Samson Ernest
JF-Expert Member
- Aug 28, 2014
- 1,237
- 1,744
Zab 143:7 SUV
[7] Ee BWANA, unijibu hima, roho yangu imelegea; Usinifiche uso wako, Nisifanane nao washukao shimoni.
Tunafahamu kuna wagonjwa wa dharura, wagonjwa ambao huwa hawapangi foleni kama wengine, kutokana na shida waliyonayo, madaktari hutumia kila njia kuokoa maisha yao.
Mgonjwa wa dharura huwa hahudumiwi kama wagonjwa wengine, simaanishi wengine huhudumiwa vibaya, nataka uelewe jambo la msingi hapa, mgonjwa aliye mahututi anahitaji umakini na huduma ya haraka ili kumsaidia asipoteze uhai wake.
Ndivyo ilivyo na mtu wa kiroho, yapo mambo ambayo yanahitaji kusaidiwa haraka, mwamini anaweza akapatwa na shida ngumu ambayo inahitaji Mungu aingilie kati haraka sana kumsaidia juu ya kile kimempata.
Tunaona katika zaburi hii, hasa mstari huu unaonyesha wazi vile Daudi alihitaji msaada wa Mungu kwa haraka sana, inaonyesha wazi alibanwa vibaya na shida ngumu, shida ambayo ilihitaji msaada wa haraka sana.
Roho ya Daudi kulegea inaonyesha wazi ni jinsi gani mtumishi huyu udhaifu ulimvaa, kukata tamaa kulimkata kisawasawa, na huenda alipungukiwa na nguvu, na tumaini lake lilianza kufifia.
Hali alliyokuwa anapitia Daudi ilikuwa ni ya kiroho au kihisia zaidi, ambapo alifika mahali hakuwa anaona tena zile nguvu ndani yake za kusonga mbele, hapo alikuwa ameshachoka, amedhoofika, na kukata tamaa.
Sasa maombi yake yalimwendea Mungu moja kwa moja na kumwambia "usinifiche uso wako", alitaka kibali kwa Mungu, maana bila kibali maombi yake yalikuwa ni kelele mbele za Mungu na yeye alikuwa na shida ngumu inayohitaji msaada wa haraka.
Tunajifunza jambo la msingi sana hapa, tunapofika mwisho wa akili zetu, na kuona zile nguvu za rohoni zimeisha, hatupaswi kukalia kimya hiyo hali, maana tunakuwa kwenye kipindi cha hatari sana kisichokuwa na kinga yeyote.
Tunapojikuta katika hali ya kukata tamaa na hatuna tumaini tena na yale tuliyoyatarajia, hatupaswi kukaa kimya, tunahitaji kuingia kwenye maombi ya dharura ya kuhitaji msaada wa haraka.
Hatari kubwa sana kwa mwamini kukosa tumaini au imani mbele za Mungu, hatari yake ni kwamba adui anaweza kumfanya chochote anachotaka, maana imani yake inakuwa tayari imepigwa.
Maombi ya dharura yanaruhusiwa mbele za Mungu, hupaswi kuchelewa wakati huu, kuchelewa kwako kutazalisha madhara makubwa sana kwako au kwa familia yako au kwa kanisa au kwa taifa lako.
Ikiwa bado umebakisha imani ndogo kwa Mungu, nenda mbele zake haraka sana, bila kuangalia taabu yako iliyokupata ina ukubwa gani, mwambie BWANA akuokoe na shida inayokukabili, atakusaidia na utakuwa salama.
Soma neno ukue kiroho
Liwe jua iwe mvua soma biblia
Mungu akubariki sana