabisa yale maumivu.

Hatma ya yote .mwaka 2024 mwezi wa 4 nikiwa kazini kwangu nikapata habari njema kutoka kwa rafiki yangu kwamba kuna kazi ya pesa ipo nisiondoke, mimi nikakubaliana naye na nikawa naisubilia mpaka jua lilipozama, kitu kilichonitokea usiku ule ni funzo kwa wanangu na wale wote wanaotegemea kupata kwa visivyo halali.

Mimi nilisubiri sana lakini kilichonishangaza ni kuona watu ambao wahusika wa mchongo wakitawanyika mmoja mmoja, mimi nikaona kwamba huu ndio muendelezo wa yaleyale ambayo nayakataa na baada ya kuona hali ile mimi nikaamua kuondoka kurudi nyumbani.

Nikiwa nyumbani nikapigiwa simu na yule aliyenipa ule mchongo kwamba rudi halaka, nikapanda gari nikarudi niliporudi katika kuakikisha kazi ninayotaka kuifanya nikawa najaribu kuwauliza baadhi ya wahusika lakini sikupewa ushirikiano wowote, kilichoniuma zaidi ni baada ya kusikia mtu wangu wa karibu ambaye alinidokeza ishu iyo kwamba wenzake wamechukizwa na kitendo cha kunishirikisha mimi ivyo hata yeye hawezi kuhusishwa tena.

Mimi baada ya kusikia kauli iyo nikaondoka nikiwa na hasira na maumivu makali ya moyo, kwa kuwa usiku mnene ulishaingia sikwenda tena nyumbani, badala yake nikaenda kwa mwanamke fulani ambaye mimi nilikuwa na mahusiano naye lakini nilikuwa nashiriki naye kwa tahadhari na kwa kutumia condom.

Usiku ule nilikwenda kulala kwake na nilishiriki naye bila condom kitu ambacho sio kawaida yangu, nilifanya kama sehemu ya faraja yangu lakini niliishia kwenye stress kubwa ya nadharia ya kuambukizwa ukimwi, baada ya siku iyo ikaja kwamba kabla ya masaa 72 niwe nimempima na nimepima HIV.

Siku iliyofuata nikafanya vipimo mwenyewe na yeye majibu ni NEG, shida ikaja kwamba asubuhi yake nikaenda kuvicheki kama vimebaki kama vilivyo nikakuta kwake inaonyesha mistari mitatu mimi ni uleule mmoja, hapa nilikuwa sina uelewa wa vipimo.

Nilikuwa najitaidi kabla ya masaa 72 niwe nimejua kila kitu, baada ya majibu kuwa vile nikamshirikisha nesi fulani kwa kumtumia picha za vipimo vingine ambavyo tulipima naye usiku wa siku ile ya pili, nesi akasema mbona kama naona mstali kwa mbali hebu njoo na mwenzio, nikamjulisha ila alikuwa mbali ivyo nikaenda mwenyewe tu na kunishauri kwa kuwa muda unaisha ni bora nianzishe tu dawa ile ya ndani ya masaa 72, nikachukua na kukinywa bila kula licha ya kushauriwa lazima niwe nimekula.

Nikiwa na stress ya juu na mapigo ya moyo ya juu nikiwa nimekunywa kidonge ,yule dada akaja nanikamuelekeza aende hospitality akapimwe na alivyokwenda na kupimwa akakutwa hana maambukizi.

Siku mbili baadaye tumbo likaanza kuniuma bila kuharisha ila choo nilikuwa napata kwa shida,sometimes nilikuwa nikienda aja kubwa natoa uteute kama kamasi nyeupe na mkojo nilikuwa nakojoa mara kwa mara, nikanywa dawa mbalimbali nikidhani ni amiba,nikaenda kupima magonjwa yote lakini hakuna kilicholeta unafuu.

Baada ya mwezi nikaanza kukosa usingizi nikama napata mawenge,kukooa wakati nimelala, na maumivu ya kichwa baadaye nikaona miguu inavimba hapo nikaona naitaji kwenda hospitality kubwa,nikaenda na kupimwa na kuelezwa figo zangu hazifanyi kazi kwa ufanisi kwa kuwa damu inaonyesha sumu zipo 130 kwa viwango vyao wenyewe wanajua nikashauriwa nifuate mtindo bora wa kura itanisaidia kupunguza uwezekano wa muendelezo wa ugonjwa.

Sasa katika hali hii niliyonayo ninaamini kwamba kama ningelikuwa na kazi nyingine mfano:UALIMU.nisingepata ugonjwa huu kutokana na nature ya kazi hiyo inatoa nafasi kubwa ya muajiliwa kuwa huru na kufanya shughuli zako nyingine.

Lakini pia napenda kuhitimisha kuwa makazini tupendane hata kinafiki kuna wengi wanapata maradhi kutokana na tabia za viongozi au wafanyakazi wenzako mimi ni mfano wa wahanga waliadhiriwa na ukabila,ukanda,chuki na mambo mengine kazini hasa ukiwa mpole na husiye na makuu na husiye na muonekano wa kuwafuraisha wengine.

Asanteni.
Pole ndugu.
Jitahidi kuitafuta furaha ili upunguze msongo wa mawazo. Pili,km umeajiriwa,ukitaka uwe na amani na uhuru wa kazi EPUKA zile kazi za ya kwamba TUMA MAOMBI YA KUANDIKISHA WAPIGA KURA,KUWA MSIMAMIZI WA UCHAGUZI,KUHESABU WATU (SENSA) badala yake wakikuhitaji wakuite wao,utaheshimiwa na kuogopwa sana.
 
Moja ya makosa ninayoyajutia ni hayo lakini changamoto kubwa ya kazi yangu ni ukionekana unajambo unafanya litakalokutoa kwenye utegemezi utaamishwa ili kukuvuruga usiweze kusimamia mambo yako.
 
Mkuu Kwa Asili ya Kazi ya police huwa inakuwa na changamoto , Mimi nimeishi na hawa jamaa miaka mingi Sana ukiwa mtu ambaye haupendi makando kando basi utapata shida.

Rafiki mmoja Mlokole aliamua kuchukua vyumba vyake viwili na kuvifanya kanisa vyumba vya kota

Mara ya mwisho nilimuacha anaumwa na alienda Bugando kutibiwa. FIGO

Kuhusu swala lako , jaribu kuipa Afya yako nafasi maana health is wealth .

Pole Sana .

Love is natural, hatred is taught.
View attachment 3223296
Kwani kasema ni police?
Km ni kweli basi pole yangu kwake nitaenda kuifuta.
Ninao ndugu ambao ni police lkn nikifuatilia visa vyao na matukio ya kiovu wanayo fanya basi huwa ninatamani wote wateketeeee.
 
Moja ya makosa ninayoyajutia ni hayo lakini changamoto kubwa ya kazi yangu ni ukionekana unajambo unafanya litakalokutoa kwenye utegemezi utaamishwa ili kukuvuruga usiweze kusimamia mambo yako.
Kwani ukihamishwa haulipwi sitahiki zako?
 
Back
Top Bottom