Analogia Malenga
JF-Expert Member
- Feb 24, 2012
- 5,108
- 10,191
Mkazi wa Kijii cha Ng’wandakw, Kata ya Haydom Wilayani Mbulu Mkoani Manyara, Philemon Tandu (50) amefariki dunia kwa kujinyonga baada ya kuachwa na mke wake akiwa na watoto watano.
Kamanda wa polisi wa mkoa wa Manyara, kamishna msaidizi (ACP) Marrison Mwakyoma akizungumza jana alisema tukio hilo lilitokea juzi kwenye kijiji hicho cha Ng’wandakw.
Kamanda Mwakyoma amesema marehemu huyo, Tandu (50) alijinyonga kwa kutumia kamba ya katani shingoni baada ya mkewe Christina Elia (45) kumuacha akiwa na watoto watano.
Amesema chanzo cha kifo hicho ni matatizo ya familia ambapo mara baada ya Tandu kuachwa na mkewe alichukua uamuzi wa kujinyonga kwa kutumia kamba ya katani.
Amesema baada ya mwanamke huyo kutaka kumwacha mumewe walijaribu kusuluhisha ugomvi wao ili wasiachane na walee watoto wao ila ikashindikana mwanamke huyo akaondoka.
“Tandu alijinyonga kwa kutumia kamba ya katani karibu na nyumba yake mara ya mkewe kuondoka nyumbani kwao akidai hamtaki tena na kumwachia watoto watano,” amesema Kamanda Mwakyoma.
Amesema baada ya majirani kuona mwili wa marehemu huyo umening’inia chini ya mti walitoa taarifa kwa askari wa kituo cha polisi Haydom ambao walifika eneo hilo akiwa amefariki.
Ametoa wito kwa jamii ya eneo hilo kutoshiriki matukio kama hayo kwani endapo kuna tatizo wanapaswa kukaa kama familia na kutatua kuliko kujidhuru nafsi yake mwenyewe.
Baadhi ya wanakijiji waliozungumza na Mwananchi wameeleza kusikitishwa na tukio hilo wakisema kutakuwa na mzigo wa kuwalea watoto hao watano.
“Watu wanakwenda hadi India kwa ajili ya kutafuta uhai kwenye hospitali za huko kisha mtu anaamua kujinyonga na kuondoa uhai wake kisa mke amemuachwa,” amesema John Thomas.
Mwananchi