Midimay
JF-Expert Member
- Apr 12, 2015
- 3,036
- 5,039
Habari za jioni mabibi na mabwana.
Ni maoni kwamba nia hii njema ya RJMT ipate muda wa kutosha katika mitandao ya kijamii na media kuu za nchi yetu.
Ikiwezekana hata na media za kimataifa kama BBC Swahili, BBC Focus on Africa, VOA Swahili, DW Kiswahili na za kikanda kama media za nchi jirani ya Kenya.
Mimi nina maoni yafuatayo kwa Tume hii, naaminini itawafikia.
1. Wakuu wa vyombo vyote vya utoaji wa haki jinai wawe na security of tenure kama ilivyo kwa CAG na Jaji Mkuu.
Kanuni hii itapunguza influence ya Wanasiasa wakuu katika utendaji wa kila siku wa vyombo hivi.
2. Bajeti na upatikanaji wa fedha kwa ajili ya uendeshaji utajwe na sheria au kuwe na mfuko maalum kwa kila chombo. Iwe kama au bora kuliko ilivyo mfuko wa mahakama. Lengo ni lile lile la kuiongezea chombo cha haki kujiamini dhidi ya maamuzi ya wanasiasa.
3. Wakuu wa vyombo hivi wapatikane kwa mchakato wa wazi na kiushindani utakaobuniwa na sheria na sio kwa bin vuu uteuzi wa RJMT.
4. Maslahi ya wakuu wa vyombo hivi yatajwe na sheria itakayotungwa na Bunge la JMT. Iwe kama ambavyo maslahi ya wakuu wa kisiasa yametajwa na hata ya kustaafu kama ilivyo kwa "Political Service Retirement Benefits Act".
5. Mfumo wa ajira katika jeshi la polisi ubadilishwe. Sifa za kujiunga na jeshi ziimarishwe ili wapatikane watu wenye sifa.
6. Mtaala wa mafunzo katika jeshi la polisi uboreshwe ili wasome kwa muda mrefu kidogo mambo ya sheria, elimu ya uraia,utafiti, haki za binadamu, sociology, maswala ya maendeleo ya jamii, ustawi wa jamii na mengine yatakayofanana kuliko sasa ambapo ni kama wanafundishwa kupambana na uhalifu tu bila kujua yanayoambatana na uhalifu.
7. Tuanzishe chuo maalum(institute) kwa ajili ya mafunzo juu ya haki jinai nchini. Iwe ni Post Graduate Institution. Tuna chuo cha kodi, chuo cha Benki Kuu, cha Ulinzi na zingine kama hizo.
8. Sheria za Criminal Procedure Act(CPA), Penal Code, Prevention and Combating of Corruption Act, Prisons Act ziboreshwe.
Karibuni kwa maoni na mapendekezo mengine.