Maombolezo ya Kawawa na Rais Mpirani

Maombolezo ya Kawawa na Rais Mpirani

FMES
ninasema hivi Rais kwenda mpira wa timu ya taifa wakati wa maombolezo ya taifa hakuvunja sheria, kama unaijua sheria aliyoivunja iweke hapa,
Mkuu FMES,

Sometimes your arrogance startles! Hakuna mahali niliposoma uliposolewa ama hoja yako kupingwa na kukubali! There are people who know better/more than you can imagine. Anyway peace! Pamoja na ubishi wako naiheshimu michango yako!

Boramaisha

FMEs,

Hakuna anayebisha kwamba hakuna sheria inayomlazimisha Rais kwenda ama kutokwenda mpirani. Nilichofanya nikutoa mawazo yangu kuhusu suala la Rais kukubali kwenda mpirani na suala la kupangiwa Ratiba, kuifuata jinsi ilivyo na kwamba hawezi kuikataa ama kuibadilisha. Hiyo ndiyo hoja yako au labda ni sub-hoja ambayo mimi nimeipinga.

You are lucky to be a 'great thinker' but at the end of it all this is just a 'discussion forum' nothing spectacular.

Peace!
- Incredible!

FMEs!
 
tuli enjoy sana ile siku. pamoja na kufungwa lakini tuliishangilia timu kwa nguvu zote na kwa kweli vijana walijitahidi sana. kulikuwa na ari kubwa sana hasa ya ushangiliaji, na vile Presida yupo!!!! ilikuwa raha sana
tulikuwa na msiba sawa lakini ni kawaida tukishatoka kuzika ile jioni tunapata one two one two
mbona watu wa musoma huwa wanapiga music kabisa jamani?

ile ziara ilipangwa kabla ya msiba na hakukuwa na sababu kuuubwa ya kuahirisha.
 
Nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. hivi alishindwa hata kujibanza Ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?

mkuu pana msemo kuwa ya kale hayanuki....

si unajua huyu alikuwa PM kwenye 60s huko, ile hisia ya kuwa ni mwenzetu inalazimishwa tu lakini sitaki kuamini kama kweli ipo kutoka mioyoni mwa viongozi wetu wengi kama inavyodaiwa isipokuwa kwa wale ambao ni rika lake.

kwa hiyo ni muhali watu kufikiria kwa mtazamo wako...kama ingekuwa ni wa kizazi hiki kilichopo madarakani...pengine wangefanya kama ambavyo unadhani ingekuwa stahiki...

lakini pia mkuu nani angetaka kuikosa ile Big Ocassion ya kumuona Drogba live....si unajua tena ulimbukeni wetu...najiuliza kama the galacticos wa madrid wanakuja one day yes itakuwaje? si ajabu serikali yote kasoro wale ambao hawakuwahi hata kucheza chandimu watahamia uwanja mpya...hata kama ni kutoka kamachumu, dakawa ili mradi waje kuwaona akina CR, Kaka & Co

ni mtazamo tu....
 
si kweli; hivi leo hii Taifa Stars ingeifunga Ivory Coast si tungeshabikia kwa kuchanga nusu bilioni nyingi kuisaidia Stars kama tulivyofanya ilipoifunga Togo; Rais hakuwa na sababu hata chembe ya kwenda kwenye mechi hii ya kirafiki isiyo na umuhimu wowote (i repeat haina umuhimu wowote ule) kwa soka la tanzania. Tunajidanganya tukifikiria kuwa kwa kucheza na Ivory Coast basi wachezaji wetu wamejifunza kitu.. Si tulifikiria hivyo hivyo walipoenda Brazili?

Ni nani leo hii akiwa amefiwa na ndugu yake ambaye amemzika siku mbili nyuma anaenda kucheza cheza na kuruka ruka kwenye michezo isiyo na maana wala mantiki?

Aliyetutangazia msiba huu "mkubwa wa kitaifa" na ambaye alishindwa kujizuia machozi ndiye wa kwanza kwenda kushangilia mechi ya mpira ambayo matokeo yake hayana maana yoyote kwa Taifa Stars wale kwa Ivory Coast zaidi ya kuwapa taste ya matumizi ya uwanja wetu mpya..

unarudi palepale kwenye ku-personalize issues, huyu sio ndugu ni kiongozi tu na tumempa heshima yote anayotakiwa kupata kama kiongozi akifa!

na pia hiyo mechi sio kuchezecheza tu, sio kama mtoto ataenda nje akafuma mpira wa manailoni akaanza kucheza, hiyo mechi imeandaliwa kwa muda mrefu na kwa kutumia pesa nyingi, sasa tuhairishe mambo makubwa tuliyopanga juu ya mtu aliyefariki siku chache zilizopita?

No wonder watanzania hatuendeleo, kwa ajili ya kuendekeza mambo madogomadogo, sasa kama tunaomboleza siku saba, mbona baa na kumbi za starehe hazijafungwa?
 
kwa hoja hii JK unamuonea jamani, mnyonge mnyongeni haki yake mpeni, jamani kwenda kwenye mechi wakati wa maombolezo ya Kawawa nayo nongwa? KHA!
 
Kwa waisilamu, mkimaliza mazisha mnaendelea na shughuli zenu kama kawaida; bila shaka marehemu alikufa akiwa muisilamu.
 
Nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. hivi alishindwa hata kujibanza Ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?
Wakati mwingine Mwanakijiji unakuwa kama 'mviziaji' yaani kiongozi akiteleza kidogo tu we unabandika!
 
tunampa pongezi Rais Kikwete kwa kuongoza ushangiliaji wa timu yetu ya Taifa Stars dhidi ya Ivory Coast.
 
Nilidhania taifa liko kwenye maombolezo ya aliyekuwa Waziri Mkuu na Makamu wa Rais na muasisi wa taifa hili kwa siku saba. Aliyetutangazia maombolezo hayo yuko mpirani kuhamasisha ushindi.. hivi alishindwa hata kujibanza Ikulu kuangalia kwenye big screen na kumtuma waziri mmoja hivi..kweli ilimpasa kwenda?

Huyu ndo JK bwana.Usanii mpaka kwenye misiba
 
Sasa naona inatupa kupitisha sheria za viongozi wakuu a nchi wakifa tubaki siku ngapi bila ya kufanya kazi sio kama hivi kila wakati
 
Mkuu, umemaliza kabisa.

Sitegemei makubwa kutokana na dakika 90 za mchezo wa kirafiki kati ya Taifa Stars na Ivory Coast katika kuitangaza nchi.

Biashara gani ambayo inatangazwa kwa kuonyeshwa kwenye TV za Taifa tu?

get your facts right, hiyo mechi waandishi wa CNN na BBC walikuwepo, sasa sijui we uko under which stone ambako hujui linaloendelea, lakini unapanda kulicommentia!

Sijawahi kuona matangazo yoyote ya uwanja huo kwenye DSTv, CNN wala channels nyingine za kimataifa.

Sasa kwani ni hadi wewe uone ndio kuwe na tangazo, kwani hujui kuwa TBC ni moja ya chanels za DSTv? na hao CNN walikuwepo uwanjani siku hiyo!
ndio maana watanzania hatuendelei tuko negative sana, hadi inakera!KHA!
 
get your facts right, hiyo mechi waandishi wa CNN na BBC walikuwepo, sasa sijui we uko under which stone ambako hujui linaloendelea, lakini unapanda kulicommentia!

Utakuwa unatania.

Sasa kwani ni hadi wewe uone ndio kuwe na tangazo, kwani hujui kuwa TBC ni moja ya chanels za DSTv? na hao CNN walikuwepo uwanjani siku hiyo!
ndio maana watanzania hatuendelei tuko negative sana, hadi inakera!KHA!

Hiyo TBC1 inaonyeshwa na DSTv hapo hapo Tanzania tu. Sehemu nyingine zote iko Scrambled (if you know what I mean). CNN wameonyesha huo mpira saa ngapi na lini?

Si lazima nione mimi ndio kuwe na tangazo. Wewe kama unajua imeonyeshwa, sema tu utaeleweka. Huna haja ya kukaza misuli ya shingo. Utajiumiza bure tu.
 
Mzee mwanakijiji Sitarajii mwelewa kama wewe uwe na chuki zisizo na msingi[nachelea kutumia neno halisi kwa kuhishimu JF Lakini inaelekea una biff kubwa na bwana Mzee. Wenzangu nyie alivyoahirisha spichi yake ya mwaka ambayo ilitakiwa aitowe mlimponda sana na kusema ingawa kuna msiba lakini ile spich ni ;national issue na ni muhimu angeitowa siku ya mkesha. Maskini jamaa alifanya vile kwa sababu ambayo watu wa kawaida walielewa. Na alipotoa hiyo spich siku ya tarehe 1 mkaanza kuiponda sasa tarehe 4 amekwenda kwenye shughuli ya kitaifa mnasema mbona nyinyi wazee mlianza sherehe ya mwaka mpya kwa kunywa kustarehe hivi ule msiba nyie haukuwahusu????

ingawa nimeshakuthank, naomba nikushukuru...akhsante!
labda sasa wataelewa!
binadamu hamridhiki, loh, hata kama JK anasoma humu kupata mawazo ya kujenga taifa sasa ataona mnamkomfuse tu na hamna tofauti na watu wa vijiweni! KHA!
 
si kweli; hivi leo hii Taifa Stars ingeifunga Ivory Coast si tungeshabikia kwa kuchanga nusu bilioni nyingi kuisaidia Stars kama tulivyofanya ilipoifunga Togo; Rais hakuwa na sababu hata chembe ya kwenda kwenye mechi hii ya kirafiki isiyo na umuhimu wowote (i repeat haina umuhimu wowote ule) kwa soka la tanzania. Tunajidanganya tukifikiria kuwa kwa kucheza na Ivory Coast basi wachezaji wetu wamejifunza kitu.. Si tulifikiria hivyo hivyo walipoenda Brazili?

Ni nani leo hii akiwa amefiwa na ndugu yake ambaye amemzika siku mbili nyuma anaenda kucheza cheza na kuruka ruka kwenye michezo isiyo na maana wala mantiki?

Aliyetutangazia msiba huu "mkubwa wa kitaifa" na ambaye alishindwa kujizuia machozi ndiye wa kwanza kwenda kushangilia mechi ya mpira ambayo matokeo yake hayana maana yoyote kwa Taifa Stars wale kwa Ivory Coast zaidi ya kuwapa taste ya matumizi ya uwanja wetu mpya..

Sasa nani alaumiwe kwa kuchezwa kwa mechi hii? Nafikiri mentality kama hizi zinachangia kurudi kwetu nyuma kwa kutafuta kila sababu za kutofanya kazi kila tunapopata nafasi. Kama kweli ni maombolezo ya siku saba kama ambavyo unataka ieleweke, maana yake watu wasiende kazini kwa siku saba, ni kiasi gani cha pesa taifa litapoteza? Kumbuka hata hiyo mechi ni mojawapo ya vyanzo vya pesa, sio burudani tu! Huu utamaduni wa kujikongoja utatutoka lini? We need to be aggressive, Kawawa (RIP) katutoka lakini maisha yetu yanaendelea kama kawaida....kwa wana familia ni vema wakaendelea na maombolezo lakini si kwa nchi nzima....tukiambiwa wabongo tuna mentality ya uvivu tunakasirika!!
 
Mimi nafananisha kwenda kwa JK mpirani na mtu anaedai anaumwa halafu anakwenda Bar kupata mvinyo. Halafu wengine wanasema, mgonjwa alisikia kiu na ni sawa tu kwake kujipatia mvinyo.

Kinachotokea hapo si kosa la mtu huyo kwenda Bar, au kupata mvinyo. Bali ni imani aliyoijenga kwa wale aliwapa taarifa ya hali yake. Mtu huyo anakuwa anaondoa imani na kuonekana muongo kwa wale aliowapa taarifa ya ugonjwa wake, nao watadharau ugonjwa alionao. Hiyo ndiyo hali inayojidhihirisha katika mijadala hapa.

Wale wanaoona kuwa hakukuwa na tatizo kwa Mheshimiwa kwenda uwanjani kuangalia mpira, wanonyesha dhahiri pia kuwa msiba huo haukuwa na maana sana kwa Taifa, kwani aliekufa ameshakufa, na maisha yaendelee bila kuhuzunika sana. Afterall, hata tukihuzunika hatarudi tena. Nadhani hii si sahihi.

Ndio maana nasema, kama hivyo ndivyo, kwanini tulitangaziwa kwa majonzi makubwa kuhusu msiba huo? Kwanini hatukuambiwa kuwa imetokea, lakini maisha yaendelee kama kawaida? Kwanini tulijidai kuhuzunika sana?

Mtu mwenye heshima (anaejiheshimu) hutoa kauli zinazoshabihiana na matendo yake kwa kiasi kikubwa. Ikiwa kinyume, anakuwa anatafuta dharau ambazo hazikuwepo awali.

wabongo tuna matatizo, KHA!
 
Nona baadhi ya watu wanaanza kubadilisha mjadala.

Hakuna aliesema mechi isingechezwa kwa sababu ya msiba ule mkubwa. Kwanini isichezwe wakati pamoja na umashuhuri wa marehemu, si kila mtu alieguswa na msiba ule kiasi hicho? Na pia mechi ile ilishapangwa na si ajabu isingeweza kubadilishwa. Maana nafasi ya kufanya hivyo labda isiwepo tena kwa siku chache zijazo.

Kinachoshangaza baada ya watu ni hatua ya Mkuu wa nchi kutangaza kwa masikitiko msiba mkubwa kwa Taifa, kutangaza maombolezo ya siku 7 na baada ya camera kuondolewa, akaenda uwanjani kushangilia mpira. Ni hiyo tu basi.
 
Utakuwa unatania.

Hiyo TBC1 inaonyeshwa na DSTv hapo hapo Tanzania tu. Sehemu nyingine zote iko Scrambled (if you know what I mean). CNN wameonyesha huo mpira saa ngapi na lini?

Si lazima nione mimi ndio kuwe na tangazo. Wewe kama unajua imeonyeshwa, sema tu utaeleweka. Huna haja ya kukaza misuli ya shingo. Utajiumiza bure tu.

tatizo unadhani mpira kuonyeshwa lazima iwe LIVE, mi nimesema CNN na BBC walikuwepo, nikimaanisha walikua wanarekodi hilo pambano (na sio lazima iwe kwa taarifa ya habari, labda ni kwa kipindi fulani, sasa mi siwezi jua wataonyesha lini na saa ngapi, na pia wanaweza kutupa hizo materials tusizione milele, waandishi wa habari wanajua material kutotumika kwenye TV, radio au gazeti ni kitu cha kawaida)), kama unabisha juu ya uwepo wao i cant help it as mi najua kuwa walikuwepo!
 
Mi nafikiri kuna tofauti kati ya maombolezo na bendera kupepea nusu mlingoti. Nafikiri kinachofanyika ni bendera kupepea nusu mlingoti lakini kama ni maombolezo huwezi omboleza kwa burudani (kwenda mpirani).
1999 baada ya kifo cha Nyerere tulikaa mwezi mzima bila mipira kuchezwa wala TV na vyombo vya habari kutangaza au kuonesha burudani
OMG! This is 21st Century, WAKE UP!!
Hivi ni nchi gani umewahi kusikia mambo kama hayo?!
 
NAsema hivi, kwetu ndingala na pombe hufanyika kwenye msiba wa mtu mashuhuri. Sio hayo tu, kimele na kibota ni usiku kucha kiasi kwamba kina kaka na dada hupashana moto migombani kwa sana tu na hata nyumba ndogo huserebuka sana kwa kisingizio cha msiba. Ni kwa sababu ya uharibifu wa kufyeka kila kitu kwa jazba kwa kutumia mikuki kwenye ndingala (ngoma ya kilio) ilipigwa marufuku labda kama inachezwa kwa low grade morale. Lakini pombe na ling'oma bado hadi kesho hasa kwa marehemu aliyekuwa mshiriki wa ngoma hiyo.

Siku 7 za msiba hazikusema tusiende kazini na tusichane nywele au kupaka mafuta vichwa vyetu. Kawawa alikuwa nambari moja Simba Sports Club na Kikwete kaenda kumuenzi baba yake kwa mchezo huo, hakucheza mwenyewe. Kipi bora, angekaa ofisini kutwanga mzigo kama kawa, au alie mfululizo siku 7 na asile wala kunywa?

Sijaona ubaya hapo.

Leka
Naloli kangi naloli
 
Back
Top Bottom