Mkuu japo serikali kuu huwezi kuacha kuilaumu katika hili...Lakini nilichojifunza kwa miaka kadhaa ya kuwepo serikalini ni kwamba ma-CEO, Wakurungenzi na maafisa utumishi wengi kwenye hizi taasisi za umma wanageuka kuwa miungu watu na kuwanyanyasa sana wafanyakazi hali inayopelekea lawama zote ziwe kwa serikali kuu.
Furaha ya mtumishi wa umma inatokana na viongozi wa taasisi husika aliyopo, na hizi lawama hazojaanza leo.Mfano
Taasisi niliyoajiriwa Boss na viongozi wa ngazi za juu wako peace sana, kiasi kwamba wakigundua mtumishi una tatizo ambalo linapelekea kutokuwa sawa kiakili lazma wakuite na wanahakikisha wanalisolve...ukipatwa tatzo linahusiana na uchumi watatafuta namna yoyote hata kukutengenezea safari ya kikazi au masaa ya kikazi ya ziada ili ulipwe pesa utatue tatizo lako.....hali hii imetufanya wafanyakazi hata weekend tunaenda kufanya kazi kumaliza viporo hata Kama itafikia usiku na bila malipo na hatuna manung'uniko kabisa.
Kuna baadhi ya wafanyakazi kwenye taasisi za umma wana maisha mazuri hata hilo ongezeko la mshahara la Magufuli hawana shida nalo.., wao mishahara na posho ziko vizuri na bado wana viongozi wanaojali na madaraja wanapanda kwa haki na kwa wakati.
Hebu angalia, Ofisini ukiwa hauko sawa kiakili kufanya kazi mkoa X na ukasema ukipelekwa mkoa Y utakuwa sawa basi utahamishwa kama uhamisho wa kawaida na utalipwa lakini taasisi zingine utaambiwa uandike barua ya kuomba kujihamisha mwenyewe ambapo hutalipwa haya mambo yako halmashauri na taasisi zingine
Taasisi Kama BOT, TMDA, TASAC, TCRA,TPDC,EWURA, WCF,NHIF, TBS ni baadhi ya taasisi zinazolipa vizuri na zinajali watumishi wake huwezi kukuta mtumishi kule analalamika.
Pamoja na hayo serikali imezingua sana kwenye fao la kujitoa na pensheni