Maoni: Elimu ya Tanzania imeshuka

Maoni: Elimu ya Tanzania imeshuka

Kibishi

JF-Expert Member
Joined
Nov 17, 2013
Posts
1,139
Reaction score
1,031
Habari zenu!

Serikali inaridhisha wananchi kupandisha elimu na ufaulu kupitia Big Results Now kwa GPA mpya.GPA hiyo na GRADES zake zinampendelea mtahiniwa ili mradi afaulu tu, tena kwa kiwango rahisi. GPA mpya haifui dafu kwa GPA ya zamani. GPA mpya ina nafasi kubwa ya kumfaulisha mtahiniwa, pia ina nafasi ndogo ya kufelisha, hatari!

Angalia nafasi zenyewe;

DISTINCTION: 3.6 - 5.0,nafasi 15
MERIT: 2.6 - 3.5,nafasi 10
CREDIT: 1.6 - 2.5,nafasi 10
PASS: 0.3 - 1.5,nafasi 13
FAIL: 0.0 - 0.2,nafasi 3.

Wakati GPA ya zamani;

DIV I,7-17, nafasi 11
DIV II,18-21, nafasi 4
DIV III,22-25, nafasi 4
DIV IV,26-33, nafasi 8
FAILED,34-35, nafasi 2

Tukija kwenye grade, Grade mpya;

A: 75-100
B+: 60-74
B: 50-59
C: 40-49
D: 30-39
E: 20-29
F: 0-19

Grade za zamani;

A: 81-100
B: 61-80
C: 41-60
D: 21-40
F: 0-20

Ukilinganisha grade mpya na za zamani unapata picha gani?

Elimu imeshuka, ni mpango mradi wa serikali ili watu waje wengi kwenye elimu. GPA ya zamani ilikuwa ngumu kwa PC kupata DIV II, kwa GPA mpya ni rahisi sana kupata DIV II(MERIT), angalia matokeo ya kituo chochote ujionee. Serikali haijafanya chochote kuhusu GPA mpya,zaidi tu,imeshusha elimu.

Haya sasa, wanaotaka kufaulu kiubwete wakati ndiyo huu.
 
Ktk taifa lolote ukishachezea elimu tayari umeua injini ya kukuza uchumi. Acha twende kwa mfumo wautakao ila kusema ukweli elimu ya Tz ndo basi tena.
 
Ktk taifa lolote ukishachezea elimu tayari umeua injini ya kukuza uchumi. Acha twende kwa mfumo wautakao ila kusema ukweli elimu ya Tz ndo basi tena.

Kweli kabisa Ndg. Kisangiro.
Uchumi haukuzwi kwa kuichezea elimu,uchumi unakufa kwa kuichezea elimu.
 
Awamu nyingine nayo itakuja na ya kwake.Pengine watarudisha grade za zamani.
 
Tunajenga taifa la wajinga na matokeo yake tutayaona punde. Bahati mbaya sana hatuna mkakati endelevu wa elimu baada ya kuanza kuchakachua katika awamu ya pili na kuruhusu kila mjanja kuchapisha kitabu chake. Tumetoka kwenye vitabu, na kuidunisha taaluma ya ualimu na sasa tuko kwenye awamu ya kudidimiza wanafunzi na kuwapumbaza kana kwamba tunaishi kwenye kisiwa chetu wenyewe.
 
Back
Top Bottom