Maombi yatawala nyumbani kwa Lulu

Maombi yatawala nyumbani kwa Lulu

Hivi hakuna kaujanja cha kulikisha hukumu, ili ujiandae hata kisaikolojia
 
Mungu hachezewi,ukiwa huna shida humjui unamjua ukiwa na shida?Maombi yapi na ukahaba ule anaofanyaga?Kwanza si alitangaza kuokoka kipindi ametoka mahabusu?Mbona hakuonyesha kuendelea?
Usimhukumu san mkuu tumwache Mungu atatenda haki
 
Hiki kikombe hakimuepuki lazima akinywe kulipa dharau aliyoonyesha kwa mama kanumba,hamna hamna miaka mitatu jela.
 
Tukumbuke Mungu hajibu baada ya sisi kum_preempty afanye tunavhotaka. Yesu aliomba had jasho la damu lakini bado alisulubiwa, Ayubu alijivika magunia na majivu lakini bado aliteseka. Mawazo ya Mungu si sawa na ya wanadamu
 
Yohana 9:31 inasema, “Tunajua kwamba Mungu hawasikilizi watu wenye dhambi. Yeye husikiliza mcha Mungu anayetimiza mapenzi yake.“ Na pia imesemekana kwamba “sala tu Mungu anasikia kutoka kwa mwenye dhambi ni sala kwa ajili ya wokovu.” Kwa madhumni hayo, , baadhi ya wengine huamini kuwa Mungu hawasikizi / au kamwe hajibu maombi ya asiyeamini. Kwa mkudhatha ingawa, Yohana 9:31 inasema kwamba Mungu hatendi miujiza kupitia kwa asiyeamini. Kwanza Yohana 5:14-15 inatuambia kwamba Mungu anajibu maombi kama yameombwa kwa mujibu wa mapenzi yake.
Kwa kifupi ni kwamba anatakiwa akae kwenye maombi ya toba!
Toba ya kilichotokea,kilichofingua mlango wa yy kuhusika na hilo tukio ! Toba tu ndo itamtoa!

Ss sijui km ana huu ufahamu,hapo kukemea ,kukataa,kubatilisha wala hakutamtoa zaidi ya toba!
 
View attachment 621810


Zikiwa zimesalia siku 12 tu kabla ya hukumu yake kusomwa kufuatia kesi yake ya kuua bila kukusudia inayomkabili, taarifa zinasema maombi na sala zimekua zikitikisa nyumbani kwa msanii Elizabeth Michael ‘Lulu’.

Mtu wa karibu wa msanii huyo alilidokeza , baada ya kesi hiyo kufikia katika hatua ya hukumu, hivi sasa kila siku maombi yanafanyika asubuhi, mchana na jioni, kwani kwa hali ilivyo hivi sasa, kila kitu kimo mikononi mwa Mungu.

“Si Lulu, si Mama yake, si ndugu zake, kila mmoja anaomba kwa muda wake, wakati mwingine kwa pamoja, au mmoja mmoja, wanachojua wao hatima ya kila kitu ipo mikononi mwa Mungu, ndiyo maana sala zinaelekezwa kwake,”

Lulu anashtakiwa kwa kosa la kumuua bila kukusudia, aliyekuwa mpenzi wake, Steven Kanumba, katika tukio lililotokea nyumbani kwa msanii huyo, Sinza Vatican mwaka 2012.

Baada ya kusikilizwa kwa ushahidi wa Jamhuri, upande wa utetezi na wazee wa mahakama, sasa hukumu hiyo itasomwa Novemba 13, mwaka huu katika Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam na Jaji Sam Rumanyika.
Kama kweli hakuhusika kwy kilichomtokea Kanumba she will be safe,hila kama ndy chanzo cha kifo....hata mahakama ikisema yupo huru hana hatia KARMA haita muacha salama....ile DAMU ya Kanumba itamfuata kwy maisha yake na kizazi chake,ndy anaweza kuja kukuta mumewe au mtoto wake nae anakufa kwy mazingira kama hayo ya Kanumba nk nk!
 
Kwa kifupi ni kwamba anatakiwa akae kwenye maombi ya toba!
Toba ya kilichotokea,kilichofingua mlango wa yy kuhusika na hilo tukio ! Toba tu ndo itamtoa!

Ss sijui km ana huu ufahamu,hapo kukemea ,kukataa,kubatilisha wala hakutamtoa zaidi ya toba!
Kwa muongozo anapaswa asome kitabu cha Zaburi 51
 
Amechelewa hawezi kubadilisha hikumu wakati ushahidi ulishatolewa,ushahidi ndiyo hukumu yenyewe angeomna zaidi mwanzo siyo mwishoni
 
Chechela aka Segedansi aka nondo aka gereza aka inside aka ndete aka lupango ,amebakiza siku mbili tu uraiani tarehe 13 ataanza kula maharage ya jela.
 
Mungu hachezewi,ukiwa huna shida humjui unamjua ukiwa na shida?Maombi yapi na ukahaba ule anaofanyaga?Kwanza si alitangaza kuokoka kipindi ametoka mahabusu?Mbona hakuonyesha kuendelea?
Sikuja kuwaita watu wema, bali wenye dhambi ili wapate kutubu.

Tukiwapenda wanaopendeka twafanya ziada gani, wapendeni waombeni wanaowaudhi...
Baba yenu wa mbinguni atawapa thawabu...
 
Back
Top Bottom