SoC04 Maoni juu ya kurekebisha miundombinu ya kiafya (vyoo na takataka)katika mosoko ya jumla Dar-es Salaam, hasa Soko Kuu la Ilala

SoC04 Maoni juu ya kurekebisha miundombinu ya kiafya (vyoo na takataka)katika mosoko ya jumla Dar-es Salaam, hasa Soko Kuu la Ilala

Tanzania Tuitakayo competition threads

piusluckness

New Member
Joined
May 31, 2024
Posts
4
Reaction score
1
Tanzania, kama nchi ambayo ukuaji wake wa kiuchumi unategemea sekta mbalimbali basi Masoko ya jumla yana nafasi kubwa na chanya katika pato la Taifa, kwani ukusanyaji wa mapato huwa ni kwa kiasi kikubwa katika masoko kulingana na shughuli mbalimbali zinazofanyika.

Pamoja na faida kubwa ambazo zinapatikana kutoka kwenye masoko haya(yaani upatikanaji wa pato kubwa) wajasiriamali na wafanyabiashara katika masoko haya wamekua wakipitia changamoto mbalimbali hasa za kiafya,ambazo kwa namna kubwa zimekua zikirudisha maendeleo katika masoko ya jumla.

Zifuatazo ni changamoto kuu mbili ambazo zinazowakumba wafanya biashara katika masoko ya jumla jijini Dar es salaam,na Hasa katika soko kuu la bidhaa za jumla na rejareja la Ilala.

1.MIUNDOMBINU MIBOVU YA HUDUMA YA VYOO VYA UMMA KATIKA SOKO LA ILALA,DAR ES SALAAM.
Hii ni moja ya changamoto na kero kubwa katika soko la ilala,ikiwa Kuna uwepo wa huduma hii katika maeneo yasiyopungua manne(4) tofauti ndani ya soko la ilala. Na hii inageuka kero baada ya uongozi kushindwa kusimamia mifumo hii na kupelekea wamiliki kuachia chemba za maji taka yanayomwagika katika sehem za biashara katika mitaa mbalimbali ya soko la ilala. Mfano chemba iliopo mtaa wa moshi (maarufu mtaa wa Ndimu na malimao),lakini pia mtaa wa tabora. Athari hii inapelekea.

a)baadhi ya wateja kutofanya manunuzi katika mitaa baadhi katika soko la ilala kutokana na uchafu huo kutoka vyooni.

b) uhatarishi wa afya hasa za wafanyabiashara ambao wanakaa hapo kwa muda mrefu,wanunuzi, na kwa kiasi kikubwa watumiaji wa bidhaa hizo katika maeneo mbalimbali hasa mahotelini na migahawani.

Maoni juu suluhu inayoweza kufanyika kupunguza changamoto hii katika masoko.

i)wadau husika ndani ya masoko kwa kushirikiana na uongozi wa serikali kwa kupitia halmashauri,wanatakiwa kuhakikisha uwepo wa mifumo salama ya vyoo na majitaka,kwa kujenga vyoo vya kisasa ili kupunguza hali hatarishi kwa wafanya biashara na wanufaika wengine.

ii) kupunguza uwepo wa vyoo vingi vya umma ili kurahisisha usamimizi mzuri wa huduma hizi na kupunguza uwepo wa athari mbalimbali.

iii)katika mpango mpya wa ujenzi wa masoko bora, serikali ihakikishe inapata maoni kutoka kwa wafanyabiashara ili kuepusha urudiaji wa makosa ya kimiundombinu katika miradi mipya inayotekelezwa.

20240620_115241.jpg

Picha na.1.
Hii ni picha inayoonesha hali halisi katika soko la ilala..ikiwa hayo ni maji yanayotoka kwenye chemba katika mtaa wa Tabora.

2.UCHELEWESHWAJI WA UKUSANYAJI WA TAKATAKA KATIKA SOKO LA ILALA
.
Kulingana na shughuli mbalimbali zinazofanyika katika masoko ya jumla,zoezi la ukusanyaji wa taka linapaswa kuwa ni kipaumbele. Pamoja na jitihada zinazoonekana kuchukuliwa lakini bado hili limekua ni kero kutokana na Takataka kukaa kwa muda mrefu baada ya kukusanywa, hasa katika mtaa wa nzasa. Ambapo kwa wakati mwingine huoza na kutoa harufu mbaya, na kugeuka kero kubwa baada ya mvua kunyesha kwani kwa muda huzuia barabara inayopaswa watu kupita. Na hali hii si nzuri kwani ni chanzo kikubwa cha magonjwa ya mlipuko yanayoweza kutokea kama kipindupindu

Na ili kuweza kurekekebisha changamoto hii uongozi wa soko la ilala kwa kushirikiana na halmashauri, wanapaswa wahakikishe usafi wa kiwango cha juu kwa kuhakikisha ukusanyaji wa taka unafanyika kila siku. Ili kuondoa dhana ya wananchi kwa kuona serikali inajali mapato kuliko afya na maendeleo ya wananchi.

3. KUTOPITIKA KWA BAADHI YA MAENEO HASA WAKATI WA MVUA.
Hii husababishwa na uwepo wa matope baada ya mvua kunyesha na kupelekea baadhi ya mitaa kutopitika. na changamoto hii hupelekea wafanyabiashara kukosa wateja kwani wanunuzi wengi huofia hali hio.

Changamoto hii inaweza kuchukua mda mrefu kukebishika kulingana na taratibu za kibajeti za nchi. Japo viongozi wanaweza kutumia njia mbadala kana kumwaga Kokoto na vipande vya mawe ili kupunguza adha hiyo wakati wa mvua. Na gharama hii inaweza chukuliwa katika mapato ya wafanyabiashara.

20240620_115349.jpg

Picha na. 2.
Hii ni picha inayoonesha hali halisi ya tope katika kipindi cha mvua,katika soko la ilala.

Mapendekezo ya ziada.
i)Ni muhimu serikali kutatua changamoto hizi ili kuhakikisha wananchi wafanyabiashara wanakua katika mazingira salama na watumiaji pia.

ii) usafi wa mazingira katika maeneo ya masoko ni swala linalotakiwa kuwa kipaumbele kwani ndiko asilimia kubwa ya pato linapokusanywa kila siku katika jiji la dar es salaam.

Tuijenge Tanzania pamoja 🇹🇿.
 
Upvote 4
Back
Top Bottom