Manyara: Mama aua watoto 3 kwa kuwalisha sumu kutokana na ugomvi wa kifamilia na mume wake

Manyara: Mama aua watoto 3 kwa kuwalisha sumu kutokana na ugomvi wa kifamilia na mume wake

Miss Zomboko

JF-Expert Member
Joined
May 18, 2014
Posts
4,599
Reaction score
9,532
Mama mmoja aliyetambuliwa kwa jina la Regina Daniel (24) mkazi wa Louxmanda Kijiji cha Bashnet Wilaya ya Babati mkoa wa Manyara, anatuhumiwa kuwauwa watoto wake watatu kwa kuwalisha maembe yenye sumu inayodaiwa ni ya Panya .

Tukio hilo la kusikitisha limetokea Desemba 5 mwaka huu ambapo mtuhumiwa aliyapaka sumu maembe mawili kisha kuwapatia watoto hao.

Leo Jumatatu Desemba 7,2020 Kamanda wa Polisi mkoa wa Manyara ACP Paul Kasabago amethibitisha kutokea kwa tukio ambapo amesema chanzo cha Mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia kati ya mama huyo na mume wake ambao umesababisha mke kuchoshwa na maisha hayo na kuamua kufanya tukio hilo kwa lengo la kumuokoa mume wake.

Kamanda amewataja watoto waliopoteza maisha ni Emmauel Agustino (7), Emiliana Agustino (4) na Elisha Agustino ambaye umri wake ni mwaka mmoja (1).

Kasabago ameeleza kuwa wamefanikiwa kumkamata mtuhumiwa kwa ajili ya kumfanyia mahojiano.
 
So sad, Haya matukio ya kifamilia yamekuwa mengi sana siku hizi
 
Dunia ya sasa ingekuwa daladala inatoka Dar kwenda mwanza amini kabisa kuna abiria wangeshuka njiani na kutembea kwa miguu kukwepa kuchoshwa na foleni kama hizi.

Eeh mwenyezi Mungu wasamehe wazazi wangu kama walivyonilea mimi tangu nikiwa mdogo.

Wazazi wa siku hizi baadhi yao wana ushetani fulani ndani ya mioyo yao na hawahofii kutoa kafara kwa namna yoyote ile, iwe kwa kubaka watoto wao au kuwaua.
 
Mauaji hayo ni ugomvi wa kifamilia kati ya mama huyo na mume wake ambao umesababisha mke kuchoshwa na maisha hayo na kuamua kufanya tukio hilo kwa lengo la kumuokoa mume wake.
Aliyeelewa hii statement tafadhali.

Sijui mvinyo umenielemea kichwani,sina uhakika...
 
Mpumbavu sana uchungu wote alioupata kuwapata hao watoto, bora angejiua yeye mwenyewe
 
Mpumbavu sana uchungu wote alioupata kuwapata hao watoto, bora angejiua yeye mwenyewe
Yaan akili yake haitokaa irudi mahali pake akikumbuka alivowabeba na kuwalea, wakawa wanampigiza kelele ndani miaka yote iyo afu leo kabaki ivi ivi dah
 
Hii habari imenisikitisha sana, hibi kweli ugonvi wako na mume unaua watoto, the innocent kids ambao umewabeba kwa tabu na kuwazaa kwa uchungu

Huu ni ukatili usioelezeka[emoji24][emoji24][emoji24]
 
Akili za kitoto. Ndo madhara ya ndoa za utotoni,kazaa akiwa na miaka 17 stress na mengineyo yamechangia. R.I.P malaika watoto

Kapumzike jela mama mtu
 
Back
Top Bottom