Maoni: Bila kuathiri Katiba, Spika Ndugai anapaswa kujiuzulu

Nchi ina wananchi ambao hawatakiwi kuzungumza lolote ambalo ni kinyume na mtawala wa nchi.

Ni jambo la ajabu na sio haki kabisa.

Kwanini watu hawatakiwi kusema lolote wanatakiwa wakae kimya tu??
Akina Lisu walivyokuwa wanatoa maoni tofauti na akina jiwe walivyoshambuliwa mbona ulikenua meno?
Acha unafiki
 
M
Nchi ina wananchi ambao hawatakiwi kuzungumza lolote ambalo ni kinyume na mtawala wa nchi.

Ni jambo la ajabu na sio haki kabisa.

Kwanini watu hawatakiwi kusema lolote wanatakiwa wakae kimya tu??
Mda wa kuzungumza umekwisha,kazi iendelee.
 
Haujui darasa linarudishaje mkopo? Seriously!!!
 
Hagombei tena Uspika na alitamka mahali fulani.
Pensheni ya Spika mstaafu inakidhi kuishi maisha mazuri muda wote.
Labda zitumike kanuni za kumlazimisha kujiudhuru. Ila yeye kama yeye hajiudhuru kamwe
 
Mbona hakuwahi kusema kwenye awamu iliyopita..Kulikuwa na ugumu gani wa kuongea Hilo swala na uongozi bila kadamnasi..
Huyu anatakiwa ajitafakari achukue hatua..huwezi kupingana na mwenyekiti wa chama na amiri jeshi mkuu hadharani bado mkaendelea kufanya kazi pamoja..Sema mama ni mvumilivu sana..na ni mpenda demokrasia
Kazi iendelee
 
Kutoa maoni siku hizi wameitoa kwenye Katiba ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977?
 
Kosa lake ni kutokuwa Spika bali kibaraka
 
Sijaona kosa la Ndugai
Kwanza Naona Bado hajaongea
Kwa hiyo Ndugai kupishana na mwenyekiti wake wa chama na amiri jeshi mkuu hadharani unaona sawa eti!..Lini ulimsikia akiinua mdomo wake kumpinga baba Jesca..au na wewe unajitoa ufahamu..kwanza yeye ni mkuu wa muhimili na mjumbe wa halmashauri kuu ya chama chake Kama sijakosea..anauwezo wa kumpigia mama simu moja kwa moja na mama akaongea naye..alishindwa nini kuwasiliana na viongozi wenzanke ndani ya serikali..kabla hajaja hadharani kulalamika Kama akina Mbatia na wenzake wa upinzani....na alienda mbele akasema 2025 tuchague mikopo au..hapa inaonesha aidha ana ajenda yake ya 2025.. na wenzake Sasa wanaanza kutafuta umaarufu kwa wananchi..
Na sisi wananchi tunamwambia hatudanganyiki..Kama ikiwezekana ajiuzulu atafanyaje kazi na muhimili uliojichimbia chini zaidi wakati ameshauchefua...na " Atake asitake Samia ni rais wake 2025-2030
Kazi iendelee
 
Naunga mkono hoja
 
Sema wewe sasa darasa pale shule shikizi linazalishaje pesa ya kulipa deni
Litatengeneza wataalamu ambao, wataleta kodi na pia wataajiri watu Mkuu....hizi ni chache tuu.
 
Spika wa Bunge ni muhimili unaojitegemea sio sehemu ya serikali, ndio maana tunataka Katiba Mpya. Ili muhimili wa Bunge na Mahakama ujitegemee. Kazi ya Bunge ni kuiwajibisha serikali na kutunga Sheria. Job Ndugai yupo sahihi.

Sent from my Infinix X657 using JamiiForums mobile app
 
Nani kasema, yaani auachie ugali wa bure arudi mtaani..subutuuu.
 
Hoja ya ndugai ilikuwa sahihi, hatuwezi kukopakopa bila breki. Ila sasa kwa vile mama yeye anasema atakopa mpaka mwisho ikaonekana ndugai anapingana na mwenye dola. Kimsingi, mama ndiye aliyekosea kusema kuwa sisi tutakuwa taifa na kukopa mpaka tufikie malengo yetu, bila kutambua kuwa mikopo ina gharama zake. Tunajua kuwa serikali itakopa tu, lakini ile kutangaza kuwa mikopo ndiyo tegemo letu, nadhani haikuwa sahihi kabisa; yaani ni kama alitangaza kuwa sera ya serikali ni kukopa hata kama mapato ya serikali yakiongezeka tutakopa tu. Mara zote katika maisha yetu binafsi mikopo huwa ni kwa ajili ya dharura tu pale tunapopungukiwa, siyo kuwa huwa tunaishi kwa kupanga maisha yetu tukitegemea kukopa.

Azimio la Arusha linasema "Kujitawala ni kujitegemea; kujitawala kwa kweli hakuwezekani iwapo taifa linategemea miassada na mikopo kutoka taifa jingine kwa maendelo yake." Mama alisema wazi kuwa kila mradi tunaofanya tutakwenda kukopa, yaani akawa ameshajenga utegemezi.
 
Nchi ina wananchi ambao hawatakiwi kuzungumza lolote ambalo ni kinyume na mtawala wa nchi.

Ni jambo la ajabu na sio haki kabisa.

Kwanini watu hawatakiwi kusema lolote wanatakiwa wakae kimya tu??

hahahahaha
 
Nyie watu sijui mmekula nini, yaani mnawaza utafikiri hamna ubongo, bunge sio rubber stamp ya watawala, kukosoa ni muhimu na ndio inatakiwa iwe hivyo, huyo Ndugai ni culture hiyo hiyo ya CCM ya kinafiki ndio maana kaomba msamaha
 
Naunga mkono hoja
P
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…