Chachu Ombara
JF-Expert Member
- Dec 11, 2012
- 6,067
- 10,938
Basi kampuni ya Mohammed Classic ya kutoka Arusha-Kigoma imepata ajali Eneo la Gehandu Hanang mkoani Manyara.
==============================
Akizungumzia tukio hilo, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Manyara, Benjamin Kuzaga amesema: "Ajali hiyo imetokea imetokea Kijiji cha Ming’enji Wilaya ya Hanang katika Barabara ya Babati, ajali imehusisha gari aina ya Fuso lenye namba za usajili T380 DWF lililokuwa likitoka Tabora kwenda Moshi limegongana uso kwa uso na Basi la Mohammed Classic.
“Basi hilo lilikuwa likifanya safari zake kutoka Arusha kwenda Kigoma, katika ajali hiyo waliopoteza maisha ni dereva wa Fuso jina Amir Haruna pamoja na msaidizi wake ambaye jina halijajulikana.
“Wengine waliofariki ni ni msaidizi wa dereva wa basi aliyefahamika kwa jina moja la Omari na utingo wake.
“Chanzo cha ajali ni dereva wa basi kutozingatia alama za barabarani, kwani eneo la tukio kuna ujenzi wa barabara unaendelea, kuna alama ambazo hakuzizingatia, badala yake akajikuta alivaa gari hilo aina ya Fuso.
“Kuna majeruhi 26, kati yao wanaume ni 14, wanawake 10 na watoto wawili, wote wamefikisha hospitali kwa ajili ya matibabu, lakini wanaendelea vizuri.
“Natoa wito kwa madereva wote wa vyombo vya moto kuzingatia alama za barabarani kwani zina maana yake, kufanya uzembe kama huyo unakuwa unasababisha madhara makubwa.”
PICHA: Hawa na BobDere Omari Marangi