Maofisini kuna aina ya watu uwepo wao ni kero kwa wengine

Moto wa volcano

JF-Expert Member
Joined
Jun 3, 2018
Posts
2,682
Reaction score
6,638
Jitahidi sana maisha yako yawe baraka kwa wengine hata ukitoka sehemu watu waone wamepungukiwa , kuna aina ya watu huwa wakitoka sehemu watu waliobakia wanasema afadhali hayupo , hii ipo sana maofisini kuna aina ya watu uwepo wao tu ni kero kwa wengine hadi wafanyakazi wenzake wanaomba dua usiku na mchana huyo mtu ahamishwe ili wapumue. Jitahidi sana kuwa barua iliyo njema ,
 
1.Chawa.
2. Wajivuni.
3. Wafitini/ wakoloni.
 
Hii imekaa kwa MaHR wengi, ulevi wa madaraka huwa unawasumbua
 
Kaa mbali, narudia tena, Kaa mbali na mfanyakazi mwenzako unaemjua au unaemhisi atakuharibia kazi yako.
 
Hata wahasibu wanaobania malipo ya wengine wanwazungusha
Mhasibu usipokuwa na manufaa naye atakuzungusha sana; mimi namshirikishaga madili madili mpaka naambiwa she's my work wife kumbe wala, yaani hata aende mwingine na deal natafutwa mimi kwanza kujua kama huyo ni snitch 🤣
 
Ni kila walipo watu zaidi ya mmoja
 
Hayo matatizo yapo kila mahali,cha muhimu fanya kilichokuleta hapo,ukimaliza nenda nyumbani kwako.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…