Maombi ya Kibatala juu ya Polepole kusikilizwa Oktoba 15

Maombi ya Kibatala juu ya Polepole kusikilizwa Oktoba 15

DuaZaMama

JF-Expert Member
Joined
Jun 2, 2025
Posts
1,882
Reaction score
4,153
Maombi yaliyowasilishwa mahakamani na Wakili Peter Kibatala Oktoba 7, 2025 akiiomba mahakama itoe amri ya Polepole kufikishwa mahakamani ama mamlaka husika ziseme yupo wapi kufuatia tukio la kutekwa kwa Balozi huyo wa zamani nchini Cuba ambaye taarifa zake zilisambaa katika mitandao ya kijamii siku ya Jumatatu Oktoba 6,2025 yatasikilizwa tena mahakamani mnamo Oktoba 15, 2025.

Maombi hayo ambayo leo yamesikilizwa kwa mara ya kwanza leo Oktoba 9, majira ya saa tatu asubuhi mbele ya Jaji Maghimbi yanatarajiwa kusikilizwa tena tarehe 15 baada ya majibu kuletwa na wahusika walioshitakiwa na Wakili Kibatala majira ya saa 3 asubuhi.

Wakili Peter Kibatala alifungua maombi hayo dhidi ya Mkuu wa Jeshi la Polisi nchini (IGP), Mkurugenzi wa Mashtaka (DPP), Mwanasheria Mkuu wa Serikali, ZCO wa Dar es Salaam na Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam.

Awali, Wakili Kibatala aliiambia Mahakama kuingilia kati mara moja akidai kuwa Polepole alitekwa nyara alfajiri ya Jumatatu, Oktoba 6, 2025, kutoka katika makazi yake yaliyoko eneo la Ununio, Wilaya ya Kinondoni, Dar es Salaam na watu wasiojulikana wanaoshukiwa kuwa ni askari wa Jeshi la Polisi la Tanzania.

Katika hati hiyo ya dharura Wakili Kibatala aliieleza Mahakama kuwa Polepole hajawahi kushtakiwa kwa kosa lolote la jinai katika Mahakama yoyote, na kwamba kwa sasa inaaminika anashikiliwa katika eneo lisilojulikana na maafisa wa Jeshi la Polisi.
 
Huo ni mtego mkubwa sana kwa Serikali ,maana ikatokea serikali ikakana kuwa haijahusika na utekaji maana yake ikitokea walalamikaji wakaja na ushahidi utakaowatambua watekaji kama maafisa wa serikali ,serikali itakuwa imeingia kwenye kashfa nzito sana .

Nikifiiisha nacho nikwamba serikali inaweza usije na majibu kwa wakati huu ,pengine inasubiria hadi Uchaguzi upite (kama utakuwepo)

Akili zakiuchunguzi ,inaweza kuwa hata Kibatara ametumika na system ili kuweza kuipiga pin family isiweze kuachia ushahidi hata kama wao hadi hapo baadae ili kupisha jopo la Uchaguzi ,maana yawezekana kama family isingeliwekwa chini ya uangalizi pengine ingeliweza kuachia ushahidi hovyo hovyo na mwisho kuiongezea ugumu serikali ambayo kwa sasa ipo kwenye mchakato wa usajiri mpya.
 
Back
Top Bottom