Maoni kuhusu Law School, Mzengwe au ajali?

brazaj

JF-Expert Member
Joined
Jul 26, 2016
Posts
31,698
Reaction score
41,733
Kumekuwa na jitihada za kuona hali ya shule ya sheria (LST) inaanikwa kwa uhuru.

Hata hivyo jitihada mbalimbali zimekuwa zikiyeyuka "miraculously" bila sababu halisi kuwekwa hadharani.

"Hii nchi ni ngumu sana" - alisikika ndugu mmoja akiugulia maumivu moyoni.

Hili ni la kamati ya majaji:

IMG_20221024_081910_500.jpg

Hili ni la Kongamano la kukusanya maoni juu ya Mwenendo wa Ufaulu wa wanafunzi wa Shule ya Sheria nchini Tanzania nalo:

IMG_20221024_074306_021.jpg

Kwenye sintofahamu yote iliyoelezewa kuhusu LST kulikoni wadau hawa kuyeyuka mithili ya barafu kwenye moto?

Zingatia: post #2 ilikuwa wito kwa ajili ya kongamano Hilo la kukusanya maoni.
 
Kongamano la kukusanya maoni juu ya Mwenendo wa Ufaulu wa wanafunzi wa Shule ya Sheria nchini Tanzania nalo:

"Salamu kutoka Chama cha Wanasheria Tanganyika (TLS)
TLS pamoja na Wakili TV inapenda kukualika rasmi katika Kongamano la kukusanya Maoni Juu ya Mwenendo wa Ufaulu wa Wanafunzi wa Shule ya Sheria Nchini Tanzania. Litakalofanyika tarehe 22/10/2022 katika ukumbi wa Wakili House; TLS Makao makuu kuanzia Saa 3:30 Asubuhi mpaka saa 8: 00 Mchana.

Baadhi ya wadau wanaotarajia kushiriki kongamano hili ni
1. Mawakili
2. Baraza la Elimu ya Sheria nchini
3. Wizara ya Katiba na Sheria
4. Umoja wa Mawakili Vijana (AYL)
5. Wahadhiri Shule ya Sheria (LST)
6. Wahadhiri Vyuo Vikuu Vitivo vya Sheria
7. Wanafunzi wa Sheria
8. Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA)
9. Wanahabari
10. Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC)
11. Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC)
12. Na wadau mbalimbali

Kwa mawasiliano zaidi Salima Mseta, 0778626022"
 
Huu ndio mfano unaoonesha dhahiri hata mambo huko Law School huendeshwa kisiasa, kwa hali hii ndipo malalamiko ya kufaulu kwa kujuana, rushwa, yanazidi kupata nafasi.

Hili nilianza kulitilia shaka baada ya waziri Dr. Ndumbaro kuunda kamati huku tayari akiwa na majibu ya kile kilichomfanya aunde kamati, kama waziri aliamini ufaulu wa LST unaridhisha, basi pasingekuwepo na lolote la maana.

Lakini kiuhalisia ni ujinga tu kuamini kwamba pale LST wanaofaulu ni wale wenye ufaulu mzuri, ikiwa siasa za CCM zinapewa nafasi mpaka huko, kuficha uozo.

Kuogopa watu kutoa maoni yao ni uoga wa ajabu kabisa, ikiwa wangeweza kuyapokea hayo maoni na wasiyafanyie kazi kama kawaida yao.
 
Kama nia ilikuwa njema ya kupata maoni kwa uboreshaji sahihi hakuwa na composition bora kuliko Ile ya lile kongamano la TLS kwa maana Hilo hata waalimu LST walikuwa waalikwa kwenye forum 1.

Kama nia ilikuwa njema huo kwa Mwakyembe ndiyo ulikuwa mgodi sasa. Kwamba ghafla umeyeyuka na bila Maelezo? Ngoja tuone.

Inaonekana nia inawezakuwa ni kufunika funika mambo. Ili kina sisi uswahilini tuendelee kusikiliza tantarira za kina Stroke na warusi uchwara wa Buza kuwa sheria ni kama udaktari yashughulika na maisha na vifo vya watu. Eti kuwa kufeli watu ndiyo kielelezo cha kuwa Kuna seriousness kwenye utahini.

Anasema beberu "Bull shit."
 
Ukienda LST sasa hivi ukahoji jambo, mfano, kujua kama wamekubali kurejesha booklets kwa wanafunzi wanaohitaji kuziona, wanakujibu, umekuja kutujaribu sio, hatukupi na nenda kalalamike kokote unakotaka.
 
Kwa majibu haya wanaonesha vile wanastahili kutiliwa shaka kwenye utendaji wao.
 
Huu ndio mfano unaoonesha dhahiri hata mambo huko Law School huendeshwa kisiasa, kwa hali hii ndipo malalamiko ya kufaulu kwa kujuana, rushwa, yanazidi kupata nafasi.

Hili nilianza kulitilia shaka baada ya waziri Dr. Ndumbaro kuunda kamati huku tayari akiwa na majibu ya kile kilichomfanya aunde kamati, kama waziri aliamini ufaulu wa LST unaridhisha, basi pasingekuwepo na lolote la maana.

Lakini kiuhalisia ni ujinga tu kuamini kwamba pale LST wanaofaulu ni wale wenye ufaulu mzuri, ikiwa siasa za CCM zinapewa nafasi mpaka huko, kuficha uozo.

Kuogopa watu kutoa maoni yao ni uoga wa ajabu kabisa, ikiwa wangeweza kuyapokea hayo maoni na wasiyafanyie kazi kama kawaida yao.
Vijana someni, someni acheni kwenda vyuoni na kuuza sura.
 
Vijana wa siku hizi hawataki taabu wanataka mtelezo ili wapate ajira fasta. ndio maana leo hii hakuna tija maana wengi wao ni mbumbumbuuu
 
Mkuu hapa kulikuwa na mchanganuo wa waliotegemewa kujadili suala hili kwa mapana na marefu:

Baadhi ya wadau wanaotarajia kushiriki kongamano hili ni
1. Mawakili
2. Baraza la Elimu ya Sheria nchini
3. Wizara ya Katiba na Sheria
4. Umoja wa Mawakili Vijana (AYL)
5. Wahadhiri Shule ya Sheria (LST)
6. Wahadhiri Vyuo Vikuu Vitivo vya Sheria
7. Wanafunzi wa Sheria
8. Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA)
9. Wanahabari
10. Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC)
11. Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC)
12. Na wadau mbalimbali

Unadhani #12 pale chawa nao walijumuishwa?
 
Vijana wa siku hizi hawataki taabu wanataka mtelezo ili wapate ajira fasta. ndio maana leo hii hakuna tija maana wengi wao ni mbumbumbuuu

Hapa chini pana wadau wakiwamo majaji wanaotambua Kuna mambo hayako sawa LST. Ila kinyangarika wewe na wala hujishangai:

--------
Baadhi ya wadau wanaotarajia kushiriki kongamano hili ni
1. Mawakili
2. Baraza la Elimu ya Sheria nchini
3. Wizara ya Katiba na Sheria
4. Umoja wa Mawakili Vijana (AYL)
5. Wahadhiri Shule ya Sheria (LST)
6. Wahadhiri Vyuo Vikuu Vitivo vya Sheria
7. Wanafunzi wa Sheria
8. Chama cha Wanasheria Wanawake (TAWLA)
9. Wanahabari
10. Kituo cha Haki za Binadamu (LHRC)
11. Mtandao wa Watetezi wa Haki za Binadamu (THRDC)
12. Na wadau mbalimbali
----------

Unaonesha una makasiriko sana na hali yako kimaisha.

Mafanikio au kukwama kwa wengine hakuhusiani na wala hakutapunguza machungu yako ya maisha ndugu.
 
Kwa majibu haya wanaonesha vile wanastahili kutiliwa shaka kwenye utendaji wao.

Ni ajabu kuwa composition hii awaye yote anayetaka ukweli anaweza kutaka isisikike:

IMG_20221025_071710_816.jpg

Kwani anataka kumficha nani nini?

Hapa ndipo ulipo umuhimu wa option zero kwenye mapambano.
 
Ukienda LST sasa hivi ukahoji jambo, mfano, kujua kama wamekubali kurejesha booklets kwa wanafunzi wanaohitaji kuziona, wanakujibu, umekuja kutujaribu sio, hatukupi na nenda kalalamike kokote unakotaka.

Kwamba mtu hataki maoni ya watu hawa:

IMG_20221025_071710_816.jpg

Ila ya akina zandrano, Ikoko au Stroke? Wala hajishangai.

Tuna jamii ya ajabu sana. Haipo shaka ndiyo maana tupo hapa tulipo.

Bure kabisa.
 
Back
Top Bottom