Think2
JF-Expert Member
- Jan 3, 2025
- 3,087
- 6,024
Nanenane ni siku ya wakulima kuonyesha bidhaa zao za kilimo, ikiwemo teknolojia za kilimo ambazo zitawasaidia wakulima kuongeza ufanisi katika kilimo.
Lakini siku za hivi karibuni, maonyesho haya yamevamiwa na wafanyabiashara wasiokuwa wakulima, jambo ambalo limesababisha kwa kiasi kikubwa kushuka kwa hadhi na uhamasishaji wa kilimo nchini.
Ambapo wafanyabiashara mbalimbali wa mitumba, masufuria na majagi wameteka maonyesho haya. Leo ukienda Nanenane utakuta hata wachezesha kamari nao wamekuja kuonyesha "kilimo" chao!!
Leo ukienda Nanenane utawakuta Vodacom, mtandao wa blue na njano, Airtel na wengine wengi. Sasa hawa wanahamasisha kilimo au nini?
Na muuza masufuria naye anahamasisha kilimo?
Makampuni ya vileo nayo yanahamasisha kilimo?
Itoshe kusema kwamba hadhi na malengo ya siku ya Nanenane yamepotea. Siyo tena siku ya wakulima, bali ya wafanyabiashara.
KILIMO KINAENDA KUANGAMIA. TUWAOMBE SERIKALI MUANZISHE SIKU ZA WAFANYABIASHARA, NA SIKU YA NANENANE IBAKI KUWA SIKU YA WAKULIMA.