Maombolezo ya Kawawa na Rais Mpirani

Maombolezo ya Kawawa na Rais Mpirani

Aliyekufa amekufa bwana na Life goes on mi sioni tatizo kwa hilo, hatakama unamchukia mtu you must judge vitu vingine! kwendampirani ni njia moja wapo ya kupumzisha na kusahau machungu yako!!
 
100% ni upuuzi kumshutumu JK kwenda mpirani. Ndiyo Kawawa kafariki, JK kama mkuu wa serikali amefanya kila awezalo kumuenzi marehemu kawawa, kama vile kutoa siku saba za maombolezo, kushusha bendera nusu mlingoti, kupiga mizinga wakati wa mazishi nk. Na ileweke kwamba kifo cha mtu mmoja katika jamii hakiwezi kufanya shughuli zisimame, maisha yanatakiwa yaendelee kama kawaida. Kusimamisha shughuli kamwe hakutamfufua aliyekufa. Amekufa na tumemzika kwa heshima zote full stop. Sasa MMJ ulitaka maduka, mahospitali, magenge, store za bia, maofisi yote yafungwe ndiyo ujue kweli tunaombeleza kifo cha Kawawa?.
 
Nyie watu vipi?

Wengine wanakuja na maneno kama tuko karne ya 21. Sasa kutoa tangazo kuwa Taifa litakuwa kwenye msiba kwa siku 7 ndiyo karne ya 21? Si angelitoa siku tatu tu na ziishe Saa 18 jioni, saa moja kabla ya mechi. Angelifanya hivyo kuna mtu angelisema? Sanasana hata kama Maombolezo yatakuwa yameisha, wangeliweza kusimama kwa dakika 1 kumkumbuka Kawawa.

Kama tunasema maombolezo basi lazima tuheshimu. Vinginevyo basi tupindishe masaa hata kama itakuwa KUSIMAMISHA MAOMBOLEZO kwa masaa kadhaa na baadaye tuendelee na maombolezo kama nyie mnavyodai kuwa tuko karne ya 21, wakati AIR port zetu hazina VYOO, tunatapisha vyoo kama kipindi hiki cha mafuriko, foleni za barabarani kwa Dar zinatisha, na upupu mwingine kibao. So longer tuna-drive na kuangalia Panel za TV, tuna vyombo vya High tech basi na sisi tunajiona tuko karne ya 21. Jitu linaishi kwa Mgawo wa umeme na Makelele ya Generator na mwisho linasimama bila aibu kujisifu "tuko karne ya 21".

Hivi kipato cha Mtanzania kwa mwaka (wastani) ni kiasi gani vile?

Life span ya hawa Watanzania walioko karne ya 21 ni kiasi gani vile?

Karne ya 21, mhhhh my A**.
 
100% ni upuuzi kumshutumu JK kwenda mpirani. Ndiyo Kawawa kafariki, JK kama mkuu wa serikali amefanya kila awezalo kumuenzi marehemu kawawa, kama vile kutoa siku saba za maombolezo, kushusha bendera nusu mlingoti, kupiga mizinga wakati wa mazishi nk. Na ileweke kwamba kifo cha mtu mmoja katika jamii hakiwezi kufanya shughuli zisimame, maisha yanatakiwa yaendelee kama kawaida. Kusimamisha shughuli kamwe hakutamfufua aliyekufa. Amekufa na tumemzika kwa heshima zote full stop. Sasa MMJ ulitaka maduka, mahospitali, magenge, store za bia, maofisi yote yafungwe ndiyo ujue kweli tunaombeleza kifo cha Kawawa?.

Mijitu isiyokuwa na utu bwana!
 
Duuh!Kuna chuki zingine too much,maana huyo mwanakijiji amemchukia Kikwete kiasi kwamba kila anachokifanya Kikiwete ni baya na la kijinga!

Hey! Kuna tofauti kati ya chuki na kukosoa! Sidhani kwamba Mwanakijiji ama yeyote yule anayesekosoa utendaji wa Kikwete ana chuki yoyote naye. Kikwete ni Rais wa nchi yetu. Sisi kama wananchi tunao wajibu na tunayo haki ya kukosoa utendaji wake kama Rais na hatufanyi hivyo kwa chuki bali kwa kutoa mawazo yetu kama wananchi huru katika taifa huru lenye kufuata misingi ya demokrasia ya kutoa mawazo kwa uhuru midhali sheria haivunjwi. Kudai kwamba wanaomkosoa Kikwete wana chuki ni mawazo duni yasiyo na tija.
 
Mimi nafananisha kwenda kwa JK mpirani na mtu anaedai anaumwa halafu anakwenda Bar kupata mvinyo. Halafu wengine wanasema, mgonjwa alisikia kiu na ni sawa tu kwake kujipatia mvinyo.

Kinachotokea hapo si kosa la mtu huyo kwenda Bar, au kupata mvinyo. Bali ni imani aliyoijenga kwa wale aliwapa taarifa ya hali yake. Mtu huyo anakuwa anaondoa imani na kuonekana muongo kwa wale aliowapa taarifa ya ugonjwa wake, nao watadharau ugonjwa alionao. Hiyo ndiyo hali inayojidhihirisha katika mijadala hapa.

Wale wanaoona kuwa hakukuwa na tatizo kwa Mheshimiwa kwenda uwanjani kuangalia mpira, wanonyesha dhahiri pia kuwa msiba huo haukuwa na maana sana kwa Taifa, kwani aliekufa ameshakufa, na maisha yaendelee bila kuhuzunika sana. Afterall, hata tukihuzunika hatarudi tena. Nadhani hii si sahihi.

Ndio maana nasema, kama hivyo ndivyo, kwanini tulitangaziwa kwa majonzi makubwa kuhusu msiba huo? Kwanini hatukuambiwa kuwa imetokea, lakini maisha yaendelee kama kawaida? Kwanini tulijidai kuhuzunika sana?

Mtu mwenye heshima (anaejiheshimu) hutoa kauli zinazoshabihiana na matendo yake kwa kiasi kikubwa. Ikiwa kinyume, anakuwa anatafuta dharau ambazo hazikuwepo awali.
 
Hey! Kuna tofauti kati ya chuki na kukosoa! Sidhani kwamba Mwanakijiji ama yeyote yule anayesekosoa utendaji wa Kikwete ana chuki yoyote naye.

Na wengine pia wanakosoa ukosoaji wa Mwanakijiji hata kwenye jambo lisilo la zima kukosolewa. Kuna haja ya watu sasa kutoka hadharani na kutangaza azma zao ili na wengine tupate kuhoji maoni yao. Unapotangaza usafi Mwanakijiji ni bora ukawa mfano wa usafi wenyewe, kuna watu pia wanavichwa vya kufikiri kama ulivyojaaliwa wewe.
 
Namtetea, yeye kama mfiwa, nahitaji kufarijiwa, kwenda msibani ni kwenda kufariji wafiwa. Pale msibani, kuna stories nyingi sana kuwafanya wafiwa washau haraka machungu ya kuondokewa na ndugu yao. Mhe. Rais kwenda kuangalia kandanda ni moja ya hatua ya kusahau machungu ya kuondokewa na SIMBA WA VITA. Kwa hili mimi namtetea
 
Mie hata 'silii' kama unavyodai mheshimiwa Lunyungu. Kwangu mimi 'kulialia' ni pale mnapoanza kukosoa hata mambo yasiyo na mshiko kama hili la rais kuhudhuria mechi ya mpira wa miguu. Tumempoteza mheshimiwa Kawawa tangia tarehe 31 December. Taratibu zote za kitaifa zimefanyika na mazishi tayari sasa tupo kwenye 'maombolezo ya siku saba'. Tatizo ni kuhudhuria mechi? Huwa nakubaliana na hoja za msingi aziletazo Mwanakijiji lakini sio hii...Mimi sipendi kufata upepo...Mzee Lunyungu acha 'kulialia'!
.

Yadumu mawazo sahihi ya Mzee Mwanakijiji.Yadumu!!
 
Hivi tulitegemea kuwa JK alale uvunguni kule Ikulu kwa siku saba?
Wakuu this is the 21st cetury, life MUST go on.



Gwakisa, hapa tunazungumzia Rais, kiongozi mkuu wa nchi. And being a leader entails role modelling, anatakiwa aoneshe mfano. Hivi watoto na ndugu wakaribu wa marehemu kawawa wamemchukuliaje mkuu wetu kwenda kushangilia hadharani kwa furaha kubwa siku chache tu baada ya mtu anayedai kuwa alikuwa muhimu sana kufariki, na kuutangazia uma wiki ya maombolezo?.

Jamani ndo maana kunatakiwa kuwe na delegetion of responsibilities, angeenda waziri wa michezo, isingeleta muonekano mbaya na kuondoa ile mantiki nzima ya kuomboleza.
 
Gwakisa, hapa tunazungumzia Rais, kiongozi mkuu wa nchi. And being a leader entails role modelling, anatakiwa aoneshe mfano. Hivi watoto na ndugu wakaribu wa marehemu kawawa wamemchukuliaje mkuu wetu kwenda kushangilia hadharani kwa furaha kubwa siku chache tu baada ya mtu anayedai kuwa alikuwa muhimu sana kufariki, na kuutangazia uma wiki ya maombolezo?.

Jamani ndo maana kunatakiwa kuwe na delegetion of responsibilities, angeenda waziri wa michezo, isingeleta muonekano mbaya na kuondoa ile mantiki nzima ya kuomboleza.


Mjadala huu umekuwa na mvutano labda kwa sababu watu walio wengi wameshindwa kuelewa vizuri dhana ya kuomboleza. Kama tungeelewa hilo basi tusingehitaji kubishana sana.

Kwa uelewa wangu, kuomboleza kunahusisha kutofanya mambo yote ya starehe labda kama ni lazima sana. Ndiyo maana katika kipindi cha maombolezo, watu wa karibu (wafiwa), hawawezi kufanya vitu kama harusi au sherehe. Kwa msingi huo, Rais alikuwa kiongozi wetu katika shughuli hii ya kuomboleza msiba wa Mzee Kawawa ambaye alikuwa miongoni mwa waasisi wa Taifa letu. Kwa hiyo nchi nzima pamoja na Rais hatukutakiwa kujihusisha na mambo ya starehe labda pale ilipoonekana kuwa haiepukiki. Na katika mazingira hayo, kunakuwa na masharti kuendesha sherehe au shughuli hiyo. Pamoja na taratibu zilizofuatwa katika mchezo wa jana, halikuwa jambo la busara kwa kiongozi wa waombolezaji kuhudhuria mchezo huo. Kwa maoni yangu Rais wetu hakutakiwa kuwepo uwanjani kama ambavyo asingeweza kuandaa dhifa ya kitaifa kwa Kiongozi yeyote ambaye angemtembelea Ikulu.

Hata hivyo Watanzania tumeingiwa kasumba mbaya ya kuamini kuwa kila kitu katika kuasisi Taifa letu kilifanywa na Nyerere kwa hiyo yeye tu ndiye anayestahili kiwango kikubwa cha kutambuliwa mchango wake. Ni jambo la hatari kujaribu kuiweka historia nzima juu ya kichwa cha mtu mmoja. Jambo ambalo ni kosa kubwa na kutowatendea haki wote waliotoa michango muhimu sana.
 
Nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. hivi alishindwa hata kujibanza Ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?
acheni ujinga kama Kawawa amekufa so what shughuli za kitaifa zisimame na wanamichezo vipi hawahitaji support yake! Muende mkalale muache topic zisizo na miguu!
 
nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa waziri mkuu na makamu wa rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. Hivi alishindwa hata kujibanza ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?


mzee hii ni staili yako ya kupunzika kabla ya kutuletea skendo jengine la muungwana? Hivyo ukingojea bufee unatafuna nuts au sivyo?
 
Mzee wetu Rashidi Mfaume Kawawa alikuwa na sifa zifuatazo kati ya sifa nyingi
1. Moja ya wasisi wa taifa letu
2. Mwasisi wa TANU na CCM
3. Mtetezi wa wanyonge
4. Simba wa vita
5.Mwanamichezo mahiri
6.etc etc

Ili kumuenzi tunatakiwa tufanya yale yote mazuri aliyapenda na kuyasimamia na hapa rais kama kiongazi wa nchi na mwanamichezo aikuwa anatekeleza kwa vitendo moja ya sifa za Mzee wetu Kawawa. Jamani sio lazima ulie sana au uvae nguo nyeusi au ujifungie chumabani wakati wa msiba ndipo uonekane unaomboleza sana. Unaweza kucheka na kuimba na bado ukawa unaomboleza kwa dhati ya moyo.
 
Code:
Nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. hivi alishindwa hata kujibanza Ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?
Code:

Nakushangaaa Mwanakijiji. Tena ulimwengu utanishangaa sana kwa nini shangai watu wanaoshangaza kama wewe.

Unafiki wa Muungwana umeuona jana kwenye mpira tu? Unashangaa anapofanya jambo ambalo yeye mwenyewe kwa maneno humaanisha hatafanya?

Nenda kawaulize wabunge hotuba aliyoitoa wakati anazindua ofisi ile ya uwakilishi wa watanzania uliza wabunge ametimiza mangapi.

Kama unadhani ni utani kawaulize wakazi wa Loliondo wakati wanapata ile taabu ya Krne Muungwana alikuwa hotele ipi akila Raha mwenyewe anasema alikuwa amepumzika.

Unashangaa nini wakati hadi sasa watanzania wanakufa kwa Malaria yeye akiwa Mwenyekiti wa Chama anaruhusu ununuliwaji wa magari bei mbaya ya Chama chake kwa ajili ya kampeni?

Au huelewi kuwa wakati kuna watanzania wanakufa kwa kushindwa kujifungua tena kwenye hospitali ya serikali mtumishi mmoja wa Ofisi ya Umma anajengewa Jumba la zaidi ya shilingi Bilioni 1 na yeye amekaa kimya?

Unajifanya hujui kuwa Muungwana kila wiki lazima apoteze lita zaidi ya 500 kwa msafara wake wa magari zaidi ya 10 yanayoenda na kurudi kukagua HEKALU lake Chalinze ilhali wana wengi wa chalinze hata mlo mmoja kwao ni mtihani?

Usijifanye hujui kuwa wahuni waliua mifugo na raia Tarime kwa sumu ya kutoka kwenye mgodi lakini yeye anakenua meno tu utadhani waliokuwa wanadhurika ni mende.

Kawawa ni nani kwa Muungwana? Kama watu wake anawaona hawana maana, Msiba wa Kawawa hauna maana yoyote kwa Muungwana.

Najua unajua na unajua kuwa tunajua kama unajua sema unataka kutest mindsets zetu.
 
NADHANI KATIKA HILI WAKULAUMIWA NI WEWE NA SI J.K;

KAMA RAIS WA NCHI, IVORYCOST NI TIMU KUBWA NA UKUMBUKE RAIS KATIKA MOJA YA AHADI ZAKE KWETU WATANZANIA (sijasema wana-CCM) ALITUAHIDI KUINUA SOKA LA BONGO...NA NAAMINI KWA KUMLETA MAXIMO, KUKUSOA USIMAMIZI WA MPIRA NCHINI KWA BUSARA, KUHASISHA UTALII (UWANJA MPYA) HAS KWA FAINALI ZA KOMBE LA DUNIA 2010 ALISTAHILI KUWEPO GIVEN ALIKUWEPO NCHIN, KAMA ANGEKUWA KWENYE "BEMBEA" INGEKUWA TOFAUTI.

ITAFIKIA KIPINDI MTASEMA RAIS HATA ****** ASIENDE KWASABABU ANAMSIBA (KWANI KUJISAIDIA NAYO SI STAREHE?)
 
Wakuu, hivi unafikiri wale viongozi wote walio na falsafa za Nyerere na ambao ni waasisi wa taifa na Azimio la Arusha wanatakiwa?? Kakwambia nani?? Ni lazima tujifanya kuwa tunaomboleza lakini kwa matendo na moyoni ni opposite!!! Wanafiki bwana!!
 
siungi mkono kwa hilo Rais yupo sahihi kabisa kwenda uwanjani mzee!!!ni kweli msiba ulikuwepo lakini umeshapita sasa tunapoteza mawazo na kama ulitaka rais asiende basi mashabiki wote wasingeenda kwa hilo mzee umepotoka kumkosoa rais kwa kwenda mpirani mbona msibani baada tu ya maziko watu huwa wanacheza bao!suala ni kwamba ni mpirani na sio kwenye bar au sehemu yeyote ya anasa embu msimchafue Rais wetu yupo sahihi kabisa namuunga mkono!pamija na watanzania wote waliofika uwanjani!
 
100% ni upuuzi kumshutumu JK kwenda mpirani. Ndiyo Kawawa kafariki, JK kama mkuu wa serikali amefanya kila awezalo kumuenzi marehemu kawawa, kama vile kutoa siku saba za maombolezo, kushusha bendera nusu mlingoti, kupiga mizinga wakati wa mazishi nk. Na ileweke kwamba kifo cha mtu mmoja katika jamii hakiwezi kufanya shughuli zisimame, maisha yanatakiwa yaendelee kama kawaida. Kusimamisha shughuli kamwe hakutamfufua aliyekufa. Amekufa na tumemzika kwa heshima zote full stop. Sasa MMJ ulitaka maduka, mahospitali, magenge, store za bia, maofisi yote yafungwe ndiyo ujue kweli tunaombeleza kifo cha Kawawa?.
uko sawa kabisa ndugu kidatu,kufa amekufa hatorudi huyo,maisha yanaenda mbele,iliyobaki tumuombee dua kwa mwenyezi mungu amlaze mahali pama peponi amin,je kama fainali za kombe la dunia zinaendelea kuchezwa ghafla kafariki sepp blater ambae ni rais wa fifa je fainali za mwaka huo zitafutwa au zitasimamishwa au watasimama kwa dakika 1 na soka litaendelea kama kawa,acheni kukosoa kila kitu,kama mna chuki binafsi semeni au wivu?
 
Back
Top Bottom