TheCrocodile
JF-Expert Member
- May 31, 2021
- 1,199
- 3,307
Mahakama ya Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara imemhukumu Shamsudini John maarufu SIKUKUU mwenye miaka 35 kunyongwa hadi kufa kwa kosa la kuwauwa kwa kukusudia kwa kuwanyonga kwa kanga mkewe Asia John aliyekuwa na umri wa miaka 25 na mtoto wake Ahmed Shamsudini aliyekuwa na miaka Tisa (9) baada ya mke wake kumkatalia kuongeza mke wa pili.
Hukumu hiyi namba 13 ya mwaka 2020 imetolewa leo Disemba 07 kwenye Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Manyara na Jaji Devota Kamzola ambapo ameieleza mahakama kwamba mshtakiwa alitekeleza mauaji yao kwa kukusudia.
Awali Jaji Devota aliieleza mahakama kwamba mshatakiwa huyu Shamsudini John alikuwa na ugomvi na mkewe Asia John baada ya kutaka kuoa mke wa pili ndipo marehemu mkewe alikataa jambo hilo na kupelekea mumewe kufanya mauaji hayo katika Kijiji cha Hidet wilayani Hanang mkoani Manyara.
Jaji Devota aliendelea kwa kusema, mshtakiwa Shamsudini alitekeleza mauaji hayo kando ya Bwawa la Hidet wilayani Hanang umbali wa zaidi ya kilo mita moja kutoka kwenye nyumba waliyokuwa wakiishi na kwamba mshtakiwa alianza kumnyonga mkewe Asia kwa kutumia kanga, huku mtoto wao Ahmed Shamsudini akipiga kelele baada ya kuona mama yake ananyongwa na kisha kunyonga na mtoto wao na kumtupa kwenye bwawa hilo, kabla ya kumtoa na kisha kuondoka na mwili wa mkewe hadi nyumba.
Imeelezwa kuwa mshtakiwa alipofika nyumbani alianza kuchimba shimo kwa minajili ya kuuzika mwili wa marehemu Asia, kabla ya mke mdogo kumuona na kumuhoji mshtakiwa ambaye alijibu anachimba shimo la taka na kuuzika jirani na nyumba waliyoishi.
Imeelezwa mahakamani hapo kwamba mshatakiwa alikana kuhusika na vifo hivyo na kueleza kwamba mke wake na mtoto walikufa maji, huku shahidi namba tatu ambaye ni daktari alithibitisha vifo hivyo vilisababishwa na kukosa hewa na siyo kufa kwa maji kama alivyojitetea mshtakiwa lakini baadaye Shamsudini alikiri kutenda matukio hayo na kuwapeleka polisi mahali alipouzika mwili wa mke wake na ulipo mwili wa mtoto kando ya bwawa.
Mshtakiwa amekutwa na hatia kinyume na vifungu vya Kanuni ya 196 na 197 vya kanuni ya adhabu Sura namba 16 Toleo mwaka 2002.
My take: Jamaa anastahili adhabu zaidi ya kunyongwa kwa kitendo hiki cha kikatili kabisa, ingefaa afungwe jiwe zito shingoni kisha atupwe mto Kagera akawe chakula cha mamba.