Manzoki aiaga rasmi klabu ya Vippers, anaelekea Nchini China kujiunga na klabu ya Dallian FC. Juhidi za simba kuinasa saini yake zagonga ukuta

Manzoki aiaga rasmi klabu ya Vippers, anaelekea Nchini China kujiunga na klabu ya Dallian FC. Juhidi za simba kuinasa saini yake zagonga ukuta

sky soldier

JF-Expert Member
Joined
Mar 30, 2020
Posts
5,407
Reaction score
19,264
Muhimu: Mchina kamwaga milioni 930 kuinasa saini na mshahara mnono, wanaoaminishwa na tetesi kwamba Manzoki atacheza China miezi minne na kisha kurudi simba wajaitafakari upya, Ni sawa na rubani wa ndege apate kazi shirika la ndege halafu mtegemee baada ya miezi minne aanze kuendesha mabasi ya mikoani,

Imeshakuwa kawaida sasa kwa Simba kuporwa tonge mdomoni kwenye usajili wa wachezaji wa kigeni, badala ya kuweka kitita wao wanatumia muda mwingi kuomba kupunguziwa bei, kusubiri wachezaji mikataba yao iishe ile wawanunue kwa bei rahisi, n.k. matokeo yake ndio haya sasa, Mchina kasikia kuna mchezaji anatajwa tajwa sana kaweka kitita, case closed!,simba wanabaki kuangaliana tu.


Mo Dewji kabla hajapewa umiliki wa simba milele alikuwa ananunua wachezaji fasta bila kujali gharama zao, ila sasa baada ya kupewa timu ameridhika maana anajua tayari simba ni yake, ni kama vile unapomtongoza binti inabidi ujiongeze lakini baada ya lengo lako kutimia unakuwa huna presha ya kumfanyia vitu special kama mwanzoni,saizi kaigeuza simba kama biashara yake na anaiendesha kikanjibahi kibahili bahili sana kwa lengo la faida kubwa, Faida kwanza mambo mengine baadae

FB_IMG_1661598591869.jpg
 
Sisi makolo mbumbumbu si walisema mkataba miezi minne jamani mbona hivi tena
 
Mkataba na hiyo timu yake anayoenda China ni wa miezi minne, December unaisha, sioni shida iko wapi hapo, wacha akale pesa za hiyo miezi minne, then after anatua Msimbazi.

Mpunguze makasiriko.
 
Cesar Manzoki anahusishwa kwenda China kunako klabu ya Dalian kwa ada ya Tsh 970m kwa mkataba wa miaka minne kwa mujibu wa @kawowosports
 
Bongo bwana sasa unataka simba ishindane na team za China wakati league kuu ya uingereza wameshindwa kaondoka oscar Chelsea chini ya abromovic kwani manzoki hawapendi hela.
 
Hio timu ishakua alinunua babu hadi wajukuu wanatumia........ndo mmiliki huyo hadi vitukuu
 
Uzi wa Manzoki lakini anaeshambuliwa ni Mo
Ukiangalia hizi comments za mashabiki wa yanga inasadiki ile kauli ya manara wenye akili ni wawili kwasababu duniani hakuna team inayoweza kushindana na hao wachina kwenye mishahara na dau la uhamisho sasa simba ina hela gani ya kushindana na china naona watu wanamshambulia mo sijui walitaka afanyeje.
 
Back
Top Bottom