Raphael focus
JF-Expert Member
- Nov 4, 2018
- 789
- 4,640
Habari ya muda huu wana janvi!
Kama mada inavyo jieleza hapo juu:
Kwa upande wangu naweza kulielezea swala la Elimu bure kwa Shule za Sekondari kama utashi wa mtu binafsi na propaganda ilioanzishwa ili kumuwezesha mtu huyo kulifikia lengo lake pasipo kutambuwa athali za jambo hilo.
Ninaweza kuzielezea athali mbalimbali zilizotokana na sela ya Elimu bure kama ifuatavyo;
Changamoto ya upungufu wa vyumba vya madarasa:
Ndugu wana JF sote tumeshuhudia au kusikia maelufu ya wanafunzi kuchelewa au kutoripoti kidato cha kwanza kutokana na sababu za upungufu wa vyumba vya madarasa.
fig: mulundikano wa wanafunzi katika chumba kidogo cha darasa.
Changamoto ya upungufu wa madawati:
Kutokana na kuanzishwa kwa sela hii ya Elimu bure, imepelekea upungufu mkubwa wa madawati mashuleni kwani shule zimeshindwa kujiendesha zenyewe ikiwa ni pamoja na kushinwa kutengeneza na kukalabati madawati, hivyo kupelekea baadhi ya wanafunzi kusoma kwa shida wawapo darasani.
fig: upungufu wa madawati kwa wanafunzi.
Mkwamo wa Shule katika ukalabati wa thamani na miundombinu ya Shule:
Sela ya Elimu bure imepelekea Shule kushindwa kujiendesha zenyewe ikiwa ni pamoja kushindwa kujenga au kukalabati majengo ya Shule, madawati na hata pia miundombinu ya maji na umeme.
fig: Ubovu wa madarasa.
Ombwe la ajira kwa wahitimu wa fani ya ualimu:
Ninakumbuka nilipokuwa O-Level, form One na form Two masomo ya Civics,Geography, Mathematics, Physics, Chemistry na Biology nimefundishwa na walimu waliokuwa wameajiriwa na shule(waitimu wa form Six).
Ninakumbuka somo la Physics nimefundishwa na walimu tofauti waliokuwa wameajiriwa na shule(form six)
kwanzia form One mpaka form Four.
masomo ya Chemistry na Mathematics term ya kwanza form three nilifundishwa na walimu waliokuwa wameajiriwa na shule (form six).
Nilipofika form five masomo ya Biology, BAM na Chemistry nimefundishwa na walimu walioajiriwa na shule.
Hebu fikiria kama shule iliweza kumuajiri Mwalimu wa muda kumufundisha mwanafunzi. Leo hii Shule haiwezi tena kumuajiri Mwalimu lakini pia na serikali imeshindwa kuajiri walimu.
Serikali kupoteza mapato:
Wakati nasoma O-Level nililipa ada ya shule Tsh 20,000/= kwa mwaka.
Sidhani kama shilingi elfu20 inamushinda mzazi kuilipa kwa mwaka wakati uwo mkulima anamulipia mtoto ada form five Shilingi elfu 70 kwa mwaka.
Hivyo ndugu zangu watanzania tuache unyonge wa kijinga nakujiona kama vile hatuwezi kumulipia mtoto ada ya Shule Shilingi elfu 20.
Pendekezo langu kwa serikali sela ya Elimu bule ipitiwe upya.
.....🖊Raphael Phockus.