Maonesho ya Biashara ya China CIIE yaongeza idadi ya wateja wa makampuni ya Afrika

Maonesho ya Biashara ya China CIIE yaongeza idadi ya wateja wa makampuni ya Afrika

ldleo

JF-Expert Member
Joined
Jan 9, 2010
Posts
1,116
Reaction score
1,121
379.jpg


Maonesho ya kimataifa ya Uagizaji Bidhaa nchini China (CIIE) ya mwaka 2022, yamemalizika hivi karibuni huko Shanghai. Maonesho haya yameonekana kuongeza chachu kwenye uhusiano wa kiuchumi na kuufanya uendelee mbele zaidi, baada ya mikataba iliyosainiwa na makampuni yaliyoshiriki kwenye maonesho hayo kuzidi dola za kimarekani bilioni nne.

Mbali na kutoa fursa kwa nchi za mabara mengine, maonesho haya ya CIIE pia ni jukwaa zuri kwa makampuni ya Afrika kuweza kujipenyeza katika soko kubwa la China na kuonesha bidhaa zao, kutangaza chapa zao, na kutafuta washirika zaidi wa kibiashara katika nchi hii ambayo ni ya pili kwa uchumi mkubwa duniani pamoja na nchi nyingine mbalimbali. Kwa makampuni ya Afrika fursa tayari ipo mbele yao, kubwa ni kuhakikisha kwamba wanazichangamkia na kuzinyakua, kwani ukweli umethibitsha kuwa China ina nia na hamu kubwa ya kushirikiana na nchi za Afrika kukuza uchumi wake.

Kwa miongo miwili iliyopita, mtazamo wa kiuchumi wa China barani Afrika unaweza kuonekana kwenye maeneo mawili ambayo ni Uwekezaji na Biashara. Tangu mwaka 2000, kiwango cha biashara kati ya China na Afrika kimeongezeka zaidi ya mara 17. Wakati huo huo, uwekezaji wa China barani Afrika umeongezeka zaidi ya mara 100.

Jicho la China kwenye maonesho hayo lilikuwa kwa Afrika kwasababu nchi nyingi za Afrika sasa zinajiendeleza vizuri, hasa katika uwezo wake wa Pato la Taifa (GDP) na viwanda. Kwa hiyo makampuni ya Afrika yanapaswa kutumia maonesho ya CIIE, kama hamasa ya kukuza uchumi wao. Makampuni mengi kwa sasa yanajitahidi kujitokeza na kushiriki kwenye maonesho haya, lakini hata hivyo muitikio bado haujawa wa kuridhisha sana.

Afrika Kusini imeshiriki katika maonesho ya Shanghai CIIE kwa miaka mitano mfululizo. Licha ya athari za COVID-19, makampuni ya biashara ya Afrika Kusini yalishiriki kikamilifu katika maonesho ya miaka ya nyuma na mwaka huu, yakitangaza kwa nguvu nyama ya ng'ombe, mvinyo, chai na bidhaa nyingine za kilimo zenye ubora wa juu, ambapo katika mwaka 2020 mauzo yalifikia dola za Kimarekani milioni 210. mwaka 2021, mauzo ya mvinyo mwekundu, matunda, chai, na bidhaa nyinginezo yalifikia takriban dola milioni 38, na kuweka msingi imara kwa bidhaa za ubora wa juu za Afrika Kusini kupanua soko lake hapa nchini China.

Kahawa ya Rwanda nayo pia inapokelewa vyema na Wachina kutokana na harufu yake ya kuvutia. Maonesho haya yametoa fursa kwa makampuni ya kahawa ya Rwanda kujitangaza kwa Wachina ili kuongeza masoko yao. Kupitia maonesho haya kahawa ya Gorilla ambayo imejizolea umaarufu sana nchini Rwanda, umaarufu huo kwa sasa umefika hadi China. Kupitia maonesho ya CIIE, bidhaa hii sasa imeongeza idadi ya wateja kutoka soko la China, na pia kuongeza ajira katika mashamba ya kahawa huko nchini Rwanda.

Hata hivyo, uhusiano wa kibiashara kati ya China na Afrika pia umekuwa ukikabiliwa na suala la usawa wa kibiashara kwani tatizo la nakisi ya biashara limekuwa likionekana muda mrefu. Wakati Afrika ikiagiza kiasi kikubwa cha bidhaa za viwandani, mashine na vifaa vya elektroniki kutoka China, mauzo ya bara la Afrika nchini China zaidi yanajumuisha madini na metali.

Ili kuondoa tatizo kama hilo, ndio maana China inatengeza fursa mbalimbali yakiwemo maonesho kama haya ya CIIE, na kuzifanya nchi za Afrika zizidi kutanua mbawa zake kibiashara, na sio kuishia kwenye madini na metali ama bidhaa ndogo ndogo tu. Nchi za Afrika zikiwa zinasafirisha malighafi na bidha zilizokamilika nchini China, hiyo ndio italeta matokeo ya kunufaishna ambayo yanahitajika katika mfumo wa biashara kimataifa.

Takwimu za biashara kati ya China na Afrika zimekuwa za kushangaza. Kwa mfano, kwa mujibu wa Wizara ya Biashara ya China, mwaka 2018, kiwango cha biashara kati ya China na Afrika kilifikia dola za Marekani bilioni 204.2, ikiwa ni asilimia 20 kila mwaka. Zikilinganishwa na mwaka huo huo wa 2018, biashara kati ya Afrika na Marekani ilipungua hadi dola za Marekani bilioni 61, ikiwa ni asilimia 45 tu ya thamani yake ya mwaka 2008. Hivyo wakati milango ya China ikiwa iko wazi kwenye masuala ya biashara, Afrika inapaswa kutumia milango hiyo kuingia na kunufaika na matunda ya ushirikiano huu tunaotarajia udumu milele.
 
Back
Top Bottom