Magical power
JF-Expert Member
- Sep 27, 2022
- 2,158
- 5,626
Eee Bwana ni usiku tena asante kwa neema hii. Tuliikabili siku kwa juhudi zetu huku tukiwa na tumaini ndani mwetu.
Yawezekana haikuwa vile tulivyotarajia yawezekana haikuwa fungu letu kesho inaweza kuwa vile tulivyotami leo
Bwana wakati mwingine hili nililopitia leo ni kwasababu ya kusababishiwa na mtu kwa hila zake au kwa makosa yangu ya kibinadamu.
Nashinda nikiwa mwenye huzuni na nalala mwili tu akili na nafsi zinakesha zikiweweseka kwa hili nilinalopitia kwenye maisha yangu
Bwana ulisema, wewe ni mwingi wa rehema, naomba rehema zako kwenye maisha yangu.
Nipe zaidi ya nilichoporwa au kupoteza. Nipe zaidi ya nitamanivyo ili furaha yangu iwe kubwa kuliko wasemavyo watesi wangu juu ya yangu
Bwana kama kuomba kwangu kusipokuwa kitu sadaka, machozi na imani yangu iwe nguzo ya kunitendea wema wako kama ulivyowatendea watumishi wako waliokuwa kwenye mapito na changamoto mbalimbali ila uliwastahilisha na wakastahili kwenye maeneo ya matamanio yao
Bwana nitendee wema wako nami nistahahili nisipostahili na ukawe ushuda wa kesho njema.