Maoni: TANESCO isimamiwe na jeshi

Maoni: TANESCO isimamiwe na jeshi

MSD alipewa mwanajeshi enzi za Mwamba, nini kilibadilika? Si bado madawa ya mabilioni yaliendelea kuozea maboharini wakati hospitali zetu hazina dawa? Tatizo ni mfumo wenyewe na ufumbuzi wake ni lazima uwe wa kimfumo pia. Kwa hali ilivyo hata umpe nani mtu mmoja peke yake hatafua dafu!

Kama unataka kujua umuhimu wa kubadili mfumo; na siyo nguvu za mtu mmoja tu nenda ukamuulize Magufuli. As an individual huwezi kushindana na mfumo ukaibuka kidedea! Ama mfumo utakutema; na ukishupaza shingo sana unaweza kupelekwa Pagak kabla ya siku zako!

Na pa kuanzia tu:

➡️ Unafikiri tatizo HASA la TANESCO ni nini? Na suluhisho lake ni lipi?

➡️ Kuna shirika au taasisi yo yote hapa nchini ambayo unaweza kusema kwamba inaendeshwa kwa ufanisi mpaka kukidhi mahitaji na matarajio ya wanajamii? Kama ipo, tunaweza kujifunza nini kwayo? Kama hakuna unafikiri ni kwa nini? Tufanyeje?
 
Habari za leo
Kutokana na hujuma zinazoendelea katika Shirika la Ugavi na Usambazaji wa Umeme Tanzania (TANESCO) kwa maoni yangu binafsi nashauri Shirika hili Mkurugenzi Mkuu apewe Mwanajeshi na liwe chini ya usimamizi jeshi.

Sababu kubwa ni uwepo wa nidham ya hali ya juu Jeshini hivyo wataweza kuwajibika na kuzuia michezo inaofanywa na Watendaji wanaohujumu uchumi wa Nchi kwa maslahi ya wachache.

Mfano ni hujuma za kuzuia maji yasijae katika mabwawa mbali mbali licha ya uwepo wa mvua nchini hoja hizi zimetolewa na baadhi ya Wabunge lakini kuna namna zinapotezewa
Sahihi 100%
 
Wafanyakazi wa tanesco wapumzishwe alafu jeshi liwe na kitengo cha umeme wa Taifa.Kuwe na kamandi moja ya umeme ikiwa na wataalamu waliosemeshwa na serikali hapo kama tupo siriazi basi tatizo la umeme tutasahau.
Kwamba jeshi ndio wana ufanisi, mbona walifanya ufisadi wa deep green? Pia walihusika na kutorosha madini chini ya ukuta wa mererani. Hakuna jipya hapo
 
Labda Jeshi la Wokovu lakini kama ni hawa Matapeli na majizi ya JWTZ mambo ni yaleyale!.

Hilo jeshi lipo na rasilimali zinaibwa na kutoroshwa nje ya nchi huku Wakuu wa Vikosi wakila kuku na kugonga cheers pale Magogoni ndilo unataka lisimamie masuala ya umeme?

Hebu jaribu kufikiri tena yawezekana unaota!
 
Habari za leo
Kutokana na hujuma zinazoendelea katika Shirika la Ugavi na Usambazaji wa Umeme Tanzania (TANESCO) kwa maoni yangu binafsi nashauri Shirika hili Mkurugenzi Mkuu apewe Mwanajeshi na liwe chini ya usimamizi jeshi.

Sababu kubwa ni uwepo wa nidham ya hali ya juu Jeshini hivyo wataweza kuwajibika na kuzuia michezo inaofanywa na Watendaji wanaohujumu uchumi wa Nchi kwa maslahi ya wachache.

Mfano ni hujuma za kuzuia maji yasijae katika mabwawa mbali mbali licha ya uwepo wa mvua nchini hoja hizi zimetolewa na baadhi ya Wabunge lakini kuna namna zinapotezewa
Hivi akili yako imeshindwa kuelewa kwamba rais ndiyo chanzo cha kukatika umeme?
 
Habari za leo
Kutokana na hujuma zinazoendelea katika Shirika la Ugavi na Usambazaji wa Umeme Tanzania (TANESCO) kwa maoni yangu binafsi nashauri Shirika hili Mkurugenzi Mkuu apewe Mwanajeshi na liwe chini ya usimamizi jeshi.

Sababu kubwa ni uwepo wa nidham ya hali ya juu Jeshini hivyo wataweza kuwajibika na kuzuia michezo inaofanywa na Watendaji wanaohujumu uchumi wa Nchi kwa maslahi ya wachache.

Mfano ni hujuma za kuzuia maji yasijae katika mabwawa mbali mbali licha ya uwepo wa mvua nchini hoja hizi zimetolewa na baadhi ya Wabunge lakini kuna namna zinapotezewa
Ni ujinga kudhani Kila kitu Jeshi linaweza.

Jeshi likishindwa Kuzuia katika katika ya umeme utalikosoa? Tanesco wanahitaji pesa sio swala lakusimamiwa.

Mwisho Jeshi lilisimamia Bandari wakati wa Mwendazake na Tanzanite Merelani,vipi wizi ulikoma?
 
Ujinga ni Mzigo, Akili za Mwendazake izo Kupeleka mpaka Jeshi letu kwenda Kubangua Korosho matokeo yake wote tuliyaona,
Changamoto za Umeme hazipo tanzania tu tuelewe ilo South africa ambae ana total capacity ya 48000MW ana Blackout na Load shedding ambazo zilipelekea mpaka Rais Kuataka kuondolewa ofisini, South wameunda wizara ya Umeme na Kusafisha top layer ya management ya Escom ila still tatizo bado lina persist,
Afu inatakiwa Mjue kuwa Inshu za Umeme ni mambo ya Budget tu Miundo mbinu yetu ni Chakavu sana ivo hapo Mchawi mkubwa ni pesa ila pia msishau Viwanda na Inverstors wamerudi kwa Kasi ambao kipindi cha Mwendazake kipaumbele havikuwa Viwanda na Mostly wali halt their operations ila kwa sasa demand zao ziko Juu na Kuleta scarcity ya Power kwa domestic users ambao ndio wananchi hao au Aka Wanyonge
 
Wafanyakazi wa tanesco wapumzishwe alafu jeshi liwe na kitengo cha umeme wa Taifa.Kuwe na kamandi moja ya umeme ikiwa na wataalamu waliosemeshwa na serikali hapo kama tupo siriazi basi tatizo la umeme tutasahau.

Hakuna kitu kama hiko. Jeshi lina majukumu mengine, labda katiba na sheria mama kuhusu jeshi ziwe bended. Which halitotokea
 
Jeshi lina nidhamu ni kweli
Na amiri jeshi mkuu ni rais ni kweli
Kata umeme kinondoni
Kata umeme Mwananyamala
Kata umeme mwenge
Sawa mkuu na salute juu

Hivi mnadhani ni meneja gani wa TANESCO ambaye ndiyo tatizo katika suala hili la umeme?
Hivi mnadhani ni mkurugenzi gani ni tatizo yani yeye ndiyo chanzo cha haya yote?

Ni waziri yupi anayeajiamulia kwamba umeme ukatwe?
Inawezekana kabisa rais ana kikundi chake cha wachache ambao wanafaidika na kukatika kwa huu umeme

Lalamiko lolote linalohusu umeme liende kwa rais moja kwa moja na siyo kwa mtu mwingine yeyote yeye yuko na majibu sahihi ya nini kinaendelea kwenye umeme

Sababu zao hazina mashiko wala uhalisia
Sababu ya kwanza ilikuwa maji hakuna baada ya kauli hiyo ya hovyo hazikuisha siku tatu mvua kila sehemu ilinyesha mafuriko wakabadili maneno

Rais alitoa kauli ya umeme wa mgao ni hadi miezi sita
 
Back
Top Bottom