Habari yenu ndugu zangu natumaini mnaendelea vizuri
Mwaka 2015 kulikuwa na uchaguzi nchini, japo vyama vingi vilishiriki uchaguzi ule ila mchuano mkali ulikuwa kati ya mgombea wa CCM na mgombea wa muungano wa UKAWA.
Kwa kweli uchaguzi ule ulikuwa mzuri sana (nazungumzia kwa upande wa bara acha Zanzibar) wagombea wote walifanya kampeni zao vizuri, na pia hata kama kulikuwa na vurugu zilikuwa kwa kiwango kidogo kiasi kwamba kama mtu hukukumbana na vurugu katika uchaguzi ule unaweza sema kwa jeuri kuwa amani ilitawala. Wananchi walipiga kura, matokeo yalitangazwa kwenye runinga, mgombea wa CCM alitangazwa mshindi, na picha nzuri ya rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania akiwa amemkumbatia rais mtarajiwa na wote wawili wakiwa wametabasamu iliwekwa kwenye kurasa ya mbele ya gazeti la mwananchi. Kishapo mgombea wa UKAWA alikubali matokeo na rais wa tano wa jamhuri ya muungano wa Tanzania aliapishwa kwa nderemo na vifijo kwenye uwanja wa Uhuru jijini Dar es Salaam.
Nipende kuchukua nafasi hii kumpongeza sana rais wa awamu ya nne kwa maana ni serikali yake ndio ilijenga mazingira ambayo yaliwezesha tukawa na uchaguzi mzuri namna ile. Ushahidi kuwa mambo mazuri yale hayakuja kwa bahati bali yaliwezeshwa na serikali yake upo kwenye hotuba yake yakufungua bunge mwaka 2005. Pia nipende kuchukua nafasi hii kumpongeza mgombea urais wa UKAWA wa mwaka ule 2015 kwa kukubali matokeo na hivyo kuhakikisha amani inaendelea kutawala katika nchi yetu.
Baada ya hapo wote ambao tulikuwa watu wazima kipindi kile tulishuhudia jinsi ambavyo rais mteule wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alivyoanza kutekeleza ahadi zake alizozitoa kipindi cha kampeni. Rais wa JMT ambaye pia alikuja kuchaguliwa kuwa mwenyekiti wa CCM baadae alianza kutekeleza majukumu yake kwa uhodari wa hali ya juu yaani utadhani ndoto lakini ilikuwa kweli kupata rais mzuri namna ile. Moja ya mambo mazuri aliyoyafanya yalikuwa ni
1. Kupambana na ufisadi
2. Kubana matumizi ya fedha za serikali
3. Kurejesha nidhamu ya kazi serikalini
4. Ujenzi barabara muhimu kwenye jiji la Dar es salaam na hivyo kupunguza foleni
4. Kuanzisha Ujenzi wa treni ya umeme.
5. Kuanzisha ujenzi wa bwawa la kufua umeme la Julius Nyerere
6. Kurekebisha mikataba na wawekezaji kwenye sekta ya madini
Hata hivyo kama ilivyo kwa binadamu wengine wote madhaifu hayakosekani, hivyo baadhi ya wapinzani wake wakisiasa katika vyama vya upinzani walifanya kazi ya kupeleleza udhaifu wa rais, wapate cha kuzungumza, utendaji wa rais usije ukawapoteza kabisa kwenye ramani ya siasa, Yafuatayo ni mambo yaliyolalamikiwa
1. Kutoajiri (ajira mpya) serikalini.
2. Kutoongeza mishahara watumishi serikalini
3. Kuongezeka kwa ugumu wa maisha mtaani (vyuma vimekaza)
Na mengineyo
Hata hivyo mema aliyokuwa akifanya rais yalishinda kwa kiasi kikubwa madhaifu yake machoni pa wananchi.
Mbali na shughuli njema alizofanya rais katika kuliletea taifa maendeleo. Kuna maamuzi aliyafanya kwa habari ya siasa. Yafuatayo ni maamuzi aliyafanya
1. Kuzuia kurushwa kwa mikutano ya bunge mubashara kwenye runinga
2. Kuzuia mikutano ya hadhara ya vyama vya siasa isipokuwa kwa majimbo waliyoshinda
3. Kupiga marufuku maandamano ya kisiasa
Wengine katika vyama vya upinzani walipinga sana hatua hizo wakisema ni ukandamizaji wa demokrasia wakafika hatua ya kumuita mheshimiwa rais dikteta uchwara. Hivyo Habari ya demokrasia ikawa ndio kelele kuu ya wapinzani katika kipindi cha serikali ya awamu ya tano.
Hata hivyo kwa macho yangu kelele zilizopigwa na wapinzani, maonyo waliokuwa wakiyatoa, maneno mazuri na ya busara waliokuwa wakiongea mara zote kwa habari ya demokrasia hayakuzingatiwa na watanzania wengi. Wengi walikuwa wamelewa na Pombe aah! samahani namaanisha walikuwa wamelewa na utendaji uliotukuka wa mwana wa Pombe aitwaye Yohane. Wengi walishangilia utendaji wa rais wakipuuza maonyo ya wapinzani, wengine wakiwaita wapinzani kuwa ni vibaraka wa mabeberu
Dalili zote zilikuwa zinaonyesha kuwa mheshimiwa rais na chama chake wangeshinda uchaguzi wa mwaka 2020 kwa kishindo.
Hapa sasa ndio wakaanza kukosea.
Inaonekana CCM hawakujiandaa kuridhika na ushindi katika uchaguzi ule bali walitaka vyama vya upinzani vyenye nguvu ikiwezekana vife kabisa. Matokeo yake uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2019 ulikuwa wa ajabu sana. Kwa kweli wapinzani walichezewa rafu mbaya sana. Vivyo hivyo uchaguzi mkuu wa mwaka 2020 ulikuwa na uonevu kwa wagombea wa upinzani. Hakukuwa na uhuru na amani kama ule wa 2015. Baada ya kampeni baadhi ya wagombea wa upinzani walikimbia nchi kuhofia usalama wao. Kwa kweli hayo matata ya uchaguzi wa mwaka 2019 na 2020 ndio yalijenga msingi wa machafuko ya mwaka 2025. Kwa maana CCM waliona kama tuliweza kipindi kile tufanye tena na saa hii. Kinachosikitisha ni kuwa hakukuwa na ulazima wa kufanya yote hayo. Maana dalili zote zilikuwa zinaonyesha kuwa wangeshinda.
Mwaka 2021 rais wa jamhuri ya muungano wa Tanzania alifariki na makamu wa rais akaapishwa kwa mujibu wa sheria. Kwa kweli ilikuwa ni kipindi cha majonzi sana kwa watanzania kuona jembe lao limeondoka na halitarudi tena.
Rais mpya wa Tanzania alijaliwa hekima akaona marumbano na wapinzani hayana maana tufanye kuridhiana. Wapinzani waliokimbia nchi walirudi, wakakaa na rais kwa mazungumzo, kwa kweli yalikuwa ni maamuzi yaliyokuwa yakitia matumaini sana. Rais mpya akafanya bidii kuimalizia miradi iliyoachwa na mtangulizi wake. Wapinzani wakaruhusiwa kufanya siasa, wakazunguka huku na huku kwa furaha na wafuasi wao wakiwasilisha sera zao na kuonyesha udhaifu wa serikali.
Lakini mwaka 2024 mambo yakabadilika kwanza mkutano wa Chadema Mbeya ulivurugwa na baada ya hapo mmoja wa viongozi wa Chadema akauawa na watu wasiojulikana akiwa kwenye basi. Mmmh wasiwasi ukaanza tena, ina maana tunarudi kulekule. Yote tisa jambo lililoumiza sana lilikuwa ni uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024 ambao haukuwa na tofauti yoyote na ule wa mwaka 2019. Kama kawaida wagombea wa upinzani wengi walienguliwa na CCM ilijipatia mitaa yote. Kwa kweli kwa viongozi wa upinzani nchini jambo hilo lilikuwa ni la kuumiza na kukatisha tamaa sana. Kinachosikitisha tena ni kuwa CCM ilikuwa haina haja ya kufanya dhuluma yote hiyo maana hata kama uchaguzi ungekuwa fea bado wangepata mitaa mingi kuliko wapinzani.
Baada ya vyama vya upinzani kuona rafu walizochezewa kwenye uchaguzi wa serikali za mitaa wa mwaka 2024 hapo ndipo walipoamua kutoshiriki uchaguzi mkuu wa mwaka 2025 na badala yake kudai mageuzi kwenye mfumo wa uchaguzi wakija na kauli mbiu "No reforms no elections".
Tusinge fika hapo pengine kama CCM isingekuwa katili namna ile kuengua wagombea vile kujipatia mitaa yote wenyewe. Kauli mbiu ya "no reform no elections" bila shaka kama ilivyosema tume ya uchunguzi ya jaji Chande ni moja ya sababu kubwa ya vurugu za uchaguzi mkuu wa mwaka 2025.
Tofauti na mwaka 2015 katika mwaka wa 2025 wala hakukuwa na uchaguzi bali kulikuwa na vurugu na mauaji, watanzania wengi walipoteza maisha wengi waliuawa kwa risasi. Kama niliipongeza serikali ya awamu ya nne kwa kufanikisha uchaguzi mzuri wa mwaka 2015 sasa sijui nimlaumu nani kwa uchaguzi ule mbovu wa 2025.
Ndugu zangu lawama hazijengi lakini bila shaka uonevu uliotokea katika chaguzi za mwaka 2019, 2020 na 2024 ni sababu kubwa ya vurugu za uchaguzi mkuu wa mwaka 2025. Kinachosikitisha zaidi ni kuwa CCM kwa mambo mazuri waliyoyafanya kwa kipindi cha miaka kumi iliyopita wala hakukuwa na haja ya ubabe wote huo wangeshinda tu. Sasa CCM wamejiweka kwenye wakati mgumu wenyewe
Maana hivi sasa watanzania wengi wana uchungu na mauaji yaliyotokea. Na wengi wanaichukia serikali kwasababu hiyo. Matumizi ya nguvu kupita kiasi dhidi ya ndugu zao yamewagharimu
Katika mazingira ya sasa si ajabu kuamini kuwa upinzani unaweza chukua nchi.
Je upinzani utachukua nchi mwaka 2030?