Manyanyaso na chuki kazini zimepelekea kuugua ugonjwa wa figo

Naomba unipatie kozi fupi ya kuwa na roho mbaya na ya ukatili, nisiyejali wala kujua ya wengine kwa ufupi nifunze kuwa kama wao kwa kuwa naamini mimi sijajiumba ila naitaji kubadilika niwe zaidi yao.
 
Wewe ndyo uliyeandika barua kwa IGP ya kuacha kazi?
 
- Kuna cha kujifunza hapa, Sawa na kale kamsemo "Kosa fedha ujue tabia ya mkeo"
 
''Toshekeni na mishahara yenu''
Ukiangalia kwa kiasi kikubwa hayo matatizo umejitafutua wewe mwenyewe kiongozi. Hautakiwi kutaka watu wakupokee positive kila mahali, watu wasipokupenda wewe waelewe huo ndio uamuzi wao then wewe endelea na maisha yako.

Fanya kazi zako kwa umakini, epuka majungu na vikundi vinavyosema watu kazini, toa salamu kwa wote ila usijipendekeze. Kuwa muwazi kwenye maamuzi na mtazamo wako usitake kuwaridhisha wengine. Wenyewe tu watakaa kwenye mfumo wako.

Hawatakuchukia, hawatakupenda ila watakuheshimu na kutamani kuwa kama wewe, hivyo ndivyo walivyo wanadamu.

No offense ila nilipoanza kusoma nilihisi ni mdada analalamika, hadi nilipofika hapo ulienda kwa mwanamke ndio nkajua kumbe ni mwamba. Sasa acha malalamiko Mkuu kaza kiume.
 
Hata mimi Mkuu nilijua ni mdada, jamaa analalamika sana. Huwa nikisikia tu mwanaume anasema 'nanyanyaswa/nanyanyasika' huwa sijui namuonaje.
 
Useme tu ni Bukoba ndio kuna ukabila sana hasa wageni wananyanyasika sana.
 
Ni kweli ila tambua binadamu tunatofautiana, mimi natamani niwe na roho mbaya, nisiyejali wala kuthamini wengine ila nimeshindwa.

Naomba kama kuna mahala unaweza kubadilisha nafsi ya hofu ya mungu na kuwa na roho mbaya nipeleke au nipe notes nipitie niweze kubadilisha nafsi hii.
 
Anazungumzia nini kwa aliyeelewa.
 
Nakupa mbinu mbili mkuu!!

1.Andika majina ya mkuu was kazi Yako,na member wote kwenye karatasi nyeupe ya rim ile!ambatanisha na neno kama mathayo 7:7 halafu andika maombi yako unataka waweje kwako ,Ile karatasi ikunje weka kwenye maji yenye chumvi ya mawe iliyoyeyuka kwenye hayo mahi!maji hayo unaweza yaweka kwenye chupa ya soda ya plastic ikiwa na hiyo karatasi ,fungal chupa iweke ndani kwako hasta kwenye kabati au sehem ambayo mtu yeyote hawezi ifikia!

2.kwenye mshahara wako toa fungu la kumi kwenye madhabahu ya kiroho unayoiamin halafu unapomuomba mungu Anza Kwa maneno haya"Kwa mamlaka ya zaka niliyotoa kwenye madhabahu Yako ewe mungu naomba ...... Unasema unachokitaka kuanzia afya hadi michongo ya pesa!!

Hiyo nimejaribu nimeona matokeo!na wewe jaribu!!
 
Kanda ya ziwa ndiko neno POTI lilikozaliwa. Poti maana yake ni WA Nyumbani au wamuhira kwa ndugu zangu kigoma. Ukiona mtu yeyote anayependa kutumia majina hayo ni M nepotism
 
Naomba unipatie kozi fupi ya kuwa na roho mbaya na ya ukatili, nisiyejali wala kujua ya wengine kwa ufupi nifunze kuwa kama wao kwa kuwa naamini mimi sijajiumba ila naitaji kubadilika niwe zaidi yao.
Kuzaliwa mwanaume tu ni kibali tosha cha wewe kuwa na maamzi magumu pale panapo hitajika kufanya hivyo;
Haiwezekeni unyanyaswe kwa miaka zaidi ya10 hadi unapata magonjwa ya moyo na bado hujafanya maamzi.Kuna shida mahali
 
Mkuu pole sana... cha kukushauri hebu hebu kuwa mtu wa ibada sana... pia kama changamoto.. zipo kila sehemu... cha msingi kujitaambua tu. Kwa sababu umeshawajua... wewe piga kazi tu usiwafuatilie wala usotegemee michongo ya kazini.. pokea mshahara wako wa halal.. panga mipango yako binafsi ya maendeleo kimya kimya... Acha shobo nae labda ucheke nao kinafiki.. maaana umeshajua upo na nyoka....

N.B wahi kazini mapema na ukifika
, fanya kazi.. muda wa kurudi ukifika.. fungal mafaili yako na urudi nyumbani uendelee na majukumu binafsi pia ufurahi na familia.....

Ukifanya hivyo walau utaona raha ya maisha
 
📌📌📌COMMENT BORA KABISA KWA MWANZO WA MWEZI.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…