Maoni na maswali yangu kwa TCRA

Maoni na maswali yangu kwa TCRA

Full charge

JF-Expert Member
Joined
Mar 1, 2018
Posts
1,678
Reaction score
1,617
Poleni na majukumu ndugu zangu wana jamvi.

(a)Kwanini kusiwe na namba ya huduma ya TCRA?
[emoji117] Yaani mteja wa mtandao husika anaponunua kifurushi kikaisha kabla ya muda wake apige simu TCRA ili wahoji au kuchunguza uhalali wa matumizi. Hapa ikibainika mtandao umefanya wizi umrudishie mteja haki yake ikibidi na faini juu hii itasaidia kupunguza wizi tunaoibiwa kila siku na mitandao ya simu.

(2)Kuwe na option ya kukataa matangazo kwenye line ya simu.
[emoji117] Kuwe na mkataba wa kujaza pindi mteja anaposajili line yake. Matangazo mengine yamekuwa kero kwa watumiaji, taasisi iweke utaratibu wa kukubali au kukataa baadhi ya matangazo. Mfano, dini ya mtumiaji x inakataza michezo ya kamali, pombe, kondom nk. Ila analetewa.

(3)Mteja awe ndiye mwamuzi wa matumizi ya pesa yake.
[emoji117]Hapa namaanisha ukinunua kifurushi kisiishe kabla ya wewe kukimaliza.Siyo mtandao umpangie muda wa matumizi,je kama na nunua leo kwakuwa nimepewa ofa ila nataka kuongea mwaka kesho? Hiyo ni haki yangu mtumiaji maana hata ukinunua chumvi dukani mtu hawezi kukulazimisha uunge iishe ukanunue nyingine.

(4)Mteja ashirikishwe na aridhie juu ya mabadiliko ya huduma 'vifurushi'. [emoji117]mabadiliko yasifanyike kwa siri bila mteja kujua.Hiyo ni hujuma nyingine TCRA ilione hilo.

(5)Mtandao ubainishe wazi pesa iliyopotelea kwenye line baada ya kugawiwa mtumiaji mwingine. [emoji117]Mteja anaweza kusafiri nje ya nchi au kuugua zaidi ya miezi 9 au zaidi ikapelekea yeye kuwa nje ya huduma kwa muda mrefu lakini akaunti yake ya mtandaoni kuna pesa.Hivo basi TCRA iweke wazi utaratibu wa mtumiaji kutambua ngazi za wapi aanzie kudai pesa zake na alipwe.

(6)Anaetuma pesa akikatwa basi anaepokea asikatwe.
[emoji117]Kwanini pesa ikatwe pande zote mbili? Haiwezekani mtumaji atume 10000 mpokeaji apate 5000!!

NB:Kuna mambo mengi yanatakiwa yafanywe na TCRA ikiwemo kusimamia mikataba baina ya wasanii na ma meneja wao.
*Hapa namaanisha kwamba mkataba utakao sainiwa nje ya utaratibu wa kupitia TCRA uwe ni batili kisheria, hiyo itasaidia kupandisha uchumi wa wasanii na taifa kwa ujumla. Siyo kufungia nyimbo za Roma kisa kaikosoa selikari afu wakati huo huo video ya Gwajima anaonekana siyo yeye Ila Amberuty na mwenzake wao zinaonekana.Asante
 
Tigo Pesa isharudi? Yaani Bongo unaweza kua na hela yako kwenye simu ila wenye maamuzi nayo wengine kabisa.
 
Back
Top Bottom