Maombi ya usiku

Maombi ya usiku

Magical power

JF-Expert Member
Joined
Sep 27, 2022
Posts
2,158
Reaction score
5,626
Tunasema, asante tena kwa majira haya ya usiku. Bwana uliyagawa majira na nyakati kwa ilivyokupendeza nasi tuyafurahia majira haya katika utukufu usioringanishwa na chochote.

Asante kwa wakati wa kutwa zima ya leo. Bwana tunaomba ulinzi utokao kwako katika majira haya ya usiku tena. Tulale salama na kesho tuamke salama tuendelee na ratiba zetu

Tupe amani mioyoni mwetu, tufanikishie katika mahitaji yetu na tukutanishe na wale watu tunawatamanio katika maisha yetu nasi tuwe furahani. Bwana tupe zaidi ya tutamanivyo sisi
1731186453601.jpg


Tujalie amani na furaha katika mahusiano yetu pia tukumbuke nasi tusio na wenza Eee Bwana tupate wenza sahihi kwenye maisha ya ndoa ili tuifurahie maisha ya mahusiano na familia 🙏🏾

Bwana tupe watu wema ili na sisi tuwe tunalala unono na kuamka tukiwa wenye tabasamu na nguvu kwasababu tuna watu wanaotupenda💞
 
Back
Top Bottom