Maombi ya ushauri wa kitaalamu kuhusu wazo la biashara

Maombi ya ushauri wa kitaalamu kuhusu wazo la biashara

Bob Manson

JF-Expert Member
Joined
May 16, 2021
Posts
4,564
Reaction score
8,810
Habari zenu waungwana, nawasilisha wazo langu la kibiashara ili nipate mawazo Kwa wazoefu na hata wasio wazoefu wa biashara hizo, lengo ni kujifunza na kupata mawazo ya wengine.

Nina wazo la kuanzisha biashara zifuatazo:

Picsart_26-01-11_18-46-08-824.jpg

1. Ninunue pool table jipya na niweke sehemu ambayo tayari nimeichangua, sehemu ambayo shughuli za vijana zipo na vijana wapo Kwa wingi, hasa vijana ambao vipato vyao ni vyakutegemea kipato Cha Kila siku.

2. Nichukue machine za betting ambazo watu wasio na access ya smartphone wanaweza kutoa mikeka na Mimi kunufaika Kwa kupata commission kutoka kampuni husika ya betting.

3. Ninunue machine Kwa mchina, zile ambazo hutumiwa Kwa kuweka miambili maarufu kama dubwi, kwakuwa nitanunua na zitakuwa zangu binafsi, hivyo baada ya muda nazifungua mwenyewe na kuchukua faida yangu.

4. Kwakuwa biashara hizo zote zitakuwa sehemu Moja, nitachukua frem au kuweka banda ambalo nitauza pombe kali na fegi pamoja na tokeni kwaajili ya machine na pool table.

Nawasilisha wazo hili kwenu mnipe mawazo na uzoefu Kwa wale ambao waliwahi kufanya au wanaufahamu kuhusu shuhuli hizo.

Rejea: Fursa ya ujinga na matrix katika mfumo wa maisha ya kisasa
 
Pool table liko vyema zaidi, kama kuna sehemu wana kijiwe cha fegi na tungi na pame changamka basi parukie.

Kuna la 200/500 ina tegemea na aina yako ya wateja, kila mzunguko mmoja ni token1 ya kucheza.

ukipata master pool mjanja basi utazidaka, maana ata hamasisha wacheze game za aina nyingi.

I mean no malice to nobody.
 
Sijuagi kwamba hizo mashine za kichina zinauzwaga, mi nnachojua wanazimiliki wenyewe wewe wanakupa tu kamishen yako
Wapo wanauza ambazo ni used, maeneo ya kimara yupo mchina anauza hizo machine.
 
Pool table liko vyema zaidi, kama kuna sehemu wana kijiwe cha fegi na tungi na pame changamka basi parukie.

Kuna la 200/500 ina tegemea na aina yako ya wateja, kila mzunguko mmoja ni token1 ya kucheza.

ukipata master pool mjanja basi utazidaka, maana ata hamasisha wacheze game za aina nyingi.

I mean no malice to nobody.
Kweli kabisa kaka, Mimi ni mchezaji wa pool table hivyo kilasiku naona namna watu wanavyoweka pesa nyingi kwenye pool.

Na sehemu ambayo nimeichangua hakuna pool kabisa, hivyo Nina Imani wateja watakuwa wengi.
 
Watarajie serikali za mitaa na mapolisi kuwa wageni wako sometimes, sikutishi ila waweke kwenye mkakati.

Wekeza kwenye hobby yako huwa anasema Liverpool VPN
 
Kweli kabisa kaka, Mimi ni mchezaji wa pool table hivyo kilasiku naona namna watu wanavyoweka pesa nyingi kwenye pool.

Na sehemu ambayo nimeichangua hakuna pool kabisa, hivyo Nina Imani wateja watakuwa wengi.
kama una mishe nyingine, basi na support uanzishe hapo ili u gain wateja na kuusoma mchezo kwa kadri inavyo kua.

Pafanyie utafiti, piga story na masela wa mtaa ujue usalama, vurugu, na usome mazingira ya biashara yako.
 
Utafiti nimefanya Kwa zaidi ya miaka Sasa, pia nitaiweka sehemu ambayo Mimi binafsi ni mzaliwa/mwenyeji wa sehemu hiyo.
 
Back
Top Bottom