Manyara: Ahukumiwa kifo baada ya kunyonga mkewe na mtoto baada ya mkewe kumkatalia kuongeza mke wa pili

Manyara: Ahukumiwa kifo baada ya kunyonga mkewe na mtoto baada ya mkewe kumkatalia kuongeza mke wa pili

Ni kweli uko sahihi.
Lakini pia, mke hakua sahihi kumkatalia kuongeza mke, japokua kama ulivyosema hatua aliyochukua jamaa ni sio sahihi pia hata kidogo. Angempa talaka tuu.
Mke nae alikuwa sahihi, Uislamu haulazimishi mke kukaa kwenye ndoa atayokosa furaha Kwa ajili ya wivu....Mwenyezimungu anasema amejaalia kwenye ndoa kuwe na mapenzi na huruma baina ya wanandoa, Kama mke ameona hawezi kumpenda tena mume Kwa kuongeza mke, wangekaa wakajadiliana, ingewezekana wangeachana tu Kwa usalama kila mtu maisha yaendelee.
 
Amekipata alichokua anakitafuta.
 
Ukatili mkubwa.

Unamuua mama huku mtoto anatazama, haitoshi unamuua na mtoto.

Wanawake tunanyanyaswa
 
Hiyo Dini ndo inaruhusu umnyonge, Dini inasema ishi nae Kwa wema, ikitokea kuachana muache Kwa wema....Kama alipata inayofinyia Kwa ndani huko nje angempa talaka zake tu, sio kumtanguliza kaburini.
Hakufata mafundisho ya Dini.
Hao wakristo wote
 
Sasa anaenda kuolewa yeye na manyapara
Ataolewaje wakati "condemn" wanatengwa sehemu maalumu halafu kila mtu na selo yake, mawazo tele moyoni!

Muda wa kuchanganyika na wafungwa wa kawaida haupo.
 
Itakuwa jamaa alikuwa ana magonjwa ya akili sio kawaida

Bora uoe au uolewe na malaya, atacheat ila jion atarudi, watoto watakula, watasoma, watalala.

Ila ukiolewa na mgonjwa wa akili yani mentally unstable atafanya jambo la hatari mda wowote ndio hao wakupiga risasi wake zao

Na ukioa mgonjwa wa akili anaweza wafanya watoto wako kama mawe, unakuta mwanamke anampiga mwanae kama anampiga mnyama au mti kumbe kamzaa mwenyew

Kwenye uchumba tu ukiona tu dalili zozote za uchizi chizi, hasira za kijinga, sheria za kipumbavu, mipaka isiyo namantiki, bora umwepuke mapema.

Sheria ifuate mkondo wake.
Huyo ni mzima kabisa. Kawapeleka bwawani ili asingizie walikufa maji. Huyu alijua na alipana alichofanya. Sema huku hatanyongwa. Nchi za wenzetu mfungwa wa kosa kama hilo akiingia tu jela wafungwa wenzake wanaye. Hata wiki hamalizi.
 
Ataolewaje wakati "condemn" wanatengwa sehemu maalumu halafu kila mtu na selo yake, mawazo tele moyoni!

Muda wa kuchanganyika na wafungwa wa kawaida haupo.
Hapana Condemn hawakai kila mtu chumba chake wanakaa pamoja selo kama wapo 50-70 wanakaa pamoja.
 
Huyo ni mzima kabisa. Kawapeleka bwawani ili asingizie walikufa maji. Huyu alijua na alipana alichofanya. Sema huku hatanyongwa. Nchi za wenzetu mfungwa wa kosa kama hilo akiingia tu jela wafungwa wenzake wanaye. Hata wiki hamalizi.
"Wanaye" kwa maana ya kumuwowa, si ndio?
 
Magonjwa ya akili...mapepo..kukosa elimu ni shida Sana..
 
Back
Top Bottom