LGE2024 Manyara: RC Sendiga apeleka nyama ya nyumbu kwa jamii ya Wahadzabe ili kushawishi kujiandikisha katika daftari la makazi

LGE2024 Manyara: RC Sendiga apeleka nyama ya nyumbu kwa jamii ya Wahadzabe ili kushawishi kujiandikisha katika daftari la makazi

Uchaguzi wa Serikali za Mitaa 2024

Mkalukungone mwamba

JF-Expert Member
Joined
Aug 29, 2022
Posts
862
Reaction score
1,755
Wakati yamebaki masaa kabla ya kukoma kwa zoezi la uandikishaji wapiga kura katika daftari la makazi kufikia ukomo leo Oktoba 20, Mkuu wa mkoa wa Manyara Queen Sendiga tarehe 19.10.2024 alitembelea jamii ya Wahadzabe katika kijiji cha MONGO-WA-MONO wilayani Mbulu ambao maisha yao bado yanategemea uwindaji na kuokota matunda na asali ambapo amewahimiza kujiandikisha katika daftari la makazi ili waweze kuchagua viongozi wao katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa unaotarajiwa kufanyika Novemba 27 mwaka huu.

Soma Pia: Katibu Tawala Mkoa wa Simiyu aamua kutembelea ofisi mbalimbali kuhamasisha Watu wakajiandikishe katika Daftari la Kupiga Kura

Sendiga alifika katika kijiji hicho kilichopo kata ya Yaenda Chini wilayani Mbulu akiwa na zawadi ya kitoweo cha nyama ya nyumbu ili kushawishi jamii hiyo kuwa na utulivu wa muda kujiandikisha katika daftari la makazi kabla ya zoezi hilo kufikia ukomo Oktoba 20 ili waweze kushiriki katika katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.

Pia amewata kushiriki kuwachagua viongozi wa jamii yao wenye uwezo wa kuwaongoza kuharakisha juhudi za maendeleo katika eneo lao wakati wa uchaguzi huo.

Wakizungumza kwa niaba ya wenzao baada ya kupokea zawadi hiyo na ujumbe wa kujiandikisha, Salum Joseph Duduqwe na Zuberi Mathayo wamemshukuru Mkuu wa Mkoa kwa kuwathamini kwa kuwatembelea, ambapo wamemweleza kuwa asilimia kubwa tayari wameshajiandikisha na wameahidi kuendelea kuwashawishi wengine ambao bado wakajiandikishe kabla ya zoezi hilo kufikia ukomo.

Screenshot 2024-10-20 124421.png
Snapinsta.app_463622428_484454291411327_109252966898749989_n_1080.jpg
Snapinsta.app_464079829_1482800112435467_5381245100256837309_n_1080.jpg
 
Mtu mpumbavu ni yule anayefanya vitu vile vile kila siku huku akitegemea matokeo tofauti. Hii ni sawa na uchaguzi wa Tanzania.
 
Very suspicious,eti kapinda na yeye kamgongo kama huyo mbabu ili aonekane kafanya jambo la kibunifuuu🤣🤣🤣🤣.Wanasiasa🙌🙌🙌🙌🙌
 
Sendiga alifika katika kijiji hicho kilichopo kata ya Yaenda Chini wilayani Mbulu akiwa na zawadi ya kitoweo cha nyama ya nyumbu ili kushawishi jamii hiyo kuwa na utulivu wa muda kujiandikisha katika daftari la makazi kabla ya zoezi hilo kufikia ukomo Oktoba 20 ili waweze kushiriki katika katika uchaguzi wa Serikali za Mitaa.
Hapa ndipo mnapowachanganya watu
Zawadi kwa kazi gani waliyofanya? Je hiyo zzawadi itaendelea kutolewa nyakati zote zijazo?
 
Back
Top Bottom