Home tutor Dar
Senior Member
- Feb 23, 2025
- 126
- 156
Mheshimiwa Waziri wa Kazi, Ajira na Wenye Ulemavu,
Kwa heshima na taadhima, napenda kuwasilisha malalamiko na ushauri kuhusu hali halisi ya wafanyakazi wengi hususan katika sekta binafsi hapa nchini.
Wapo Watanzania wengi wanaofanya kazi mashuleni, viwandani, hotelini, mashirika ya kimataifa na taasisi mbalimbali zinazoendeshwa na raia wa kigeni. Wafanyakazi hawa wanakumbana na changamoto zifuatazo:
1. Kutokuwepo kwa mikataba ya kazi:
Wafanyakazi wengi hufanya kazi bila mikataba rasmi, jambo linalowaweka katika mazingira hatarishi ya kunyimwa haki zao za msingi kama mshahara wa haki, likizo, na mafao ya kisheria.
2. Manyanyaso kazini (Workplace harassment):
Kuna ongezeko la matusi, kejeli, vitisho na maneno ya kudhalilisha kutoka kwa baadhi ya waajiri, hasa Raia wa nje . Wengine hutishiwa kufukuzwa kazi bila sababu za msingi.
3. Kutokuwepo kwa Bima ya Afya au kinga nyingine za kijamii:
Wafanyakazi wengi wanafanya kazi katika mazingira hatarishi (viwandani, ujenzi n.k.) bila bima ya afya au huduma za msingi za kinga dhidi ya ajali kazini.
4. Masaa ya kazi kupita kiasi:
Waajiri wengi hawazingatii sheria ya masaa ya kazi – wafanyakazi hufanya kazi zaidi ya masaa nane bila mapumziko na bila malipo ya saa za ziada (overtime).
5. Kucheleweshewa au kunyimwa mishahara:
Wengine hulipwa mishahara isiyoendana na kazi wanazofanya au hukatwa mishahara bila taarifa rasmi.
6. Ukosefu wa vyama vya wafanyakazi (Trade Unions) katika maeneo ya kazi:
Wafanyakazi wengi wanazuiwa kujiunga na vyama vyao au hata kutopewa nafasi ya kutetea haki zao kupitia miungano ya wafanyakazi.
Maombi na Ushauri:
Wako katika ujenzi wa Taifa.
Home tutor

- Serikali iweke sheria kali na adhabu kwa waajiri wote wanaokaidi haki za wafanyakazi.
- Kuwe na ukaguzi wa mara kwa mara wa mazingira ya kazi hasa kwenye shule binafsi, viwanda na taasisi zinazoendeshwa na wageni.
- Kuwe na mpango wa lazima wa mikataba ya ajira, ikiwa ni pamoja na kuhakikisha bima ya afya, NSSF, na mafao yanatekelezwa.
- Elimu ya haki za kazi itolewe kwa waajiriwa wengi ambao bado hawafahamu haki zao.
- Serikali itoe dirisha la kupokea malalamiko ya moja kwa moja kutoka kwa wafanyakazi waliodhulumiwa, bila hofu ya kufukuzwa au kubaguliwa.
Wako katika ujenzi wa Taifa.
Home tutor