KERO Maombi ya Uhamisho wa kubadilishana yamekwama muda mrefu TAMISEMI, kwanini?

Hii ni kero ambayo mwananchi ameiwasilisha JF akitaka wahusika kuchukua hatua
A

Anonymous

Guest
Nafanya kazi kama Mwalimu wa Shule ya Msingi katika Wilaya ya Buhigwe, mkoani Kigoma, kero yangu kubwa ni kuhusu kuchelewa kwa vibali vya uhamisho wa kubadilishana kwa watumishi wa kada mbalimbali nchini.

Nimekuwa nikifuatilia uhamisho wa kubadilishana sababu familia yangu ipo Singida. Nilianza kutafuta mwalimu wa kubadilishana naye kituo cha kazi tangu Mei 2026, baada ya kumpata tuliwasilisha maombi kupitia mfumo wa ESS kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa.

Maombi yangu yalipitia kwa Afisa Utumishi (HRO), Afisa Elimu Msingi (DEO) na hatimaye Mkurugenzi wa Halmashauri (DED), na taratibu zote katika ngazi hizo zilikamilika. Tangu Juni 2026, maombi yangu yanaonesha status ya “PO-RALG – TAMISEMI”, ikimaanisha yamefika katika ngazi ya TAMISEMI kwa ajili ya hatua inayofuata ya uidhinishaji.

Kinachonishangaza ni kwamba hadi sasa Septemba 2026, bado sijapata kibali cha uhamisho, kwa uelewa wangu, baada ya maombi kufika TAMISEMI, ndipo mchakato wa kutoa kibali cha uhamisho unapaswa kukamilishwa na mamlaka husika, kisha kibali hicho kutumwa kwa mwajiri kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kiutumishi na mtumishi kuhamia kituo kipya.

Maombi haya yamekaa kwa muda mrefu bila taarifa yoyote ya kinachoendelea. Hali hii inashusha morali ya watumishi na kuwaweka katika mazingira magumu kisaikolojia, hasa wale ambao wana sababu za msingi za kutaka kuwa karibu na familia zao.

Nimefuata taratibu zote nilizoelekezwa, nimepata mwalimu wa kubadilishana naye, maombi yamepitishwa na mamlaka zote zinazohusika katika halmashauri, lakini sasa yamekwama TAMISEMI. Tunachohitaji si upendeleo, bali ni mchakato huu kukamilishwa kwa wakati au angalau watumishi kupewa taarifa kuhusu sababu ya kuchelewa.

Naomba TAMISEMI itoe ufafanuzi kuhusu hali ya maombi ya uhamisho wa kubadilishana ambayo yamefika katika mfumo wao. Kama kuna changamoto inayosababisha kuchelewa kwa vibali, watumishi wajulishwe ili wajue hatua wanazopaswa kuchukua badala ya kuendelea kusubiri bila taarifa.

Tunapocheleweshwa kwa muda mrefu bila maelezo, tunapoteza morali ya kazi na kuendelea kuwa mbali na familia zetu wakati tayari tumetafuta suluhisho kwa kufuata taratibu zote rasmi.
 
Pole sana mkuu, Kwa kweli inaumiza sana.. Maombi yanafanyika kwa mfumo ila kujibu tu inachukuwa mwaka nzima. Hapa sioni umuhimu wa uhamisho kuwa digitally.

Kwama wao wanaona kazi kuchakata/kujibu kwanini wasiset mfumo ukawa unachakata wenyewe (Auto) na watu wakapata majibu yao..? Vyuo vikuu mbona wameweza hili kwenye Admission processes
 
Pole,ila kama umepata w alibadilishana nae na tayari ombi liko Tamisemi inamaanisha umefuata taratibu zote za msingi.Sasa kuna muda jiongeze,tembelea Dodoma Tamisemi utashukuru baadae.Vinginevyo hata miezi 8 litakaa ndio litoke
 
Jamani na namimi ninaomba ushauri
Mimi ni mwalimu nilituma vaccancy request katika regional secretaret ya mkoa x .
Halmashauri ya walinipitishia ikaenda ninakoomba kuhamia ikakaa siku 10 mfumo ukawa ume accept wenyewe na kuniruhusu nianzishe normal transfer.Nikaanzisha na sasa inasoma PO-PSMGG(Utumishi)
Ombi langu kwenu
1.Je ikitokea nipata uhamisho naenda kwenye regional secretairet ?
2.Au nitapangiwa shule kama kawaida?
 
Nafanya kazi kama Mwalimu wa Shule ya Msingi katika Wilaya ya Buhigwe, mkoani Kigoma, kero yangu kubwa ni kuhusu kuchelewa kwa vibali vya uhamisho wa kubadilishana kwa watumishi wa kada mbalimbali nchini.

Nimekuwa nikifuatilia uhamisho wa kubadilishana sababu familia yangu ipo Singida. Nilianza kutafuta mwalimu wa kubadilishana naye kituo cha kazi tangu Mei 2026, baada ya kumpata tuliwasilisha maombi kupitia mfumo wa ESS kwa kufuata taratibu zote zinazotakiwa.

Maombi yangu yalipitia kwa Afisa Utumishi (HRO), Afisa Elimu Msingi (DEO) na hatimaye Mkurugenzi wa Halmashauri (DED), na taratibu zote katika ngazi hizo zilikamilika. Tangu Juni 2026, maombi yangu yanaonesha status ya “PO-RALG – TAMISEMI”, ikimaanisha yamefika katika ngazi ya TAMISEMI kwa ajili ya hatua inayofuata ya uidhinishaji.

Kinachonishangaza ni kwamba hadi sasa Septemba 2026, bado sijapata kibali cha uhamisho, kwa uelewa wangu, baada ya maombi kufika TAMISEMI, ndipo mchakato wa kutoa kibali cha uhamisho unapaswa kukamilishwa na mamlaka husika, kisha kibali hicho kutumwa kwa mwajiri kwa ajili ya kukamilisha taratibu za kiutumishi na mtumishi kuhamia kituo kipya.

Maombi haya yamekaa kwa muda mrefu bila taarifa yoyote ya kinachoendelea. Hali hii inashusha morali ya watumishi na kuwaweka katika mazingira magumu kisaikolojia, hasa wale ambao wana sababu za msingi za kutaka kuwa karibu na familia zao.

Nimefuata taratibu zote nilizoelekezwa, nimepata mwalimu wa kubadilishana naye, maombi yamepitishwa na mamlaka zote zinazohusika katika halmashauri, lakini sasa yamekwama TAMISEMI. Tunachohitaji si upendeleo, bali ni mchakato huu kukamilishwa kwa wakati au angalau watumishi kupewa taarifa kuhusu sababu ya kuchelewa.

Naomba TAMISEMI itoe ufafanuzi kuhusu hali ya maombi ya uhamisho wa kubadilishana ambayo yamefika katika mfumo wao. Kama kuna changamoto inayosababisha kuchelewa kwa vibali, watumishi wajulishwe ili wajue hatua wanazopaswa kuchukua badala ya kuendelea kusubiri bila taarifa.

Tunapocheleweshwa kwa muda mrefu bila maelezo, tunapoteza morali ya kazi na kuendelea kuwa mbali na familia zetu wakati tayari tumetafuta suluhisho kwa kufuata taratibu zote rasmi.
Kuna vibali vimetoka mwezi huu wa kumi umefanikiwa ?
 
Huu muda wa kuandika hunu, ungetumia kwendz kuonana na wahusika moja kwa moja.
 
Back
Top Bottom