Manyunchwi
JF-Expert Member
- May 11, 2013
- 431
- 149
M
Maonesho kama neno linavyomaanisha ni watu waingie kuona, watapata taarifa za bidhaa... ubora, bei, matumizi, faida nk... biashara itaanza pale na hasa baadae... pale ni matangazo ya bidhaa... hali itakapokuwa nzuri bidhaa zitauzika tuu... sio lazima pale.... Sabasaba sio mtaa wa Kongo au Karume...Kwa kuzingatia uzoefu maonesho ya aina ile na maudhui Yake ni kuwa ilipaswa Watu wawe wanaingia bure ili mradi kunakuwa na umakini mkubwa ktk kuzingatia ulinzi na usalama Kwa ujumla wake ndivyo nchi nyingine kufanya, sasa haya ya hapa kwetu sijui Kwa nini wanataka Watu waingie Kwa kulipia ? Yani kwenda kuona bidhaa au huduma zinazozalishwa au kuuzwa na Watu au makampuni Mimi mwananchi nilipie? [emoji87][emoji87][emoji87] yani ni Kwa mfano Mtu anataka kuingia Kwenye Mall au supermarket halafu Kabla ya kuingia aambiwe lipa kwanza kiingilio kwa pesa ndo ukafanye window shopping au ukanunue unachotaka, je hiyo inaingia akilini? Binafsi naona siyo Sawa hata kidogo! Mwenye hoja tofauti aseme!