Maombi maalum kwa ajili ya Sativa na Watanzania wote waliofia au kuteswa mikononi mwa polisi

Maombi maalum kwa ajili ya Sativa na Watanzania wote waliofia au kuteswa mikononi mwa polisi

Mbona tuliambiwa kwamba haya mambo ya kutekana tekana na kutesana tesana yaliyaisha kwenye ile awamu mliyoiita ya kishamba, sasa na leo hii yametoka wapi tena na wakati tunaambiwa nchi ina amani raia unatembea muda wowote unaotaka na vyombo vya dola viko macho na havitumiki tena kisiasa au kwenye matukio yoyote ya kigaidi???
 
Bangi ndio imemfanya atekwe na kuteswa? Wote waliotekwa ni wavuta bangi? Sheria gani ya nchi inaruhusu wavuta bangi watekwe na kuteswa?

Ukiona mtu anatekwa na kuteswa na watuhumiwa hawakamatwi,basi hata wewe mnywa juice ya maembe upo hatarini.
Mwambie huyo dogo aache mibange inayomtuma kufanya ujinga mitandaoni alafu hana hata ulinzi wala kinga ya kimwili na kiroho anadakwa kirahisi rahisi tu na kwenda kutupwa msituni alijua mibange inafukuza MAJINI ndio walivyomuongopea?
 
Nina swali dogo hapa wanajf huyu Sativa ni mwanaharakati kiasi kwamba jambo lililomtokea linahusishwa na polisi?
Kwanini polisi wanahusishwa na jambo hili?
 
Andika Sativa Google pale alafu angalia upande wa Picha usipokuta mibange nipigwe ban na Maxence Melo mwenyewe nisiingie tena JeiF
Kwani una umri gani? Naona una kichwa kigumu cha kuelewa kama chuma cha reli,
Nimekwambia neno moja linaweza kua na maana nyingi tu,umekazania mibange!! Wake up na ipe akili yako freedom ya kuwaza zaidi ya hapo.
 
Nina swali dogo hapa wanajf huyu Sativa ni mwanaharakati kiasi kwamba jambo lililomtokea linahusishwa na polisi?
Kwanini polisi wanahusishwa na jambo hili?
Mvuta mibange TU wa huko X Hana impact yoyote kwa Taifa
 
Kwani una umri gani? Naona una kichwa kigumu cha kuelewa kama chuma cha reli,
Nimekwambia neno moja linaweza kua na maana nyingi tu,umekazania mibange!! Wake up na ipe akili yako freedom ya kuwaza zaidi ya hapo.
Ndio niambie maana nyingine ya Bange Mzee umeshazeeka au nipe maana nyingine ya Bange aina ya Sativa maana yake ni IPI?
 
Ndio niambie maana nyingine ya Bange Mzee umeshazeeka au nipe maana nyingine ya Bange aina ya Sativa maana yake ni IPI?
Ulimsumbua sana mwalimu wako Darasani kukuelewesha,

Nani amekukaririsha kua hilo jina lazima likatafsiriwe kwenye bangi? Mbona unakua na kichwa kigumu kiasi hicho?
 
Ulimsumbua sana mwalimu wako Darasani kukuelewesha,

Nani amekukaririsha kua hilo jina lazima likatafsiriwe kwenye bangi? Mbona unakua na kichwa kigumu kiasi hicho?
Google Mwalimu mzuri ingia Google hapo andika 'Sativa' isipokuletea mibange kibao mapichapicha ya mibange mfululizo Payge anipige ban ya Mwaka Mzima
 
Huna akili wewe,bila shaka upo Milembe mida hii
Basi ingia YouTube andika 'Sativa' utaona mibange inayokuja video za mibange tupu

Ninachokwambia ni kwamba Wewe na wenzio mkishakula Bange zenu nendeni mkalale mambo ya kutukanatukana watu mitandaoni kisa eti umejiboost stick zako kadhaa huo ni ujinga
 
Hayo mambo ya mungu ni hadithi za kusadikika ! Angekuwepo kweli asingekaa kimya mpaka Leo, hajawahi kutuonyesha hata kwa dalili alipo Ben saanane! Angekuwepo na kama angekuwa anasikia maombi yetu mwanetu Paul mwangosi asingekufa kinyama namna ile na mungu akawa anaona tu ! Kama angekuwepo waliomteka na kumpoteza mwandishi wa mwananchi ndugu azory gwanda huko kibiti mungu asingewaacha bila kuwaumbu na ikabaki Siri mpaka Leo ! Nasema hivi ni habari za kusadikika kumhusu mungu !angekuwepo Watu maelfu wasingetupwa na kuokotwa kwenye mifuko ya sandarusi baharini , mungu asingenyamaza angeshuka kutuonyesha ukuu wake na angetoa hukumu Kila mtu angeona ! Nahisi labda mungu anaesimuliwa kwenye hivi vitabu alikuwa mungu wa enzi zile za akina ibrahimu na akina Musa na isaka ,ama Joshua eliya na Gideon ,huenda aliyepo sasa sio yule Jehova ! Kwa nini huyu hatoi majibu !? Kwa nini huyu anakaa kimya hata watu wake wanapoonewa ? Angalia sasa juzi watu wameenda kumwabudu yeye huko saudia maelfu wamekufa na kuacha watoto yatima na wake zao wajane ! Mungu wa akina ibrahimu asingekubali maafa ya aina hii ! Ona mji Rafah yamebaki magofu lakini mungu yupo kimya ! Tuziamini nguvu zetu huenda tukifa ndio mwisho wetu !
 
Mtaomba sana wabongo hamuwezi shuruba kama hizi

1719608620130.png

1719608757262.png
 
Back
Top Bottom