Tetesi: Maonesho ya Biashara ya Kimataifa ( SABASABA ) kudorora tena kwa mara nyingine

Nilikuwa na moto wa kwenda Sabasaba baada ya kuondoka nchini kwa miaka mingi.

Nilivyorudi nilikuwa disappointed.

Nilikuta Sabasaba pameachwa bila matengenezo miaka mingi, vyoo vinanuka kiasi cha kuweza kusababisha magonjwa, kilichonisikitisha zaidi, mabanda mengi yakikuea yanafungwa saa 12. Nikauliza kwa nini? Wakasema wanaogopa wizi usiku.

Nikaona kuna sababu nyingi uchumi wetu unakuwa na matatizo mengi.
 
Ni kweli mkuu, huwa wanakuja kuuza bidhaa zao sio maonyesho, mwaka huu itakuwa maonyesho ya kweli na kutoa bidhaa za bure za promosheni
Hao wa kimataifa watakuja kumuonyesha nani bidhaa zao wakati wanajua wafanyabiashara wa ndani wanaogopa kufanya uwekezaji kwa hofu ya kukamatwa
 
Mbona pale mlimani city na rock city mail huwa tunaingia bureee na kuna hadhi kuliko huko sabasaba, tena na uchumi wenyewe huu siji kabisa
 
Naomba kujua taratibu za kupata mabanda uko sabasaba
 
Nayataman sana tena siku ya kwanza tu naenda na suzuk carry kusomba vya bure bure halaf nakuja kuwaumiza mtaan
 
Vibaka wote wanahamia hapo , polisi baada ya kujinyakulia rushwa mlangoni wakati wa mchana , huelekea banda la Kizota kula Kitimoto .
 
Uko sahihi mkuu.
 
Vibaka wote wanahamia hapo , polisi baada ya kujinyakulia rushwa mlangoni wakati wa mchana , huelekea banda la Kizota kula Kitimoto .
Kuna kipindi miaka ya tisini nilikuwa naingia Sabasaba baada ya kutoka kazini. Nimeulamba, simu kwenye mkanda.

Kibaka mmoja akanitime akachukua simu.

Hakujua kwamba ni kama nimesomea Israeli na sijawahi kuibiwa.

Nikamshtukia palepale, bado kidogo nimuitie mwizi watu wamchome moto.

Akanirudishia simu yangu.

Kwa hiyo naelewa vibaka wanahamia, lakini polisi kama unavyosema, wanacheza.
 
Hapana, hii ni namna ya kuchuja vibaka, wavuta bangi, wakabaji na watu wengine wa aina hiyo.

Hiyo haipaswi kuwa njia pekee ya kuchuja vibala, wezi na wavuta bangi, njia nzuri Ni kuimarisha ulinzi Na usalama tu that is the best practice na kuwapa wananchi mzigo wa kulipa viingilio ! Mbona Kariakoo Watu huenda bila viingilio? Mbona Kwenye ma malls Na super market Watu huingia bila viingilio? Kwa hiyo hoja yako haina mashiko!
 
Hv hua ni Maonesho au Maonyesho pls leo niwekeni sawa.
 
Napendekeza pawe na kiingilio cha kuingia kko
 
Japo ni mapema lakini kuna kila dalili ya andiko hili kutimia .
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…