Maoni: Haya ndiyo makundi/makabila yenye maendeleo Tanzania

Pia wakinga ukija kwenye biashara hawataki watu wengine waendelee. Alafu ni washirikana hatari na waongo sana
 
Jwa awamu hii ya sita tunakubaliana na wewe
Ni tangu zamani mkuu, wana asilimia kadhaa kwenye muungano, hawa sio wenzako

 
Ukabila hauna faida labda kutambika-JK Nyerere.
 
Ukabila hauna faida labda kutambika-JK Nyerere.

Mods futeni huu uzi, haya mambo ya ukabila sio mazuri hata kama ni kweli, inabidi yaachee yalivyo.
Mkuu, ukabila uko wapi hapa?? hizi ni tathmini na sio ukabila.

Tukisema kundi kubwa la wasomi wanatokea bukoba kiasi kwamba ilibidi wapandishiwe wastani hapo zamani, ukabila uko wapi??

Tukisema wanajeshi wengi wanatoka mkoa wa mara kiasi kwamba kwenye vita ya uganda walijaza mno nafasi mpaka kuombea kujiunga jeshini kwa kwenda mikoa mingine, ukabila uko wapi??

Tukisema wanaijeria ndio kundi linaloongozea kwa kuwa na wasomi wengi marekani inafika hatua mpaka kuwa na degree karibu kila mnaijeria anaeishi marekani anayo, hapo ukabila uko wapi??

Tukisema kabila lako wanajua sana kucheza ngoma kwasababu tunajiomea kwa macho yetu na kuvitiwa kwa jinsi mnavyocheza ngoma, ukabila upo wapi?

Katafute maana ya ukabila, maana unayoijua wewe sio maana halisi
 
Utakuwa una asili ya kiarabu wewe.
Nia yako ni kutuaminisha sura ya 2.mengine yote ni Zuga toto.
 
Na

Nakubaliana na wewe japo wachaga wa siku hizi ile spirt ya kupambana sio kama wale wa zamani
Zamani wachaga na wahaya walikuwa ni kundi kubwa sana lenye watu walioelimika, hii iliwapa fursa ya kuajirika sana kuzidi makabila mengine.

Kwa siku hizi shule zimekuwa nyingi sana, kile kipindi cha golden era interview ina 90% wachaga na wahaya kinapotea, kwa siku hizi elimu imesambaa sana, karibu kila pande ya nchi,

Nakumbuka mzee Mengi (R.I.P) ndie alikuwa cpa wa kwanza hapa Tanzania, enzi hizo ilikuwa jambo kubwa sana, Pia kulikuwa na shule nyingi sana moshi, hii ilipanua wigo wa wachaga wengi kupata sifa za kujaa kwenye system maana ni wao pekee ndio walikuwa na sifa za juu kwenye elimu.

Kwa siku hizo hata ukienda huko Tarime shule zipo na ufaulu umeongezeka sana, hii kitu ime neutralize dominance ya wachaga na wahaya.

Na hapo kidogo wachaga wamejikita kwenye biashara kwahio haiwaumizi sana, wahaya ndio inawaumiza maana wao mlango wao wa mafanikio ume base sana kwenye elimu na kwa sasa elimu imesambaa sana nchini hadi vijijini, interview unawakuta watu wa makabila ya aina yote.
 
Bogus .... Waluguru inakuwaje Hawapo.
 
Kujadili na kuyapima makabila hakuna tija yeyote.
kuna tija km una wivu wa maendeleo na ukaiga kile wanachofanya. Si dhambi. Yako mengi mazuri wanafanya mfano kushirikiana na kuwezeshana kiuchumi.

Ila simaanishi kwamba nakubaliana na hoja moja KWA moja kwamba hao ndiyo wako vizuri.
 
Sisi wakaguru unatuweka kundi gani?

Kumbuka utajiri si kabila; ni wewe mwenyewe. Kama huna pesa hata ungekua mchina ni kazi bure
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…